Ukiangalia ndoa ya CUF na CCM kule Zanzibar ni vigumu sana kuamini kuwa CUF inaweza kushirikiana na Chadema kwenye kambi ya upinzani. I was skeptical kwa mara ya kwanza nilipoona eti CUF na Chadema watashirikiana. Labda kama CUF ni mbili. Lakini ikiwa CUF ni moja siamini kuwa CUF ile ile inaweza kuwa na alliance na Chadema.
CUF vile vile kwenye bunge la muungano wanajiona kama losers kwani wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party. Wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party kwa Chadema si CCM. Kwa hiyo naturally CUF haiwezi kumpenda Chadema. Hata ukiangalia kwenye uchaguzi, inaelekea strategy ya CUF na CCM ilikuwa inafanana na wameshinda wote maeneo ya pwani. Kwa hiyo in future ukiangalia vizuri kwenye kurunzi, CUF wanajiona kuwa hawako tofauti sana na CCM.
Hata kampeni zao unaweza kuona kuwa CUF hawakuwa against CCM kihivyo.
Jingine ni kuwa CCM wanauona wingi wa Chadema kama threat kwao. Hivyo wako tayari ku-extend mkono kwa chama kingine. Naturally NCCR alikuwa ni direct ally wa CCM. Kampeni za kawe zilithibitisha kuwa NCCR was more against Chadema kuliko against CCM. Hili ni la muda kidogo. NCCR kina MPs wanne tu. Kwa hiyo CCM kumvutia CUF upande wake ni kupunguza nguvu ya upinzani kwani wabunge 45 wa Chadema ukijumlisha na 30 wa CUF, opposition ilikuwa inakuja na wabunge 75. Hiyo si nguvu ya kupuuza kwa CCM hivyo kwao itakuwa vizuri Chadema wakibaki peke yao.
Overall ni kuwa katika Bunge lijalo opposition itakuwa ni chadema peke yao. Na hilo litawajenga zaidi. Hawa wengine kina UDP, TLP, NCCR na CUF obviously watahamia kwa CCM. Pepo zote za kisiasa zinaonesha hivyo.
Baada ya chadema, kutangaza kiongozi wao wa kambi ya upinzani bungeni, vyama vingine vinne vimeamua kuungana na kuwa na kiongozi wao huko bungeni vyama hivyo ni TLP, CUF , UDP NA NCCR MAGEUZI
source TBC1( MUKTASARI WA HABARI)
Nafikiri CHADEMA wanatakiwa kutambua kuwa watanzania wanawaangalia wao kwa uongozi wa upinzani bungeni. Na kiongozi mzuri ni yule mwenye kuunganisha watu wake. Bunge lililopita Hamad alikuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwa nini wasimpe hata umakamu this time?. Mnawakatisha tamaa watanzania kwenye hili na mjue kuwa mvua huwa hainyeshi upande mmoja 2015 inaweza ikanyeshea upande mwingine.
Kumaliazika kwa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao. CCM watatumia miaka mitano hii kuhakikisha CHADEMA kinakuwa hoi kabla ya 2015, believe me CHADEMA onesheni uongozi, acheni ubabe wabebembeleni CUF kwa mustakabali wa CHADEMA 2015
nashukuru mkuu umeiona point, chadema wanajiona vichwa juu kwa wabunge 45 tu wakati cuf in 34. Bunge lililopita chadema walikuwa na 11 na walipewa nafasi ya naibu kiongozi wa pinzani leo cuf in 34 hakupewa hata nafasi ya naibu, eti wamekapa ka-zito, sijui wanakaogopa katavuruga chama? Kusema kweli kama chama kinaweza kuvurugwa na kavulana kama zito, basi hakuna chama hapo na nashukuru mungu hakikushinda uchaguzi. Hata kama kura zilichakachuliwa, zitabarikiwa na mungu, hikichama walahi kingeichakachua nchi nzima kwa ubinafsi. Kueni kwanza (watoto wote mnaoishabikia chadema) mtayaona!
Baada ya chadema, kutangaza kiongozi wao wa kambi ya upinzani bungeni, vyama vingine vinne vimeamua kuungana na kuwa na kiongozi wao huko bungeni vyama hivyo ni TLP, CUF , UDP NA NCCR MAGEUZI
source TBC1( MUKTASARI WA HABARI)
Hawa ndiyo vibaraka wenyewe wa CCM!!! Mbatia alitumwa Kawe aka-dilute Halima Mdee, akakwaa kisiki!!! CUF=CCM, UDP ni kwa yule mzee mapesa ambaye hata kambi ya upinzani ilimvua cheo kwa kuwasaliti aliposhabikia kilimo kwanza ambacho ni siasa za maji taka ambazo hazina resources, hebe leteni wasifu zaidi. Hakuna kitu hapo wakuu. Wanafiki hao tu!! TLP Mrema kule Vunjo kijana wa CCM aliambiwa amsindikize angalao apate ubunge wa kumalizia maisha!!!! Ni kiinua mngongo cha kazi yake kubwa ya Usalama wa Taifa na amehitimisha vizuri kwa kuua vyama na upinzani wenye nguvu!!! Wewe sikiliza kauli za Mrema ndipo utagundua kuwa si Mwanamapinduzi wa kweli.
CUF wanafiki si mnamuona maalim seif anachekelea kabisa tofauti ya 0.1% hata hajalalamika faster kakubali matokea, sasa hivi hao ni nyumba ndogo ya MCC.
Chadema tusimame kwa miguu yetu yenyewe, at the end of the day sisi ndio wapinzani halisi, na wananchi tuwape Support viongozi wetu.
Siasa kijana hizo! 1978 wakati wa vita ya Kagera Gadaffi alikuwa adui yetu namba 2 kwa vile alikuwa anamsaidia Amin vifaa na askari. Lakini nini kilitokea baadae? Huyo huyo Gaddafi na serikali yake wakawa marafiki wakubwa wa serikali ya CCM na misaada kibao mkapokea mpaka mafuta ya bure mlijichotea. Hivyo katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu muhimu malengo yenu ya wakati huo na ujao.Naona miguu yenu imeshindwa kuhimili mizigo na sasa mnaomba msaada wa miguu ya wenzenu