Bungeni: TLP, CUF, UDP na NCCR Mageuzi navyo vyaungana

Hujaeleza iweje kama wengine hawataki kuwa katika alliance! Maana kumbuka hili linawezekana. Kwa kuwa Chadema ndiye main opposition party na ndiye anawaalika wapinzani wengine kujoin upinzani bungeni sasa mbona hamuelezi ikiwa vyama vingine havitaki iweje? You people? Msiandike tu kabla ya kufanya utafiti angalau mdogo!

Unajua maana ya wesminster? inakuwaje?
 
quote_icon.png
Originally Posted by Zawadi Ngoda
Mawazo finyu.

Hakuna hoja ya kujibu kwani ni mbwe mbwe tupu.

Makubaliano ya vyama vya siasa ni kitu cha kwaida kabisa duniani na yametokea pengi ikiwemo pamoja na CHAMA CHA mUGABE NA SHANGIRAI.

Na ni kwa sababu hizo uzisemazo ndio vyama vya upinzani vinashindwa kuungana au kwa lugha sahihi si kuungana bali kuwa na lao moja au kushirikiana kama ukipenda. Woga eti chama kimoja kitamezwa na kingine.

Angalia CHADEMA wameshindwa hata kukipa chama kingine nafasi ya ukatibu katika kuongoza upinzani.
Kama makubaliano ya vyama ni kitu muhimu kwa nini CCM hawajakaa na Chadema na wakawa na makubaliano?
Kama kutoa ukatibu kwa chama kingine wewe umeona ni issue mbona CCM haijatoa kwa chadema? wewe hujui lolote kaa kimya wewe ni low thinker!
Post zako zinadhihilisha ujinga ulio kichwani mwako. Unaandika vitu kama mtu aliyetoka usingizini. Ndio sababu imesemwa mara nyingi kwamba post zako ni uoza tu.
 
Tulisema hao ni CCM-B mkakataa sasa mnajionea? NCCR-MANUNUZI ndiyo hovyo kabisa, CUF wao wana muafaka na CCM kwa hiyo "technically" CUF sio wapinzani. TLP na UDP njaa tu inawasumbua.

Unajua maana ya wesminster? inakuwaje? au unabwabwaja tu?
 
For your information, Mh. Mbowe ,mwenyekiti wetu wa chadema, alifanya mazungumzo ya kina na uongozi wa CUF akiwaomba washirikiane kuunda kambi ya upinzani, cha kushangaza, wenzetu wa CUF wakampa masharti magumu, kwamba ni sharti washirikishe vyama vingine, NCCR,TLP na UDP ambavyo kwa kweli kila mtu ana wasiwasi mkubwa na intergrity ya vyama kama TLP cha bwana mrema. hilo ndo likawa kikwazo, na ndio chanzo cha chadema kuunda rasmi kambi yao ya upinzani, official opposition party. hakuna jinsi mapambano yatasonga tu, tunao makamanda pale ,kila kitu kitakuwa safi usihofu.

Unajua maana ya wesminster? inakuwaje? je inashirikisha vyama vingine?
 
CUF ndio kimesaidia Chadema kukua Chadema kuvipoteza vyama vya upinzani kwenye ramani

Heshima zenu wanajf,

Poleni kwa majuku ya kila siku na pirika za uchaguzi ambao kwa kiasi kikubwa umeonyesha matumaini kwa kuwezesha vyama vya upinzani kuwa na uwakilishi mkubwa ndani ya bunge la 10. Lakini kwa wale ambao sio wanazi wa chama chochote na wapenda maendeleo watakumbuka jinsi chama cha CUF kilivyoisauidia Chadema kujulikana kwenye ramani ya Tanzania kupitia kuishirikisha kwenye KUB.

Wasiokuwa wanafiki watakumbuka nafasi ya Zitto kwenue KUB 2005 - 2010 na John Cheyo wa UDP. Na wasikuwa na ubongo wa kuku wa kusahau kwa kutumia BUK Chadema walikuwa na uwanja mzuri wa kutoa hoja na kujenga kuaminiwa na wananchi. Kwa maana hiyo basi sisi tusiokuwa wanazi hatujapendezewa na habari ya Chadema kuchukua nafasi zote za KUB na kutaka kuungwa mkono na vyama vilivyobakia kinadharia na sio kuwashirikisha kwenye maamuzi ya kamati mbalimbali. Huu ni ubinafsi na unatakiwa kukemewa kwa nguvu zote kwa wale wanaopenda mageuzi ya kweli na sio kuweka mapenzi ya vyama na kuviita vyama vyengine CCM B sijui CCM Y !!!!

Hali hii sio nzuri kwa Chadema na wanaitakia mema Chadema kwenye hili mmeteleza na watanzania wenye weledi wa kuchambua mambo wanaliona hili ni tatizo hivi mmepata 12% mnasahau fadhila na mshikamano mliopewa mlipo kuwa na wabunge watano mtakumbuka fadhila za wapiga kura?

Napenda niishie hapa kwa msisitizo Chadema mmeonyesha uchu wa madaraka na hili ni jambo baya sana kwenye demokrasia ikizingatiwa mnajiita nyie ni chama cha demokrasia sijui ni demokrasia gani nyie mnailewa zaidi kuliko sisi maana tumeona Zitto na Mbowe wakitunishiana misuli kwenye KUB.

Kabla ya kusema shukrani napenda niweke hii habari iliyonisikitisha na kunitoa chozi kwa jinsi watu walivyokuwa na uchu wa madaraka.


Upinzani watofautina bungeni

Thursday, 11 November 2010

Boniface Meena na Habel Chidawali, Dodoma


VYAMA vya upinzani vimemeguka bungeni baada ya Chadema kuchukuanafasi zote za juu za uongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni bila kuvihusisha vyama vingine.

Baada ya Chadema kutangaza jana kuwa imewateua Freeman Mbowe, Zitto Kabwe na Tundu Lissu kuwa viongozi wake wakuu bungeni, vyama vyama vya CUF, TLP na NCCR Mageuzi, viliamua kuunda kambi nyingine ya upinzani isiyorasmi.


Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge wa Chadema, John Mrema aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa chama hicho kimemteua Mbowe kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Naibu wake ni Zitto na Tundu Lisu anakuwa Mnadhimu Mkuu.

Mbowe ni Mbunge mteule wa jimbo la Hai, Zitto Kigoma Kaskazini na Tundu Lissu, Singida Mashariki.


"Tuna asilimia 12.5 ya wabunge na hiyo inatupa nafasi ya kuunda kambi ya upinzani bungeni," alisema Mrema.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kambi ya upinzani bungeni, Mrema alieleza kuwa amepata taarifa kuwa CUF kimeungana na NCCR Mageuzi na TLP kuunda kambi yao.


Mrema alisema CUF kimewaeleza kuwa kimeunda kambi yao kwa kushirikiana na NCCR-Mageuzi na TLP.


"Sijui wanaunda kambni gani, lakini Hamad Rashid ametueleza kuwa wao wameungana na NCCR na TLP kuunda kambi yao," alisema Mrema.


Kauli hiyo ya Mrema iliungwa mkono na aliyekuwa Kiongozi wa Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed aliyesema kuwa CUF imeamua kuunda kambi yao inayojulikana kwa jina la ‘Minority opposition' ambayo ina viongozi wake.


"Kama baadaye wenzetu wa Chadema watataka tushirikiane tutafanya hivyo, lakini hiyo ndiyo kambi yetu tuliyoiunda," alisema Hamad na kufahamisha kuwa yeye ndiye kiongozi wa kambi hiyo.


Alisema kambi hiyo inaongozwa na yeye (Hamad) kama mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti ni Khalifa Suleiman na Katibu Mkuu ni David Kafulila wa NCCR.


Kwa mujibu wa Hamad, CUF imeamua kuunda kambi yake kwa kuwa Chadema kimetangaza kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni.


Kitendo cha kuunda kambi mbili za upinzania bungeni kinaonyesha kuwa bado kuna tatizo la ushirikiano miongozi mwa vyama hivyo, ambavyo vimekuwa vikivutana kwa muda mrefu kuhusu kuunganisha nguvu.


Mgororo huo umesabisha kutoshirikiana wakati wa uchaguzi, ambapo kila chama husimamisha mgombea wake katika majimbo ambayo chama kimojawapo kina nguvu zaidi.


Utengeno huo umesababisha vyama hivyo kupoteza ushindi dhidi ya CCM kwa kugawana kura, kama ilivyotokea Tarime mkoani Mara katika Uchaguzi Mkuu uliopita.


Katika jimbo hilo ambalo ni ngome ya Chadema, chama hicho kilimsimamisha Mwita Waitara na CUF walimsimamisha Charles Mwera aliyekuwa mbunge wa Chadema, lakini aliunguliwa wakati wa mchakato kuteua wagombea.


Hatua hiyo ilisababisha wagombea hao kugawana kura ambazo zingejumlishwa zingewezesha jimbo hilo kuwa mikononi mwa Chadema, lakini likaenda CCM.


Pia katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijini mwaka mapema mwaka jana CUF ambayo haikuwa na nguvu Mbeya Vijijini ilimsimamisha mgombea na kuvishawishi vyama vingine kukiunga mkono.


Katika uchaguzi wa mwaka huu, Chadema nayo ilisimamisha wagombea katika majimbo yote ya mikoa ya Kusini mwa Tanzania ambako ni ngome ya CUF.

MOD: Huu nui mchango wanu napenda uwe wangu na ondoa ushabiki kuweka kapuni hii kitu :mad:

Kuwa na mawazo mapana wewe, unataka CHADEMA wafanye nini? CHADEMA ndiyo chama chenye wabunge wengi ukilinganisha na CUF, kwa hiyo walikuwa na haki ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Kuhusu suala la CUF, CHADEMA waliwasiliana nao wakasema tupo tayari kuwa pamoja, ambapo CHADEMA waliwaambia kiongozi mkuu atatoka chadema na vilevile CUF watashirikishwa kama walivyo washirikisha kwenye bunge la 9. Cha ajabu ni kwamba baada ya masaa machache CUF wakatoa tamko kuwa wao hawataungana na CHADEMA, bali watakuwa na kiongozi wao wa upinzani.
Kwa ajili hiyo wewe Sokomoko ulitaka CHADEMA wawalambe miguu hawa wajinga? Nani hajui kuwa CUF ni 2nd ruling party?
 
Vyama vya upinzani vinatofautiana sana na ndiyo maana vipo vingi. CUF wanajisahau sana na kuanza kucheza ngoma za CCM hawajui mwisho wa siku watakuwa wamemezwa na watanzania watakuwa wametoswa kwa interest za watu wachache. Kisiwaumize vichwa kwanini CUF na NCCR (Maana TLP na UDP ni majenshi ya mtu mmoja mwenyekiti tu akitoka kwisha habari) wamegoma kuungana na Chadema bali angalieni wabunge tuliowachagua watakwenda kuwawakilisha vipi bungeni na vitu gani vyenye maslahi kwa Taifa watakwenda kuvisimamia. Kwa mtizamo wangu kuna wabunge wa CCM wenye msimamo thabiti kuliko baadhi ya wabunge na viongozi wa vyama vya upinzani.
 
Mimi huwa naifagilia CHADEMA kwa mambo mengi sana ila wakti mwingine penye kasoro lazima Tusemme. Kwa hiyo na mimi Ntasema maana nisiposema wengine watafikiri kumbe MAGEUZI NI CHADEMA CHADEMA na yeye. Napenda kusema kwa hapa CHADEMA wamechemsha kidogo. Lazima tuwe wakweli wakati mwingine. Nafikiri CHADEMA wanatakiwa kutambua kuwa wananchi wanafuatilia mambo ya CHADEMA hatua kwa hatua. Hii ni kwa sababu wengi wa wananchi wanaamini CHADEMA ndio itashika hatamu 2015. Sasa nawasihi CHADEMA wasiharibu fursa hii. Watambue kwamba uongozi mzuri ni kuunganisha watu . Ninachosikitika ni kwamba msuguano kati ya ZITTO na FREEMAN pia unachangia kudidimiza CHADEMA. Tuchukue mathalani kama si huu msuguano leo Hii Mbunge mteule wa Kigoma Kusini (NCCR) David Kafulila angekuwa Chadema. Lakini sababu ya misuguano wakampoteza!!!!!!!!!!!!!! Chonde chonde CHADEMA chama chetu tarajiwa. Msichezee fursa. Mafisadi(MAFATAKI) wanawamezea mate kama vile. Mapedeshee wanavyomezea mate vibinti Vidogo ambavyo ndo vimebalehe!
Bunge lililopita Hamad alikuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwa nini wasimpe hata umakamu this time?. Mnawakatisha tamaa watanzania kwenye hili na mjue kuwa mvua huwa hainyeshi upande mmoja 2015 inaweza ikanyeshea upande mwingine. Kama itawezekana ndugu zangu Chadema Mfanye namna baada ya Muda kuwe na Bubadilishana Umakamo wa Kiongzi wa kambi ya Upinzani bungeni. Kumbukeni
Kumaliazika kwa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine. CCM watatumia kipindi hiki kabla ya 2015 kuhakikisha CHADEMA inayumba na ikiwezekana inabakia ikiwa hoi.
 
nafikiri chadema wanatakiwa kutambua kuwa watanzania wanawaangalia wao kwa uongozi wa upinzani bungeni. Na kiongozi mzuri ni yule mwenye kuunganisha watu wake. Bunge lililopita hamad alikuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwa nini wasimpe hata umakamu this time?. Mnawakatisha tamaa watanzania kwenye hili na mjue kuwa mvua huwa hainyeshi upande mmoja 2015 inaweza ikanyeshea upande mwingine.

Kumaliazika kwa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao. Ccm watatumia miaka mitano hii kuhakikisha chadema kinakuwa hoi kabla ya 2015, believe me chadema onesheni uongozi, acheni ubabe wabebembeleni cuf kwa mustakabali wa chadema 2015

nafikiri wewe hufuatilia masuala vizuri , mbowe alikuwa wa kwanza kumkaribisha hamda kuunda kambi ya upinzani, ma cuf waliahidi kuungana. Lakini si unajua tena lobbying mara tukasikia cuf hawataki kushurikiana. Ndio sasa wameunda kambi yao.

Lakini si ndio demokrasia jamani. Kama wametimiza masharti si ya kuwa na viti 38 tuwaache watumie uhuru wao. It is the content and not the quantity that matters with ccm tearing oppositiuon apart. Kitu ambachp mlikuwa hamjui ccm hufanya research kweli kweli, ni ushindi huu wa chadema walikwisha uanticvipate ndio maana ya kujnganisha nguvu na cuf.


kwani mmesahau hata 2005 cuf kwanza waliunda serikali hiyo peke yao, thena wenyewe wakajirudi na kuwashirikisha wengine? Kwa sasa majority ya wabunge iwe wa chadema au cuf bado hawajapata mzigo hasa wa kuwa kambi ya upinzani. kutayarisha all the necessary ingridients k.m bajetiu kivuli n.k tena bila ya kuwa na resources kama vile manpower etc walizo nazo chama tawala. Lets wait and see.

all in all chama tawala kikianza kuunganisha nguvu na vyama vya upinzani si ndio dalili za mabadiliko, kwani mlitakaje?
 
Kuwa na mawazo mapana wewe, unataka CHADEMA wafanye nini? CHADEMA ndiyo chama chenye wabunge wengi ukilinganisha na CUF, kwa hiyo walikuwa na haki ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Kuhusu suala la CUF, CHADEMA waliwasiliana nao wakasema tupo tayari kuwa pamoja, ambapo CHADEMA waliwaambia kiongozi mkuu atatoka chadema na vilevile CUF watashirikishwa kama walivyo washirikisha kwenye bunge la 9. Cha ajabu ni kwamba baada ya masaa machache CUF wakatoa tamko kuwa wao hawataungana na CHADEMA, bali watakuwa na kiongozi wao wa upinzani.
Kwa ajili hiyo wewe Sokomoko ulitaka CHADEMA wawalambe miguu hawa wajinga? Nani hajui kuwa CUF ni 2nd ruling party?

Hakuna habari sehemu yoyote CUF kujitoa zaidi ya humu JF na hii inaletwa kwa kusudi maana humu ndani suala la great thinkers limeshaondoka tumebakia washabiki wa vyama tu!
 
2005 cuf ilipata ridhaa ya kuunda serikali kivuli ndani ya bunge, walipoanza walitwaa nafasi zote wao bila kumshirikisha mpinzani mwingine yeyote, hamad rashid akiwa kiongozi wa kambi hiyo akajikuta anapwaya ndani ya bunge especially pale wabunge wa chadema walipoonyesha ukomavu kwa hoja binafsi na taratibu kujijengea umaarufu ndani na nje ya bunge, ndipo wakawaomba waungane nao ktk vita dhidi ya sirikali, chadema wakaridhia. Wana jf jikumbusheni siku hamad rashid alipobadili baraza lake kivuli alisemaje.

Chadema wako sahihi this time, wameingia bungeni wakiwa watu timamu kitu ambayo cuf tangu 1995 hawajawa nacho.
 
nafikiri wewe hufuatilia masuala vizuri , mbowe alikuwa wa kwanza kumkaribisha hamda kuunda kambi ya upinzani, ma cuf waliahidi kuungana. Lakini si unajua tena lobbying mara tukasikia cuf hawataki kushurikiana. Ndio sasa wameunda kambi yao.

Lakini si ndio demokrasia jamani. Kama wametimiza masharti si ya kuwa na viti 38 tuwaache watumie uhuru wao. It is the content and not the quantity that matters with ccm tearing oppositiuon apart. Kitu ambachp mlikuwa hamjui ccm hufanya research kweli kweli, ni ushindi huu wa chadema walikwisha uanticvipate ndio maana ya kujnganisha nguvu na cuf.


kwani mmesahau hata 2005 cuf kwanza waliunda serikali hiyo peke yao, thena wenyewe wakajirudi na kuwashirikisha wengine? Kwa sasa majority ya wabunge iwe wa chadema au cuf bado hawajapata mzigo hasa wa kuwa kambi ya upinzani. kutayarisha all the necessary ingridients k.m bajetiu kivuli n.k tena bila ya kuwa na resources kama vile manpower etc walizo nazo chama tawala. Lets wait and see.

all in all chama tawala kikianza kuunganisha nguvu na vyama vya upinzani si ndio dalili za mabadiliko, kwani mlitakaje?

Unapotumia system ya wesminsterutashirikiana vipi na wenzio au mmewaona wao watoto? acheni ushabiki utauwa chama!
 
2005 cuf ilipata ridhaa ya kuunda serikali kivuli ndani ya bunge, walipoanza walitwaa nafasi zote wao bila kumshirikisha mpinzani mwingine yeyote, hamad rashid akiwa kiongozi wa kambi hiyo akajikuta anapwaya ndani ya bunge especially pale wabunge wa chadema walipoonyesha ukomavu kwa hoja binafsi na taratibu kujijengea umaarufu ndani na nje ya bunge, ndipo wakawaomba waungane nao ktk vita dhidi ya sirikali, chadema wakaridhia. Wana jf jikumbusheni siku hamad rashid alipobadili baraza lake kivuli alisemaje.

Chadema wako sahihi this time, wameingia bungeni wakiwa watu timamu kitu ambayo cuf tangu 1995 hawajawa nacho.

Hamtaki kuwapa fursa watu kama kina kafulila mnajua mtawajengea umaarufu zaidi chama cha chadema ni cha majungu kama vyama vyengine tu na viongozi wake ni wabinafsi bora nisishabike chama nibaki mtu huru maana hakuna kabisa mwelekeo kila chama kina udhaifu na udhaifu wa chadema umeshaoneka ni madaraka ole wetu tuje tuwape nchi mamamamamamamama hehehehehe tutajuta majuto ya mbwa!
 
mimi huwa naifagilia chadema kwa mambo mengi sana ila wakti mwingine penye kasoro lazima tusemme. Kwa hiyo na mimi ntasema maana nisiposema wengine watafikiri kumbe mageuzi ni chadema chadema na yeye. Napenda kusema kwa hapa chadema wamechemsha kidogo. Lazima tuwe wakweli wakati mwingine. Nafikiri chadema wanatakiwa kutambua kuwa wananchi wanafuatilia mambo ya chadema hatua kwa hatua. Hii ni kwa sababu wengi wa wananchi wanaamini chadema ndio itashika hatamu 2015. Sasa nawasihi chadema wasiharibu fursa hii. Watambue kwamba uongozi mzuri ni kuunganisha watu . Ninachosikitika ni kwamba msuguano kati ya zitto na freeman pia unachangia kudidimiza chadema. Tuchukue mathalani kama si huu msuguano leo hii mbunge mteule wa kigoma kusini (nccr) david kafulila angekuwa chadema. Lakini sababu ya misuguano wakampoteza!!!!!!!!!!!!!! Chonde chonde chadema chama chetu tarajiwa. Msichezee fursa. Mafisadi(mafataki) wanawamezea mate kama vile. Mapedeshee wanavyomezea mate vibinti vidogo ambavyo ndo vimebalehe!
Bunge lililopita hamad alikuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwa nini wasimpe hata umakamu this time?. Mnawakatisha tamaa watanzania kwenye hili na mjue kuwa mvua huwa hainyeshi upande mmoja 2015 inaweza ikanyeshea upande mwingine. Kama itawezekana ndugu zangu chadema mfanye namna baada ya muda kuwe na bubadilishana umakamo wa kiongzi wa kambi ya upinzani bungeni. Kumbukeni
kumaliazika kwa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine. Ccm watatumia kipindi hiki kabla ya 2015 kuhakikisha chadema inayumba na ikiwezekana inabakia ikiwa hoi.

acha kualamikia maji yaliyokwisha mwagika, siasa ndio ilivyo haina madui wa kudumu wala marafiki wa kudumu lyatonga mrema, dr slaa, shibuda na wengine walitoka ccm na kuhit katika upinzani nao walisababiswha na zitto na mbowe, lazima utambue kuwa sasa chadema is growing ni lazima ikumbane na misuokosuoko. Tatizo la watu humu ni kutaka mkuingilia shughuli za viongozi wa chadema kwa kila jambo. Ni lazima tujifunze kuheshimu maamauzi ya viongozi tuliowachagua unless we have very strong grounds of raising our voices.

Inaonekana wengi wa wtu humu ndani ndio kwanza wanatolewa pampers za kisiasa hivyo wanareact mapem kwa kila jambo.
 
Tatizo ninaliona hapa ni muafaka wa CCM na CUF Zanzibar, wabunge wengi wa CUF wanatokea Zanzibar, sasa watu wanahiyo utakuwaje na mkakati wa pamoja, wameonyesha kwenye kura za Uspika wampa Makinda badala ya Marando.
 
hamtaki kuwapa fursa watu kama kina kafulila mnajua mtawajengea umaarufu zaidi chama cha chadema ni cha majungu kama vyama vyengine tu na viongozi wake ni wabinafsi bora nisishabike chama nibaki mtu huru maana hakuna kabisa mwelekeo kila chama kina udhaifu na udhaifu wa chadema umeshaoneka ni madaraka ole wetu tuje tuwape nchi mamamamamamamama hehehehehe tutajuta majuto ya mbwa!
tatizo lako unajikita kwenye personalities zaidi instead of issues
 
Nimeamini kweli CUF wako kwa maslahi ya wazanzibari, akina lipumba hawana lolote wamewekwa kama picha tu,kwakuwa CCM na CUF visiwani wamekubalina kuongoza pamoja kwa ajili ya uzalendo wa nchi yao,ulitegemea Hamad Rashid atasaliti nchi yake? sisi tunahitaji kujua kwamba lazima tuwe na sisi kitu kimoja kwa maslahi yetu,mmesikia rais wa zanzibar amesema Zanzibar kwanza! akina Mrema na mbatia Njaa tu zinawasumbua sio wapinzani hao.
 
kusema ukweli CUF sio wapinzani sababu wao wameshirikishwa kwenye serikali huko ZNZ. wanaweza kabisa wasi-support UPINZANI kwenye baadhi ya mijadala mikali inayogusa serikali. Naunga mkono CHADEMA ku-form upinzani peke yao bungeni; they are real front fighters agaist the evils ufisadi, rushwa, uchakachuaji, n.k. BRAVO CHADEMA!!
 
Baada ya kupitia pitia JF, imegundulika kuwa Chadema imejiweka kuwa ndio wapinzani hapa Tanzania na yeyote mwenye maoni tofauti na ya Chadema basi ni CCM. Ya nini kufanya ushirika na anayejikweza kuunda jambi ya upinzani bungeni?
Ebu angalia na maoni ya huyu!!!!! mi nadhani mkikosa ya kuandika unyamaze. Kwani ni lazima uandike kitu hapa jf?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom