Bungeni: Serukamba aomba radhi

Bungeni: Serukamba aomba radhi

Hatimae Tundu lisu atolewa nje ya bunge kibabe.
 
Halafu hawa si ndio wanapinga Big Brother! Haya wanafanya huko bungeni yanafanana kabisa na ya BBA
 
Naangalia bunge sasa hivi..Selukamba kasimama na kuomba radhi kwa maneno aliyotoa mchana.
Wenje nae kaomba muongozo kwa Ndugai..akirejea agizo la Makinda jana kwamba mbunge yoyote atakayetukana atatatolewa nje na polisi. Na anasema Selukamba katoa tusi kubwa kuliko matusi yote yaliyowahi kutolewa bungeni.
Ni matusi gani Selukamba katukana..mliosikia tafadhali mtujuze.

Alitukana akasema, "---- you"
 
Hahahah sisi huwa tunasema "Afyulile"...

Hahahaa, ni sawa na huku kwetu Sikonge, mtoto akiachia uchuzi wakati wa Chakula na anasema "Kimeniponyoka".

Ila kwa Kinyamwezi huwa ina-Sound vizuri sana. Sasa sijui yeye kaomba msamaha kwa lugha gani.

Kinyamwezi angelisema "Kanfyumpuluka......"

Kaunga , KIKUNGU , @ELNINO , St. Paka Mweusi ,na wengine mnasemaje? Nimepatia?
 
Kumbe huyu mh. Anama2c ndo mana amesema limemtoka kwa bahat mbaya.
mh bahati mbaya wapi mtu akishazoea matusi hutukana ovyoovyo
lakini ustaarabu ukiwa nao kamwe huwezi kutukana kwa bahati mbaya kwa sababu hata tusi kuelea kichwani kwako haiwezekani.
 
Ktk kikao cha bunge cha jioni hii mbunge peter serukamba aomba radhi kwa tusi alilolitoa bungeni mchana,kuwa lilimtoka kwa bahati mbaya!

Binafsi sichukui hii kitu nitaendelea kumuona Serukamba kama mwehu,mhuni tu asiyefaa kuwepo bungeni!! hakujua kama yuko bungeni? kumtoka bahati mbaya maana yake nini? mbona mk**o haukumtoka bahati mbaya?
 
Ktk kikao cha bunge cha jioni hii mbunge peter serukamba aomba radhi kwa tusi alilolitoa bungeni mchana,kuwa lilimtoka kwa bahati mbaya!
Ganja bwanaaa....duuh!!! Hizi bar zote karibu na ukumbi wa bunge zihamishiwe mbali.
 
Naomba bunge letu lifikie hatua kama ya Venezuela na Ukraine ambako hata makofi huwa yapo! Bila hivyo adabu haitakuja humo ndani.
 
Hakutolewa nje kwa kutukana msamaha ndo umsafishe,hizi nyenzo za kina LUSINDE nazo tabu tupu
 
huwezi ukatokwa na kitu usichokuwa nacho, hicho ndicho kilichokuwa ndani ya Serukamba amebanwa na amekitoa
 
Hivihivi asamehewe wakati wengine wamekula ban bila kufuata kanuni za bunge?
 
Back
Top Bottom