WA-UKENYENGE
JF-Expert Member
- Oct 1, 2011
- 2,918
- 1,236
Na bunge ni sehemu nyeti sana ya nchi, tena yenye kutolea maamuzi mazito. Hii anatakiwa awajibike zaidi siyo kusema tu samahani. Pengine, iwe ndo mwanzo wa sheria kali dhidi ya watumia lugha chafu sehemu za public kama hizo.Mimi hainiingii akilini kwamba unatukana matusi ya nguoni kisha unaishia kuomba radhi tu basi!! Mtu unafahamu kabisa kwamba hili ni tusi lakini unaenda nalo kwa kujua tu kwamba nitasema samahani?!
Sasa bunge limegeuka kuwa kichaka cha watu kutukanana na kutukana. Demokrasia sasa inakuwa karaha.