Foum Jnr
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 272
- 132
Upigaji wa kura wa siri ndio suluhisho pekee litakalowapa uhuru wajumbe kufanya maamuzi bila ya shinikizo au vitisho. Khofu hasa ya nini kushinikiza watu kupiga kura kwa uwazi huku tayari mushaweka vitisho vya kuwafukuza, na kuwa brand wasaliti? Hivi tumeamua kubadili katiba ili kunyosheana vidole baada ya mabadiliko au kufuta uhasama na kuanza chapter mpya ya maendeleo?
Kama kawaida hoja ziszo na mashiko kulifananisha bunge la marekani na la Tanzania maana sijawahi kuona kura za kumchagua house speaker wa marekani kuzidi wajumbe wenyewe. Tusijitie upofu tukasahau kwamba uoza wa rushwa, vitisho na lack of ethics ndio hasa chanzo cha bunge letu likawa bovu lenye kubeba wingi wa maslahi binafsi ya posho badala ya agenda ya mabadiliko ya kweli yenye asasi ya wananchi na maendeleo yao.
Tatizo letu ni kuzowea fitna, kunyosheana vidole na kuziba demokrasia ya uhuru wa mtu kuwa na kauli yake bila ya shinikizo. Hivi umeona wapi katika mazingira magumu kama ya sasa halafu tukaweka wazi kura ambazo zinakila ya dalili ya kuwa patronise na intimidate wajumbe kukubali wasioyaamini. Napolean naye pia aliwahasisha wafaransa kukubali mfumo wa kupiga kura kwa uwazi lakini wananchi waligoma kwa sababu bias ya kura za kuonekana hazitakuwa na uzito wa legitimacy ya kweli kwa wapigaji. Hivi hasa munakusudia kuwafanya nini wale ambao watakwenda kinyume na itikadi zenu hata mushadidie kura za uwazi?
sasa kuna wimbi la uhalifu mkubwa wa wanaomwagiwa acid n.k kwa vile tu wanamitazamo tafauti sasa munachokitaka kukifanya hamuoni kwamba munawaweka wajumbe katika hali ya hatari pale bunge linapomalizika na wenye visasi kuwasubiri kwa kuwahujumu? hamuoni kwamba uwazi wa aina hii unaweza kuzua balaa katika jamii na hata kuondosha hali ya utulivu tulionayo? Hivi uwazi wa kura unafaida gani kubwa zaidi ya kuwafitinisha watu kwa sababu ya mitazamo tafauti?
Lengo la kura yoyote ni uhuru wa kuamua ulitakalo bila ya intimidation, threat na bias. faida ya kura ya siri ni kwamba hasa katika kura ya kubwa ya katiba ni kuhakikisha beyond any reasonable doubt wajumbe wanafanya maamuzi yalio moyoni mwao na kama rais alivyosema hakuna haja ya vitisho, ngumi na kunyosheana vidole, kikubwa ni hoja. Kwa nini hasa watu wasijikite katika hoja badala ya hii hamkani ya demokrasia ya punishment ya kura za wazi au masuala ya kusomeana halbadiri?
Bunge lisiendeshwe kienyeji enyeji, hivi tuseme kura za wazi tutaziita ni uhuru wa kweli? Tunahofu nini hasa hata tukashindwa kutumia common sense katika suala kubwa na zito kwa taifa? Hoja ya kwamba suala hili ni la kitaifa na ni vyema watu wakawa mashujaa na kuwa wawazi katika kura ni hoja dhaifu, maana hakuna nafasi kubwa katika nchi kuliko hio katiba kama nafasi ya Rais na madaraka makubwa aliopewa nayo including kulivunja bunge na kuunda bunge jengine bias litakalofuta katiba na kumpa inayomfavour, lakini hatupigi kura ya uwazi bali ya siri. hata hao wajumbe wa hilo bunge nao pia hupigiwa kura ya siri na ndio sasa wanamamlaka ya kubadili katiba sasa kwa nini tusingewapigia kwa uwazi.
Misingi ya demokrasia iko wapi? tumekuwa na kangaroo courts zisizojali maadili, bunge dhaifu la wapenda posho, nahata hili la kura nalo litiwe dosari kwa kuhalalisha kisichotakiwa na wananchi? wengi tulitarajia lengo la katiba mpya ni kuanza chapter mpya ya maendeleo na kusahau yaliopita, hivi hii nia tunayo kweli wakati dalili za makusudi za kuwekeana visasi zinatunzwa ati kwa misingi ya national interests, hivi jamani tumekusudia kuipeleka wapi hii nchi. Wapeni haki na dhamana tuliowapa kwa kuwaachia kila mjumbe uhuru wake wa kura ya siri ili tuweze kupata katiba ilio bora na yetu sote.
Kama kuna umuhimu wa kura za uwazi, mungelianza basi kati chaguzi za vyama vyenu kuanzia nafasi ya Mwenyekiti na kuendelea. Kwani kisa cha kura za maruhani zilianza vipi? Hebu kuweni sensible na muwache huu utoto sasa.