Bungeni: Mbowe aweka msimamo wa posho

Mbowe safi sana. Kwa maneno tu CHADEMA ipo juu. Suala utekelezaji sasa!!! Hivi KUB- Mbowe amepewa aina gani ya gari na serikali? Akiwa shujaa aliache achukuwe RAV4. Mbowe na wabunge wengine wa CHADEMA waungane na Zitto waache kupokea posho. Huo utakuwa ushujaa lakini ushujaa wa maneno mimi siutaki. Shujaa ni Zitto tu hapo ndio ananena na kutenda.

Mimi bado naamini kuwa posho za vikao siyo stahili halali lakini sasa tuzikatae kwa vitendo. Mimi kuanzia sasa hivi sitaki na sichukui posho za vikao naungana na Mh. Zitto kwa maneno na kwa vitendo. Mbowe na wengine naomba tuungane kwa maneno na kwa vitendo pia.
 
Huwez amin kwa mara ya kwanza leo ameongea mpinzani ukumbi mzima ulikua kimyaaa!. Hadi niliona kama muda wamempa mchache vile? Maana mpaka ye mwenyewe akatingisha kichwa alipoambiwa muda umekwisha.
Huyu jamaa ni kichwa sana!
 
Yaani tunapewa msaada na wafadhili, wakija kukagua miradi mpaka wanatushangaa magari ya kifahari wakuu wetu wanayotembelea. Wakat wao wanatembelea Land Cruiser viongoz wa Tz wanatembelea Vx.
 
crappppppp
 
Nimemsikiliza Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe. Kwa kweli alichokiongea naweza Kusema Amefunga Bunge la kumi (10), bila shaka kuna watu machozi yamewatoka. Ni Misumari ya Moto mwenye Macho haambiwi Tazama

Huyu jamaa ana uchungu wa kweli na watanzania kwa sababu yeye hagangi njaa pale bungeni . Nimemsikiliza vizuri na bunge zima lilikaa kimya kwani alishusha pointi zenye mguso wa kweli na sio ushabiki wa kisiasa na nilimwona wassira, Vuai, Nundu na Ngeleja wakimeza mate kusema naaam huku wakielekeza vichwa chini kwa aibu.

Nilifurahi aliposema viongozi wengi wa serikali wanatumia fedha nyingi wanapokuwa ktk ofisi za umma kitu ambacho hakuna anayeweza kufanya akisha staafu. kwa mfano akauliza key issue hizi:

1. Je ni nani hapa akiisha staafu anaweza safiri na first class au business class kwenda nje ya nchi na kusema wengine hata kupanda ndege baada ya kustaafu ni shida ila wako tayari ku-mis use fedha za umma akiwa ofisini.
2. Ni nani anaweza nunua landcruiser mpya baada ya kuacha kazi ofisi ya umma
 
kuhusu huyo mbunge ni kweli mimi mwenyewe nimesha mtengenezea computer zake kulipa shida ni kweli wanakuwa na hali mbaya sana hata ofisini kwake ukiingia jamani ukiambiwa alikuwa mbunge uwezi kuamini
 

Hayo ndiyo marupurupu na makandokando ya ajira serikalini!!
 
Kama Arcado Ntagazwa, ana ki Mark II chake kimechokaaaaaa! Anapiga mizinga hadi petrol
 
dah! kwa kweli inaniuma kuona baadhi ya viongozi wachache katika nchi iliyo masikin kama Tanzania wakisimama na kutaka kulipana posho zisizo za msingi ili hali wananchi hawana hata uhakika wa kupata chakula nadhani zama za mapinduz zimewadia watanzania tufikilie kuhusu hili
 

hii kali ndo demokrasia tuyayoitaka hiyo.
 
hoja ya msingi si kususia posho, hoja ya msingi ni kubadili mfumo wa ulipaji wa posho.
 

Mkuu Matola hebu acha hiyo kitu bana. Unasema kweli mambo yamefikia hapo?. sitaki kusema sana inawezekana ana mtoto wake humu akajisikia vibaya nina reserve comment yangu ila Mungu amsaidie.
 
hoja ya msingi si kususia posho, hoja ya msingi ni kubadili mfumo wa ulipaji wa posho.

Sasa hapa ndio unaongea hoja. Nami huwa nasema tuangalie mfumo mzima wa posho na marupurupu mbalimbali serikalini. Si kuangalia posho moja tu ya vikao. Tuangalie posho, marupurupu, mishahara na makandokando mengine yanayoambatana na utumishi serikali ili kuvihuisha.

Tuangalie mfumo na kuufumua na kuanza upya na kama ni sheria zirekebishwe. Hapo tutakuwa tumeopiga hatua.
 
naomba kamanda mbowe na jopo lako endeleeni na msimamo wenu wa kukata posho kwani watanzania tupo nyuma yenu na tunasubiri hatima ya jambo hilo. Haiewezekani wachache wakafaidi our national cake najua wao watashinda bungeni kwa wingi wao na makofi wanayopiga hata wakiwa usingizini hivyo naomba muheshimiwa mbowe, zitto. lema, mnyika, lissu, mdehe, vicent nyerere na majemedali wengine leteni hyo hoja kwa wananchi tuone nani zaidi kati ya walipa kodi na wapokeaji kodi
 
Ili tulinganishe ufujaji bei ya economy Dar-Washington Economy class ni $ 1600 Ethiopian Airrlines sawa na Tsh Milioni 2.4 kwenda na kurudi!!
KWELI NCHI HUJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…