Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya

Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,198
Reaction score
162,744
Bunge limeanza leo mjini Dodoma na sasa ni kipindi cha maswali na majibu ambapo hoja inayoendelea kwa sasa ni wabunge kutaka wahusika wa biashara ya madwa ya kulevya watajwe. Waziri Lukuvi ameahidi kuwataja na ametaka mwenye ushahidi apeleke.Hata hivyo, wabunge wamemzomea na spika ameonya hiyo tabia ya kuzomea.

Baadhi ya wabunge waliotaka majina yatajwe ni mh.Mama Kilango wa CCM na mbunge wa karatu kupitia CHADEMA ambae amehoji inakuwaje hata Raisi amekiri kuwa na orodha ya wauza unga bila wahusika kutajwa na kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo, Waziri Lukuvi amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushahidi kwani amesema kama ni kutajwa tu na wengine wamo humu bungeni na ameongeza hata gazeti la Jambo leo limewataja kwahiyo kitu muhimu ni ushahidi na sio kutaja tu.

Vile vile mh.Lukuvi ameeleza nia ya serikali kubadilisha sheria ili madawa ya kulevya yakishakamatwa na ushahidi kupatikana(kuwa kwenye kumbukumbu) basi madawa hayo yaharibiwe mara moja kuliko utaratibu wa sasa ambao madawa hayo huhifadhiwa mpaka kesi husika kuisha na ametoa mfano wa madawa kuwekwa kwa miaka hata kumi kusubiri kesi ikamilike.

MY TAKE:
KAMA RAIS AMESHINDWA KUTAJA HAO VIGOGO HADHARANI, LUKUVI ATAWEZA VIPI?
 
Wale waliokuwa mafichoni ndo kijiwe kumefunguliwa waanze kuuza sura kwenye tv.
 
Kie kie kie. Leo utasikia kila mbunge ataongea at the end of the day wote lao moja
 
bunge limeanza leo na sasa ni kipindi cha maswsli na majibu ambapo hoja kubwa ni wabunge kutaka wahusika watajwe.waziri lukuvi ameahidi kuwataja na ametaka mwenye ushahidi apeleke.hata hivyo wabunge wamemzomea na spika ameonya hiyo tabia ta kuzomea.

apo ndo shida inapokuja
 
Wabunge wamezomea maana wamechoka na tabia ya Serikali kutaka kupelekewa majina ilhali Mkuu wa Nchi alisema anayo,kwanini wasianze na hayo? hatimaye bunge la vioja limeanza tena.
 
Huyo Lukuvi [ MAIMUNA] ni muongo hana lolote, hana ubavu wa kumtaja mtoto wa bosi wake anaempa ugali!!!
 
Usitegee chochote kwenye bunge lisiko la meno!!
 
Hayo madawa yenyewe yanayokamatwa huwa yanateketezwa wapi, ikiwa mazingira ya Airport ndio haya ya Polisi wezi, Tiss wezi, Porters wezi? Yanakamatwa mabegi ya mihadarati na wahusika wanashitakiwa kweli, lakini ushahidi unaopelekwa Mahakamani ni kipakti kimoja cha mihadarati. Mzigo mwingine wameusukuma fasta. Na ndio maana wakishakamata madawa hayo utawasikia polisi fasta fasta wanakutajia bei na thamani ya mzigo kwa masoko yote ya local na international. WIZI MTUPU!
 
Kufuatia swali la msingi lililoulizwa na Catherine magige viti maalum mkoa wa Arusha (CCM)kuhusu suala la madawa ya kulevya na kupewa majibu na wazira ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge mh Lukuvi, ambapo swali la nyongeza kutoka kwa mbunge wa Karatu kupitia chadema mchungaji Natse limeibua minongono baada ya kuuliza kuwa 'kazi ya serikali sio kutaja tu majina ya wauza madawa ya kulevya akitolea mfano kuwa hata mh Rais alishasema kuwa ana majina je ?nini kauli ya serikali kuhusu hilo'mh Lukuvi akijibu amesema wataendelea kutaja wengi maana hata ndani ya bunge wapo wengi tu wauza madawa majibu ambayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na kupelekea wabunge wengi kuguna na kuanza kunongona hali iliyopelekea Spika wa bunge kuwasihi wabunge kuwa watulivu ili wapewe majibu.tuendelee kufuatilia nini kinajili Dodoma.
 
kumbe wagonga meza wapo mjengoni?
kodi ya simu ni vipi hapo?
 
Sijawahi kuzingatia jambo lolote lisemwalo na Lukuvi, sijui kwanini!
 
Kufuatia swali la msingi
lililoulizwa na Catherine magige viti maalum mkoa wa Arusha (CCM)kuhusu
suala la madawa ya kulevya na kupewa majibu na wazira ofisi ya waziri
mkuu sera uratibu na bunge mh Lukuvi, ambapo swali la nyongeza kutoka
kwa mbunge wa Karatu kupitia chadema mchungaji Natse limeibua minongono
baada ya kuuliza kuwa 'kazi ya serikali sio kutaja tu majina ya wauza
madawa ya kulevya akitolea mfano kuwa hata mh Rais alishasema kuwa ana
majina je ?nini kauli ya serikali kuhusu hilo'mh Lukuvi akijibu amesema
wataendelea kutaja wengi maana hata ndani ya bunge wapo wengi tu wauza
madawa majibu ambayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na kupelekea wabunge
wengi kuguna na kuanza kunongona hali iliyopelekea Spika wa bunge
kuwasihi wabunge kuwa watulivu ili wapewe majibu.tuendelee kufuatilia
nini kinajili Dodoma.

Yahya unaishi wapi aka Idd azan
 
Msitegemee lolote kutoka bungeni!! Wengi mle ni kama wafanyakazi wa umma waliokwenye semina ikifika jioni wanasaini posho zao.

Bunge linasimamiwa na serikali badala ya Bunge kusimamia serikali!!
 
Bunge ni lile lile,wabunge ni walewale na hoja ni zilezile na LUKUVI ni yuleyule
 
Back
Top Bottom