Bungeni Dodoma: Mjumbe asema nchi zinazopiga kura za siri kupitisha katiba ni za mashoga!

Yule mama kweli hajatulia. Sasa anaposema kupiga kura za siri ni ushoga, na sisi huwa tunapiga kura za siri kumchagua rais, wabunge, madiwani na viongozi wa ngazi mbali mbali za kisiasa, kidini na kijamii. Sasa kama kupiga kura za siri ni ushoga, basi hata Zanzibar na Tanganyika ni za mashoga na kwa maana hiyo hata wao huko bungeni wanapopiga kura za siri kuchaguana, ushoga! Huyu mama katoa kali ya mwaka!

Ushoga upo Tz kisiri ndo maana mother kajua kila siri ni ushoga tafakari sana utaelewa!
 
Kama ni hivyo, naona huyo mjumbe anatutukana wengi sasa.

Kura ya wazi haiwezi kuwa ya haki kwani watu watapiga kura kwa nidhamu ya woga.

Hii katiba ni ya watanzania sio vyama

Halelujah!!! Wonderful!!!!! The guy is back to his senses.

Tiba
 
Kama ni hivyo, naona huyo mjumbe anatutukana wengi sasa.

Kura ya wazi haiwezi kuwa ya haki kwani watu watapiga kura kwa nidhamu ya woga.

Hii katiba ni ya watanzania sio vyama
Kosa kubwa lililofanyika ni kuwateua wanasiasa kuwa wabunge wa hili bunge la katiba. Wao wanaendeleza utamaduni uleule wa kwenye bunge la JMT wa kuamua mambo kichama zaidi.
 
Hata kwako wewe! Kuna nini? Kumbe una akili! Nilishakuweka kapuni, good to know that you can also see things the right way as others!

inawezekana lukosi uliacha page yako bila kulogout maana hiyo comment cdhani kama in we we umeiandika na kama ni we we basis nakupongeza kwa kujitoa ujinga na kujivika ufahamu kwa muda.
 
Acha uongo wa kihuni sisi tupo bungeni ukitaka kuwa muongo jipange vizuri.

Inawezekana upo BUNGENI kwa ajili ya kujiuza au kama sio kwa kujiuza basi umekwenda kuiba vya wenzio kama vile simu na Laptop na ndio maana haukuweza kusikia wala kuyaona hayo yaliyotokea.
 
Kama ni hivyo, naona huyo mjumbe anatutukana wengi sasa.

Kura ya wazi haiwezi kuwa ya haki kwani watu watapiga kura kwa nidhamu ya woga.

Hii katiba ni ya watanzania sio vyama
Kumbe kuna wakati kichwa chako kinatulia na kunena ya msingi? Umekula nini leo wewe? Basi ulichokula leo ndicho unachopaswa kula kila siku.
 
Halelujah!!! Wonderful!!!!! The guy is back to his senses.

Tiba

Hii ni leo tu chriss Lukosi amepata nafuu ya ugonjwa wake na kupata ufahamu lakini kesho angalia atakachopost utashangaa.
 
Kama ni hivyo, naona huyo mjumbe anatutukana wengi sasa.

Kura ya wazi haiwezi kuwa ya haki kwani watu watapiga kura kwa nidhamu ya woga.

Hii katiba ni ya watanzania sio vyama

duu! Kumbe una uwezo wa kufikiri na kutafakari mambo na kutoa hoja kwa maslahi ya taifa!!??
 
Wajumbe kama Hao sawa yake ni kuwarudisha home tu

Huyu mama wa zenj kasema ukweli mtupu.ukweli unaumiza wasioupenda.nani hajui kwamba nchi taja zinamsakama Museveni kwa kusaini ile sheria ya kulinda ubinadamu.Kura za siri lengo lake ni kupitisha mambo ya aina hii ni kupitisha mambo ya aina hii kisiri siri.Hatari sana.Nisiyemuelewa ni huyu Safari.anatetea nini hasa.wenyewe hawajifichi.Mama Mbunge usikatishwe tamaa.kaza buti
 
Wameshikwa pabaja na hawaaminiani, wanajua wakikubali kura y siri wataona manyoya. so hali ni mbaya kwa wahafidhina
 
Ni ajabu sana kwa wajumbe wa chama tawala ambao ni wengi mno, kuogopa kupiga kura ya siri. Ama chama chao kinafahamu kuwa kinachotaka ni bomu la kulazimisha? Kura ya wazi ni udikteta. Wajumbe watakubali tu hoja hata kama ni utumbo kwa kuhofia kupatilizwa na viongozi wao. Poor Tanzania.
 
Huyu mama wa zenj kasema ukweli mtupu.ukweli unaumiza wasioupenda.nani hajui kwamba nchi taja zinamsakama Museveni kwa kusaini ile sheria ya kulinda ubinadamu.Kura za siri lengo lake ni kupitisha mambo ya aina hii ni kupitisha mambo ya aina hii kisiri siri.Hatari sana.Nisiyemuelewa ni huyu Safari.anatetea nini hasa.wenyewe hawajifichi.Mama Mbunge usikatishwe tamaa.kaza buti
Hivi unajua ulichoandika kweli???Au umesukumwa tu na ushabiki??!!
 
Huyu mama wa zenj kasema ukweli mtupu.ukweli unaumiza wasioupenda.nani hajui kwamba nchi taja zinamsakama Museveni kwa kusaini ile sheria ya kulinda ubinadamu.Kura za siri lengo lake ni kupitisha mambo ya aina hii ni kupitisha mambo ya aina hii kisiri siri.Hatari sana.Nisiyemuelewa ni huyu Safari.anatetea nini hasa.wenyewe hawajifichi.Mama Mbunge usikatishwe tamaa.kaza buti

Wajumbe hao hao ikiwa ni pamoja na huyo mama wamemchagua mwenyekiti wa muda Mh. Pandu Kificho kwa kura za siri. Kwa maelezo yako una maana wajumbe wote ikiwa ni pamoja na huyo mama ni mashoga?! Watanzania walipiga kura katika uchaguzi mkuu uliopita 2010 kwa siri kuwachagua madiwani, wabunge na rais. Je waliopiga kura nao ni mashoga?! Na kwa uelewa wako na huyo mama kuhusu kura za siri ni kuwa, hata waliochaguliwa ni mashoga???!!!
 
Amenishangaza mama mmoja mjumbe wa bunge la katiba aliposema kuwa nchi ambazo zimekuwa zikipiga kura ya siri kupitisha katiba zao ni nchi za mashoga. Ameyasema hayo leo alipokuwa akipinga upigaji wa kura za siri wakati wa kupitisha rasimu ya katiba kufuatia mifano iliyotolewa na mjumbe mwingine aliyekuwa akitaka kura zipigwe kwa siri na kutoa mifano ya nchi mbali mbali zilizopiga kura za siri wakati wa kupitisha katiba zao. Profesa Safari alimtaka yule mama atoe ushahidi na kama hana aombe radhi na kufuta kauli yake. Mwenyekiti wa muda Bw Pandu Kificho hakumpa nafasi yule mama kutoa ushahidi au kuomba radhi badala yake alisema wajumbe wawe makini kujadili mambo ili waepushe mjadala kwenda kwenye mambo mengine.

Ni mropokaji asiyepima athari za kauli zake
 
Kama ni hivyo, naona huyo mjumbe anatutukana wengi sasa.

Kura ya wazi haiwezi kuwa ya haki kwani watu watapiga kura kwa nidhamu ya woga.

Hii katiba ni ya watanzania sio vyama

Hizo dawa ni nzuri. Endelea nazo utapona kabisa na huu mwaka uvuki utakuwa sawa
 
Back
Top Bottom