Anachokisema Trump ni kwamba Katiba za Nchi ndio zinatoa mianya ya kuiba Kura Siyo Rais. Hapa Tanzania Magufuli anaonewa bure kwa ile 2020!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,873
Kwa mfano Katiba ndio inaruhusu Watendaji wakuu wa Tume ya Uchaguzi wateuliwe na Rais

Katiba ndio inaruhusu Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi

Katiba ndio inaruhusu " Wajanja" wapite Bila kupingwa

Sasa hapo utamlaumuje hayati Magufuli kwa matokeo ya 2020?

Trump ambaye ni Rais wa Marekani anasema Katiba ya Nchi Hiyo ndio inaruhusu Wizi wa kura kwenye Uchaguzi hivyo ifutiliwe mbali
 
MAGUFULI ALITUMIA KATIBA MBOVU KUIBA KURA NDIO MAANA CCM INAOGOPA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
 
Nadhani unaelewa vibaya dhana nzima ya kumlaumu Rais. Na sidhani unamaanisha Katiba si kitu muhimu.

Na Trump unayemnukuu anasema hivo tu kwa kuwa ana machungu ya 2020. Je si ni katiba hii ilifa ya akashinda uRais huku akiwa ameshindwa popular vote?? Ndio kusema hujui kuwa hajapinga ushindi wa house reps, senators, attorney generals, governors, DAs, state reps na senators wa Republican kwa kupitia katiba na taratibu hizo hizo zilizofanya ashindwe?? Alifungua kesi 60 za kupinga matokeo. Hata moja hakushinda!!

Turudi nyumbani. Anapolaumiwa Rais wa Tanzania ni katika mambo haya;
a) JK alianzisha mchakato wa katiba na hakuufikisha mwisho baada ya chama chake kukataa rasimu.
b) JPM yeye akasema katiba sio kipaumbele na wala haikuwa kwenye manifesto yake.
c) SSH akaunda tume ya kuleta maridhiano ya kisiasa.
d) Katiba inampa madaraka Rais kuchagua Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Wakurugenzi. Hawa watu ndio husimamia shughuli za uchaguzi.

Rais wetu hakulaumiwi kwa kuiba kura. Analaumiwa kwa kukumbatia mfumo unaompa mamlaka ya kusimamia chaguzi wakati na yeye ni mshindani!! Kuna conflict of interest tena sehemu ambayo hata mahakama hairuhusiwi kuhoji ushindi wake!!

Ni kweli huoni haya? Huoni kwanini Trump sio Rais na hawezi kuwa Rais nje ya matakwa ya katiba??
 
Tangu vyama vianze Tanzania siku zote upinzani wao wanaibiwa kura uchaguzi mkuu. Iwe kweli, iwe uongo, iwe uongo-kweli matatizo ya Tanzania ni sugu sana zaidi ya ubovu wa katiba.
 
Nadhani unaelewa vibaya dhana nzima ya kumlaumu Rais. Na sidhani unamaanisha Katiba si kitu muhimu.

Na Trump unayemnukuu anasema hivo tu kwa kuwa ana machungu ya 2020. Je si ni katiba hii ilifa ya akashinda uRais huku akiwa ameshindwa popular vote?? Ndio kusema hujui kuwa hajapinga ushindi wa house reps, senators, attorney generals, governors, DAs, state reps na senators wa Republican kwa kupitia katiba na taratibu hizo hizo zilizofanya ashindwe?? Alifungua kesi 60 za kupinga matokeo. Hata moja hakushinda!!

Turudi nyumbani. Anapolaumiwa Rais wa Tanzania ni katika mambo haya;
a) JK alianzisha mchakato wa katiba na hakuufikisha mwisho baada ya chama chake kukataa rasimu.
b) JPM yeye akasema katiba sio kipaumbele na wala haikuwa kwenye manifesto yake.
c) SSH akaunda tume ya kuleta maridhiano ya kisiasa.
d) Katiba inampa madaraka Rais kuchagua Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Wakurugenzi. Hawa watu ndio husimamia shughuli za uchaguzi.

Rais wetu hakulaumiwi kwa kuiba kura. Analaumiwa kwa kukumbatia mfumo unaompa mamlaka ya kusimamia chaguzi wakati na yeye ni mshindani!! Kuna conflict of interest tena sehemu ambayo hata mahakama hairuhusiwi kuhoji ushindi wake!!

Ni kweli huoni haya? Huoni kwanini Trump sio Rais na hawezi kuwa Rais nje ya matakwa ya katiba??
Tatizo Wapinzani wanashinda pia chini ya mfumo huu huu!
 
Back
Top Bottom