Bb YangeYange
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 337
- 184
Watanzania watu wa ajabu sana! Humu JF zinapigwa kelele nyingi kuhusu uamuzi wa Serikali kusitisha kuonyesha Bunge live. Watu wanadai wananyinwa haki yao ya kupata habari toka Bungeni. Cha kushangaza ni kwamba wanaolalamikia kupata yanayojiri Bungeni ndio hao wanatuletea habarI 'motomoto' za Bungeni.
Kwa maana nyingine Serikali iko sahihi si lazima Bunge lionyeshwe live ili watu wapate habari muhimu! Wapo wanaoshupaa kabisa na kudai kwamba Watanzania wengi wanataka kuona Bunge live kwahiyo 'wengi wape'.
Ni wengi wapi hao? Tanzania imejaa maskini ambao hats mlo mmoja kwa siku kuupata niv shida. Hivi ni kweli wengi hawa, maskini wa Tanzania wanataka Serikali yao ionyeshe tv live badala kuwakwamua kwenye umaskini wao?
Ifike mahali 'sisi' Watanzania wachache wenye uwezo tuwafikirie na Watanzania wenzetu walio wengi ambao wanaihitaji sana hiyo fedha ambayo Serikali inadhamiria kuokoa kutoka matangazo live. Na wao wana haki pia!
Pengine Serikali ya HAPA KAZI TU ingetutangazia kwamba hakuna kuonyesha Bunge live ili waangaliaji wote wachape KAZI maana ni muda wa kazi kwa Watanzania wote Wakulima na Wafanyakazi!