Bunge limeisha wabunge rudini majimboni mwenu mfanye maendeleo

Omuchimati

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
427
202
Leo waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano amehitimisha bunge la Jamhuri ya muungano kwa hotuba yake iliogusa Nyanja zote za kimaisha, kisiasa, kijamiii na kiuchumi, hiki huwa ni kipindi kitamu sana kwa wabunge wote wa Jamhuri ya muungano ambapo kila mbunge uunga mkono hoja hiii kwa sauti ya ndiyoooo.

Ndugu zangu wabunge wa majimbo mbalimbali Tanzania nawakumbusha kurudi majimboni kwenu mkapigane ili kuleta maendeleo majimboni mwenu, na sio tuanze kukutana kwenye mahotel makubwa makubwa jijini Dar mkiwa na warembo na watu wa maarufu wa jijini, hilo nakwambieni sababu watu wameshagutuka wanataka maendeleo na si porojo za kisiasa kama za akina HALIMA MDEE, nenda kaulize jimboni kwake amefanya jambo gani la maendeleo, ni vilio vitupu, hata kuna watu wengine hawajui kama ni mbunge wao.

Juhudi zenu za kuleta maendeleo na kutatua kero za wananchi majimboni mwenu ndizo ztakazo warudisha bungeni.

NAKUTAKIENI UJENZI MWEMA WA TAIFA LENU.
 
kazi ya mbunge ni bungeni,majimboni hawana cha kufanya maana kama ni fedha zinapangwa na Halmashauri
 
Kazi za mbunge kisheria ni zipi mkuu. Maana neno maendeleo sidhani kama huwa lipo.
Kazi ya maendeleo ni serikali. Mbunge aende kukusanya kero ili apate cha kuishauri serikali akiwa bungeni
 
kazi zenyewe hadi waombe kibali kwa disii, si heri tu wapige zao mishemishe wasubiri msimu ujao wa bunge
 
Back
Top Bottom