Bunge limegubikwa na wasemaji wasiojua tofauti ya speak and talk

Inasikitisha sana Bashe ni mtafutaji kiki za kisiasa kuliko mbunge mwingine yeyote...yuko na mission zake ambazo anataka kuziaccomplish kwa faida yake na familia yake..MBAYA....nawahurumia wananchi wake.
Sasa hapo ungekuja na hoja inayopingana na hoja za kiuchumi za Bashe ndo ungekuwa GT kweli kweli. Hayo uliolyoandika ni mipasho isiyokuwa na ukweli wala maana!
 
Serikali inakwepa kilimo? Mpaka imweka wizara maalumu. Nilidhani Mh. bashe angekuja na hoja binafsi kuzibana benki ziwakopeshe wakulima. Hii ni hoja ya kibange. Serikali inamzigo mzito.
Unajua mkulima anatumia gharama kubwa kuzalisha halafu anakosa soko unajua inatokana na sera za serikali kukosa mipango ya kuwasaidia wakulima wake au huoni bado tunazalisha msimu baada ya msimu he na kiwanda kitakuwa kinafungwa kinasubr msimu ndo kifanye kwanini serikali isiwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji kwanza hata viwanda vikiwepo vipate raw materials through the year
 
Sasa data ndio hoja! City water inahitaji Data gani? Tanzania tuna e

ni mfano tu. Juzi Mzee makamba ameuza mkonge pia. kuna pareto ,pamaba na kadhalika

Mzee Makamba analima kwa kujifurahisha na sio kwamba analima ili aendeshe maisha yake na kusomesha watoto. Huyo mzee Makamba unayemzungumzia wewe ana miradi mingi tu inayoweza kuwa backup ya hicho kilimo cha mkonge, hivyo hata hicho kilimo kianguke bado anaweza kujaza mafuta kwenye VX yake. Nimeangalia mchango wako nikajua hujui uhalisia bali unaongea ili uonekane umetetea serekali.
 
Unajua mkulima anatumia gharama kubwa kuzalisha halafu anakosa soko unajua inatokana na sera za serikali kukosa mipango ya kuwasaidia wakulima wake au huoni bado tunazalisha msimu baada ya msimu he na kiwanda kitakuwa kinafungwa kinasubr msimu ndo kifanye kwanini serikali isiwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji kwanza hata viwanda vikiwepo vipate raw materials through the year
Wewe unadhani kilimo na kiwanda kipi kianze? Maana ukilima hakuna kiwanda bidhaa zinaoza. Nadhani tujenge viwanada alafu tupanue mashamaba. Hoja ya kulima alafu ujenge kiwanda ni upunguani.
 
Jana bungeni Mh. bashe alisema export zimepungua serikali inaficha data, naomba kumuuliza huyu kijana. Yeye ana mashamba mangapi ya korosho. Maana export haziwezi kuongezeka kama Watanzania hatulimi. Agepaswa kulalamika anauza sana nje na serikali inamfichia data.

KuhusuMabenki; Mabenki kibao hayapo kibishara. Matangazo yao kila siku yanataka fixed deposite, Mortage, na Mikopo ya wakandarasi hivi mamantilie anaweza kuweka fixed deposite? Wawakuze wafanyabishara wadogo wawe wakubwa. wanataka simple business kwanini faida zishishuke?
Mabenki mengi hapa Tanzania wanafanya biashara na serikali na matajiri wa kati na wakubwa.

Mbunge mwingine anasema Private partnership. Simuelewi! Tumeuza hapa viwanda vimebakia magofu. Private partnership hapa Tanzania ni dhambi. Tuliwaleta City Water tukala wa chuya. Tuliwaleta Celtel tukaumia, na Star Times yaleyale. Hata machungu hayajatusha. Anataka PPT ipi? Hajifunzi kutokana na makosa. Yeye kama anahela ajenge kiwanda. NDC wanataka wawekezaji au anatafuta pesa za kununua nyumba ya lugumi. Kama anataka pesa za kuandika proposal asahau. Pesa ipo shambani .

Jana imekuwa siku yangu ngumu sana. Nimehuzunika na nimenyong'onyea sana. Nimegundua kwanini bunge halionyeshwi live. Bunge halionyeshwi live kwasababu wabunge wanawalisha wananchi sumu.
Lazima wabunge wajue tofauti ya speak and talk. nimekuwa mgumu sana kusema kitu. Nimekuwa najifua sana.

Nape what is wrong? Elimu? Au nini? Tanzania is Moving in Right Direction Hata wazungu wanashangaa!!wewe huoni chochote?
Duh yaani ningekuwa na chuo kijana ningekuita nije nikupatie PhD ya heshima. Yaani umepiga penyewe kabisa. Unajua wao lengo lao ni kuivuruga serikali ya Dkt Magufuli, yaani wanatafuta muanya. Na ukitaka kujua wamekula rushwa wasikilize kauli zao, zinafanana. Serukamba anasema eti PPP ina uhusiano na ujamaa, yaani ukikataa PPP maana yake unakumbatia ujamaa. Kwanza nasema huyu mbunge hana exposure na hajui kitu, na hajui maana ya PPP. Huwezi ukawa na PPP ambayo ni nzuri kama kuna 10% (ambayo akina serukamba walizoea). Msikilize Bashe na yeye, yeye anasema Mpango hafai, Ndasa naye hivyo hivyo eti ana kiburi, sasa unajiuliza mbona hawa matamshi yao yanafanana??? Ila Bashe kaguzia kitu ambacho rushwa inaonekana ilitembea, pale anaposema watu wa sekta fulani fulani. Pia hizo monetary policy na fiscal policy anazoongelea Bashe hata hazijui, ni mbumbu, ila kuyatamka maneno na kuweka vigereza vyenye makengeza ni mahili. Kwa ufupi Haters wazoee tu, hii nchi iko safiii kabisa
 
Mzee Makamba analima kwa kujifurahisha na sio kwamba analima ili aendeshe maisha yake na kusomesha watoto. Huyo mzee Makamba unayemzungumzia wewe ana miradi mingi tu inayoweza kuwa backup ya hicho kilimo cha mkonge, hivyo hata hicho kilimo kianguke bado anaweza kujaza mafuta kwenye VX yake. Nimeangalia mchango wako nikajua hujui uhalisia bali unaongea ili uonekane umetetea serekali.

Achana na makamba nenda kaone mashamaba ya mkonge. Tajiri MO ana mashamba kila kona ya mkonge. Tembea uone acha kukaa hapa Dar unakula chips kuku.
 
Serikali inakwepa kilimo? Mpaka imweka wizara maalumu. Nilidhani Mh. bashe angekuja na hoja binafsi kuzibana benki ziwakopeshe wakulima. Hii ni hoja ya kibange. Serikali inamzigo mzito.
Loo! kunamijitu mingine huwa haioni aibu kuanika utupu wa mabichwa yao hadharani! bora ungekaa kimya kuliko kujipendekeza kwa hoja uchwara kama hizi. Hata unayemsifu na kumtetea anakudharau.
 
Serikali inakwepa kilimo? Mpaka imweka wizara maalumu. Nilidhani Mh. bashe angekuja na hoja binafsi kuzibana benki ziwakopeshe wakulima. Hii ni hoja ya kibange. Serikali inamzigo mzito

Kwa kuwa wewe ni verified user weka slip ya mkopo toka bank yoyote iliyokukopesha ukalime. Acha nadharia dogo. Sasa hivi ukienda bank kuomba mkopo kisha ukaonyesha unataka kwenda kulima hakuna atakayekusikiliza maana wanajua hela yao itapotea. Labda uonyeshe una miradi mingine mbalimbali na sio kutegemea kilimo kama sehemu ya kulipia mkopo wao. Huko kwenye kilimo kuna madhila mengi kama mabadiliko ya hali ya hewa na serekali imegeuza wakulima ni watu wa kuwa masikini daima kwa kuwapangia bei itakayowaumiza.
 
Wewe unadhani kilimo na kiwanda kipi kianze? Maana ukilima hakuna kiwanda bidhaa zinaoza. Nadhani tujenge viwanada alafu tupanue mashamaba. Hoja ya kulima alafu ujenge kiwanda ni upunguani.
Kilimo kianze rasilimali zikishakuwa za uhakika viwanda vitakuja vyenyewe baada ya kuwa na uhakika wa raw material au serikali itaruhusu watu kuuza hata nje nchi wakulima wapate hela nzuri
 
Achana na makamba nenda kaone mashamaba ya mkonge. Tajiri MO ana mashamba kila kona ya mkonge. Tembea uone acha kukaa hapa Dar unakula chips kuku.

Nakuambia unadhani unaongea jambo la maana kumbe unachekesha walionuna. nimekuambia Makamba amejitosheleza ndio maana analima mkonge, wewe unanitajia mfano wa MO wakati unajua kabisa MO ni tajiri kuliko huyo Makamba. Tuongelee wakulima wengi ni nani anaweza kukopeshwa kwenda kulima kilimo chenye tija? Unayajua masharti ya mkopo au unaongea kujifurahisha hapa jukwaani?
 
Kilimo kianze rasilimali zikishakuwa za uhakika viwanda vitakuja vyenyewe baada ya kuwa na uhakika wa raw material au serikali itaruhusu watu kuuza hata nje nchi wakulima wapate hela nzuri
Heh! kwahiyo kilimo cha mazao gani! ambacho unalima tu miaka kadhaa uasubiri kiwanda kijengwe ndio upate soko. Lababda sikuelewi.
 
Binafsi sijawahi kuona faida ya bunge hata siku moja......kwa mtazamo wangu, ni moja wapo ya wafanyakazi hewa!
Mtu asiyekuwa na tija ni bora asiwepo kabisa!!
Laiti kama ungejua sababu ya bunge kukosa Hadhi yake ungeipumzisha simu yako kuibonyeza eti unatoa comment.
 
Sasa hapo ungekuja na hoja inayopingana na hoja za kiuchumi za Bashe ndo ungekuwa GT kweli kweli. Hayo uliolyoandika ni mipasho isiyokuwa na ukweli wala maana!
hata hiki ulichoandika hapa ni mipasho poor JF GT wote kwisha wamebaki mashabiki tu wa siasa ambao wameleta ushabiki wa simba na yanga kwenye mambo ya msingi ya nchi
 
Nakuambia unadhani unaongea jambo la maana kumbe unachekesha walionuna. nimekuambia Makamba amejitosheleza ndio maana analima mkonge, wewe unanitajia mfano wa MO wakati unajua kabisa MO ni tajiri kuliko huyo Makamba. Tuongelee wakulima wengi ni nani anaweza kukopeshwa kwenda kulima kilimo chenye tija? Unayajua masharti ya mkopo au unaongea kujifurahisha hapa jukwaani?

mimi najua mikopo ya kilimo ipo mingi! Ila kwkuwa wabunge wameshindwa kuvimbia mabenki. Mabenki yanawakopesha matajiri wakalime. Masikini hawana kigezo cha kukopesheka. watu wanakopa mamilioni wanatelekeza mashamba wanafanyia kitu kingine mimi nawajua watu wanne.
 
Jana bungeni Mh. bashe alisema export zimepungua... export haziwezi kuongezeka kama Watanzania hatulimi.

Kuhusu Mabenki; Mabenki kibao hayapo kibishara. ... Mabenki mengi hapa Tanzania wanafanya biashara na serikali na matajiri wa kati na wakubwa.

Private partnership. Simuelewi! Tumeuza hapa viwanda vimebakia magofu. Private partnership hapa Tanzania ni dhambi.
...
Nimegundua kwanini bunge halionyeshwi live. Bunge halionyeshwi live kwa sababu wabunge wanawalisha wananchi sumu.
...
Tanzania is Moving in Right Direction Hata wazungu wanashangaa!!wewe huoni chochote?
Kati ya wanaJF wenye mtazamo chanya, ni pamoja na wewe, wa jinsi Serikali inavyojenga misingi ya uchumi imara na endelevu kuelekea Tanzania mpya.

Mifano uliyotoa ni kielelezo kizuri, cha kile anachokipiga vita Rais Magufuli, cha kufanya kazi kwa mazoea business as usual, na ambacho Wabunge wetu wanataka kuturudisha huko.

Kwa sasa kazitu ikifanywa kwa:
i) Malengo/Vipaumbele km kukusanya kodi - Bashe anadai ati Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo 2018/19 umejaa maswala ya kodi tu!! Aibu kwake kijana.
ii) Malengo magumu yanayoweza kugharimu maelewano katika jamii (lawama na shutuma) - Tanzania ya viwanda, elimu bure nk. Lakini Mbowe anasema ni ndoto, Serikali inachofanya ni kuwasakama wapinzani. Wao wamejenga viwanda vingapi au kusomesha watoto wangapi bure, hata kwenye Majimbo na Halmashauri wanazoziongoza!
iii) Utekelezaji wa malengo magumu kwa umakini. Kutoa elimu bure ni lazima kuwepo uwezo wakufanya hivyo kifedha, japo fedha siyo msingi wa maendeleo. Kusimamia kwa karibu utendaji wa kila mfanyakazi ni moja ya nguzo kuu za kufikia lengo. Hatua za kuondoa wafanyakazi wenye vyeti hewa imehakikisha kuwepo kwa maamuzi sahihi na kuua mizizi wa urasimu na umangimeza.
iv) Na kadhalika yanayogusa sifa 6 za kiongozi mwanamageuzi.

KESHO TUSIONE VINAELEA VINAUNDWA
 
Kwa kuwa wewe ni verified user weka slip ya mkopo toka bank yoyote iliyokukopesha ukalime. Acha nadharia dogo. Sasa hivi ukienda bank kuomba mkopo kisha ukaonyesha unataka kwenda kulima hakuna atakayekusikiliza maana wanajua hela yao itapotea. Labda uonyeshe una miradi mingine mbalimbali na sio kutegemea kilimo kama sehemu ya kulipia mkopo wao. Huko kwenye kilimo kuna madhila mengi kama mabadiliko ya hali ya hewa na serekali imegeuza wakulima ni watu wa kuwa masikini daima kwa kuwapangia bei itakayowaumiza.

Mikopo ya kilimo ipo covered tatizo Mabanki yapo tayari kuijenga nchii hii. Tena mabenki mengi yanamilikiwa na kuendeshwa na wazungu.
 
Wabunge Nape na Bashe msitulishe upupu tunajua mambo yenu mnaegemea wapi ! mzee Magu kabana majizi msituletee theory uchwara hapa wanaosema Tanzania imepiga hatua sana data si zinatolewa na wachumi wa kimataifa ? Nani atawekeza kwenye ujenzi wa reli kama sio serikali nani atawekeza kwenye umeme ? mbona haya ma IPTL yalikuwa ni sekta binafsi mnataka kutueleza nini ? Ubinafsishaji ulianza kwa Mzee Mkapa mbona makampuni mengi yamekuwa magofu . Acheni porojo
 
Back
Top Bottom