Askofu Malasusa: Sijalelewa kuwa Kinyume na Serikali, Sijalelewa kutoitii Serikali!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,023
Mkuu wa Kanisa la KKKT baba askofu Dr. Alex Malasusa amesema alipochaguliwa tu Muumini mmoja alimtumia salamu za pongezi na kusema "Mitaani Watu wanasema wewe uko Karibu sana na Serikali."

Askofu Malasusa amesema hawezi kukataa ukaribu wa na Serikali kwa Sababu hukulelewa kwenda Kinyume au kutoitii Serikali.

Askofu Malasusa amesema Hayo mbele ya viongozi wakuu wa Serikali na mihimili ya DOLA yaani Rais Samia, Spika Dr. Tulia, JM Prof Juma, Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi, Waziri wa mambo ya Ndani na RC Chalamila.

Aidha Askofu Dr Malasusa amewataka Wanasiasa kukaa mezani na kuzungumza badala ya kutumia mbinu nyingine ilu kulinda Amani iliyopo

Source Upendo TV
======For English Audience Only========

The head of the Evangelical Lutheran Church in Tanzania (KKKT), Bishop Dr. Alex Malasusa, recently shared that upon his election on being close to government officials. Bishop Malasusa affirmed that he cannot deny his proximity to the government, emphasizing that he has been raised to respect and obey the authorities.

Speaking in the presence of key government officials and pillars of the state, including President Samia, Speaker Dr. Tulia, Chief Justice Prof Juma, CCM Secretary-General Dr. Nchimbi, Interior Minister, and Regional Commissioner Chalamila, Bishop Malasusa made these remarks. Additionally, he urged politicians to engage in dialogue at the negotiation table rather than resorting to other methods to safeguard the existing peace.​

Kweli kabisa, Biblia inasema tutii mamlaka. Dk. Shoo, yeye alikuwa amelifanya kanisa kuwa annexture ya chadema kama ilivyo Bawacha na Ba-VICHAA. Dk. Shoo alikuwa anatumia muda mwingi sebuleni kwa Mbowe kuliko kanisani.

Amestaafu, Mbowe kampa VX-V8
 
Mkuu wa Kanisa la KKKT baba askofu Dr Alex Malasusa amesema alipochaguliwa tu Muumini mmoja alimtumia salamu za pongezi na kusema " mitaani Watu wanasema wewe uko Karibu sana na Serikali"

Askofu Malasusa amesema hawezi kukataa ukaribu wa na Serikali kwa Sababu hukulelewa kwenda Kinyume au kutoitii Serikali

Askofu Malasusa amesema Hayo mbele ya viongozi wakuu wa Serikali na mihimili ya DOLA yaani Rais Samia, Spika Dr Tulia, JM Prof Juma, Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi, Waziri wa mambo ya Ndani na RC Chalamila

Source Upendo TV
KKKT rasmi ime kuwa tawi ndani ya Ccm
 
Kweli kabisa, Biblia inasema tutii mamlaka. Dk. Shoo, yeye alikuwa amelifanya kanisa kuwa annexture ya chadema kama ilivyo Bawacha na Ba-VICHAA. Dk. Shoo alikuwa natumia muda mwingi sebuleni kwa Mbowe kuliko kanisani.

Amestaafu, Mbowe kampa VX-V8
Malasusa ameifanya KKKT kuwa annexture ya CCM kama Bakwata na yenyewe ilivyo annexture ya CCM. Maaskofu waliomchagua Malasusa kweli wamelinajisi Kanisa hilo kwani huyu ni afisa kipenyo kitambo tu.
 
Viongozi wa dini wanalojukumu la kuonya na kukemea watawala wanapokengeuka hata kama watakatwa kichwa kama Yohana.

Kama kiongozi wa dini atakua ni mtii kwa viongozi wa serikali hata wanapofanya mambo yanayomchukiza Mungu utakua ni unafiki.

Kuwaunga mkono viongozi wa serikali kwenye mambo mazuri ni vizuri lakini kuwaunga mkono kwenye mambo mabaya ni vibaya.

Hufai kuwa kiongozi kama huwezi kuisimamia kweli hata kama kweli hiyo inawakwaza viongozi.
Tusiogope kukatwa kichwa kama Yohana kwa kuwaeleza wenye mamlaka ukweli wakitenda vyema na ukweli wakitenda vibaya.
 
Kweli kabisa, Biblia inasema tutii mamlaka. Dk. Shoo, yeye alikuwa amelifanya kanisa kuwa annexture ya chadema kama ilivyo Bawacha na Ba-VICHAA. Dk. Shoo alikuwa anatumia muda mwingi sebuleni kwa Mbowe kuliko kanisani.

Amestaafu, Mbowe kampa VX-V8
Biblia baadhi ya sehemu ili badilishwa na wahuni enzi za rumi ,ili serikali ya rumi kuitawala dunia vizuri.

Bahati mbaya waamini hawasomi maandiko na wakisoma hawayafanyii utafiti na uchambuzi yakinifu.

Mazwazwa.

Ila KKKT itakuja pasuka mbeleni

Mimi nipo hapa
 
Sasa kumbe kauli za mwaipopo ni sahihi kuwa chadema na kanisa damu damu au Siyo.
 
Viongozi wa dini wanalojukumu la kuonya na kukemea watawala wanapokengeuka hata kama watakatwa kichwa kama Yohana.
kama Yohana kwa kuwaeleza wenye mamlaka ukweli wakitenda vyema na ukweli wakitenda vibaya.
Ni sahihi kukemea kiongozi wa serikali au hata kiongozi yeyote kanisani lakini Sio hadharani anatakiwa kuambiwa Kwa Siri ndani ya vikao kuwa hapa na hapa sio

Viongozi wakubwa wa dini wanaojielewa kama Kardinali Pengo,Mufti wa Bakwata na Shehe Mkuu wa Bakwata Zuberi na Askofu Mkuu wa KKKT Malasusa huonya sana na huwezi Ona wako Wakienda vyombo vya habari ila utashangaa maraisi wenyewe wanatimua mbio wanaenda kuwaona ofisini Kwao .Hutawaoba Wala kujikomba kwenda Ikulu Viongozi wenyewe ndio huenda

Magufuli mwenyewe na ubabe wake alikuwa akitimua mbio kwenda pale Azania Kwa Malasusa na Kwa Pengo na Shehe Mkuu wa Bakwata

Hiyo timu ya watu watatu wanajua Nini maana ya kuwa kiongozi wa dini si kujikomba na ukiona Kuna jambo hufoki vyombo vya habari unamwambia njoo ofisini kwangu na Raisi au Waziri atatimua mbio hatari kuitika wito

Viongozi wengi wa dini hawana hadhi ya kumwita Raisi au Waziri au Mkuu yeyote wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa njoo ofisini kwangu walishapoteza hiyo hadhi si rahisi wakamwita hata mjumbe wa nyumba kumi tu ajieleze Kwao au kumuonya haendi

Hao watatu wamejenga hadhi za juu sana ambayo akina Askofu Shoo nk hawajaijenga

Kiongozi mkubwa wa dini huwezi kuwa unabweka tu kama mwehu barabarani au vyombo vya habari kubwekea viongozi wa serikali
 
Mkuu wa Kanisa la KKKT baba askofu Dr Alex Malasusa amesema alipochaguliwa tu Muumini mmoja alimtumia salamu za pongezi na kusema " mitaani Watu wanasema wewe uko Karibu sana na Serikali"

Askofu Malasusa amesema hawezi kukataa ukaribu wa na Serikali kwa Sababu hukulelewa kwenda Kinyume au kutoitii Serikali

Askofu Malasusa amesema Hayo mbele ya viongozi wakuu wa Serikali na mihimili ya DOLA yaani Rais Samia, Spika Dr Tulia, JM Prof Juma, Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi, Waziri wa mambo ya Ndani na RC Chalamila

Source Upendo TV
Huyu amepata nafasi hiyo kwa kutumia nguvu za taasisi za dola na ni kibaraka anayefahamika
 
Ni sahihi kukemea kiongozi wa serikali au hata kiongozi yeyote kanisani lakini Sio hadharani anatakiwa kuambiwa Kwa Siri ndani ya vikao kuwa hapa na hapa sio

Viongozi wakubwa wa dini wanaojielewa kama Kardinali Pengo,Mufti wa Bwakata na Shehe Mkuu wa Bakwata Zuberi na Askofu Mkuu wa KKKT Malasusa huonya sana na huwezi Ona wako Wakienda vyombo vya habari ila utashangaa maraisi wenyewe wanatimua mbio wanaenda kuwaona ofisini Kwao .Hutawaoba Wala kujikomba kwenda Ikulu Viongozi wenyewe ndio huenda

Magufuli mwenyewe na ubabe wake alikuwa akitimua mbio kwenda pale Azania Kwa Malasusa na Kwa Pengo na Shehe Mkuu wa Bakwata

Hiyo timu ya watu watatu wanajua Nini maana ya kuwa kiongozi wa dini si kujikomba na ukiona Kuna jambo hufoki vyombo vya habari unamwambia njoo ofisini kwangu na Raisi au Waziri atatimua mbio hatari kuitika wito

Viongozi wengi wa dini hawana hadhi ya kumwita Raisi au Waziri au Mkuu yeyote wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa njoo ofisini kwangu walishapoteza hiyo hadhi si rahisi wakamwita hata mjumbe wa nyumba kumi tu ajieleze Kwao au kumuonya haendi

Hao watatu wamejenga hadhi za juu sana ambayo akina Askofu Shoo nk hawajaijenga
Hao wote uliowataja ni vibaraka wa CCM na wafiki wa kutisha
 
Hao wote uliowataja ni vibaraka wa CCM na wafiki wa kutisha
Kifupi Hadi Mwamposya anaheshimiwa na maraisi na mawaziri kuliko watu kama Askofu Shoo nk wasomi wabobezi kwenye theology ni aibu

Mzee Mwasapile wa Kikombe Cha Babu hadhi yake kubwa
Kwa Hadi viongozi wakubwa serikalini kuliko watu kama Askofu Shoo au Bagonza nk wabobezi wa theilojia ni aibu Kwao

Kuonya Kuna protocol hata baba Yako akikosea au mke huwezi enda mkutano wa hadhara kusema mke kikojozi msimuone anajipodoa hivyo kikojozi
 
Suala siyo kutofautiana na serekali,tatizo nipale viongozi wa dini mnapogeuka kuwa kama misukule wa serekali kwa kutumikishwa na serekali zaidi ya kumuogopa Mungu aliyewaita kumutumikia na mwisho wake munakutwa na viroba vya fedha za escrow.
 
Biblia baadhi ya sehemu ili badilishwa na wahuni enzi za rumi ,ili serikali ya rumi kuitawala dunia vizuri.

Bahati mbaya waamini hawasomi maandiko na wakisoma hawayafanyii utafiti na uchambuzi yakinifu.

Mazwazwa.

Ila KKKT itakuja pasuka mbeleni

Mimi nipo hapa
Biblia ilifanya nini?ilibadilishwa?
 
Back
Top Bottom