SDP_TZ_Mpya
Senior Member
- Jun 21, 2013
- 166
- 77
Sijui katiba inampa Rais nguvu kiasi gani kulizidi nguvu Bunge la Ana Makinda!!!
Lakini kitendo cha Rais Kikwete kutumia fedha za maskini wa nchi hii ambao watoto wao hukalia magogo mashuleni na kufa kwa kukosa kinga na dawa kwenda AU kufanya maamuzi ya kujilinda yeye binafsi kimenishangaza. Na watanzania tumelikalia kimya as if ni sawa.
Angalau Kenya walijadili bungeni na angalau kulikuwa na ushiriki wa wananchi kupitia wawakilishi wao.
Kwa hapa Tanzania, Rais aliamka asubuhi na kupanda ndege yetu ya gharama aina ya Gulfstream akiwa na wasaidizi lukuki kwenda Ethiopia kuamua ICC isimguse kwa lolote baya alilo au atakalotufanyia hadi 2015 endapo ataamua kutoka madarakani.
Pia, uamuzi wake wa kumlinda Uhuru na Ruto ilhali wakati wanagombea tayari kesi zao zilikuwa zimeshafunguliwa The Hague, kule The Netherlands haukuwashirikisha watanzania. Wengi tungepinga kwani muungano wa Jubilee (Kikuyu na Kalenjini) uliundwa ili kui-circumvent ICC. Mbona Kikwete na wenzake hawakutumia busara ya sasa kuwashauri wasigombee hadi kesi zao kule ICC ziishe!
Kwa maamuzi yao kule Addis Ababa, kweli akina Mu-7 watatoka madarakani?
Katiba ya sasa itenganishe mambo binafsi ya Rais na ya nchi. Kwani kushtakiwa ICC ni jambo binafsi la mtu husika kwa aliyowatendea watu wake. Kamwe sio suala la nchi. Hivyo,kutumia raslimali zetu ndogo kutapanya kwa ajili ya kujilinda binafsi dhidi ya hujuma zake kwetu sisi wananchi wake tena bila idhini ya Bunge ikomeshwe.
Tena, kibaya zaidi ni uamuzi wa Kikwete kuungana na wenzake ku-suspend or amend Roma Convention ambao uliridhiwa na Bunge letu bila idhini yake ni kufifisha nguvu za Bunge na kutangaza mgogoro nalo.
Makinda na Ndugai mpooo!!!?