Bunge likiendelea na msimamo huu nchi hii itasonga mbele

Bunge likiendelea na msimamo huu nchi hii itasonga mbele

Wabunge wa CCM wameamua kufanya kazi zao ipasavyo. Tuliwaachia sana CHADEMA wakitamba. Sasa chadema wamekuwa watazamaji
Kwa hiyo na wewe unakubaliana na Bashe kwamba UCHUMI UMEYUMBISHWA NA SERIKALI!?
 
Nimeamin kibajaj ana miguu mitatuu...hawez simama na miguu miwili .........kwa p......ba zake mmmmhhhh......
 
Mimi. Nauliza hivyo. Nchi hii. Waziri wa michezo. Ni Nani? Hivo. Hawa wana siasa wetu wanajuwa nn maana ya michezo. Hivyo Vijana mnatumiwa kwenye mambo mengi lakin sioni. Michezo kukua katika nchi yetu leo wazir anashindwa hata kuanzisha mashindano yoyote kwa vijana
Leo. Wenzetu kenya wanakwenda kwenye mashindano ya dunia kwa mchezo wa Rugby sisi hata fahamu hakuna. Kazi ya. Siasa wakati leo. Ethiopia kenya kuna watu matajir sababu ya mbio Na mpira hapo tanzania toka naskia mpaka nazeeka. Mchezaji mmoja. Ndo anaweza kujivunia michezo. Samata pekee yake. Bas tuna shindwa kuandaa japo kitu katika ngazi ya vyuo. Wakati michezo ni moja ya ajira na moja katika kukusanya kodi
 
Binafsi naungana na wewe katika sababu ya pili ya juwa ni ukata wa fedha mifukoni mwao uliosababisha baadhi yawabunge wa ccm kuwa wapinzani kwa muda, hakika huko mitaani pengine biashara zao zimegoma kwenda, mtu ambaye hakika ana nia ya dhati huwa hayumbishwi na jambo lolote na yuko tayari kufanyiwa lolote juu ya kile anachokiamini, kwa mantiki ni kuwa kama hawa wabungwa ccm wqngekuwa na nia ya dhati tungeiona tokea awali lakini kuibuka leo ja kusema ya kuwa wamesukumwa na hali halisi ya taifa kwangu mimi bado sijashawishika, wengi wao wanachokifanya ni kutafutia matumbo yao na ndio maana wako tayari kupaka rangi nyeupe na kuwa nyekundu wakati inajulikana kabisa kuwa ni nyeupe toka awali
 
Wabunge wa ccm wamejawa na unafiki mpaka machoni. Ukitaka kujua subir uone kweny kupitisha muswada wa habari.
 
Wabunge wa CCM wameamua kufanya kazi zao ipasavyo. Tuliwaachia sana CHADEMA wakitamba. Sasa chadema wamekuwa watazamaji

Hakuna wabunge wanafiki kama wabunge wa ccm maana wao ndio hupitisha hayo madudu halafu baadae yanakuja kuwanyonga wenyewe mapovu yanaanza kuwatoka
 
IROKOS;
Nami ninasema; Isssue sio kuwa na ujasiri kusema, siwaamini maccm! Ni nguvu ya soda tu hiyo. Wakiitwa kule ukumbi wa Msekwa, wakirudi wanakuwa "Baridiiiiii" ka maji ya mutungi. Nimesema; Wako wapi kina Kangi???? Keleeeleeee mwisho Kimyaaaaa. Hatuwasikii teena

Sikatai wa aina hiyo wapo wengi, ila kuna baadhi (mfano huyu Bashe) wameenza hivi tokea mwanzo, au yule mbunge Kessy wa kule Rukwa, pamoja na kuzibwa midomo mara kwa mara bado kuna misimamo yake ameendelea kuisimamia.
 
Wap
Habari wakuu,

Nimesikia michango ya wabunge wa CCM wakati wakichangia hotuba ya Waziri wa fedha ya mapendekezo ya Mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 na mwelekeo wa Bajeti.Katika michango ya baadhi ya Wabunge wa CCM haswa Ndg.Hussein Bashe (Mb) na Ndg. Ahmed Salum (Mb) nimetiwa moyo na michango ya wabunge hawa na kuona kuwa sasa Bunge linakwenda kujirejeshea heshima ambayo ilijipotezea.

Ninasema haya kwa kuwa tumezoea kuwaona wabunge wa CCM wakikubali na kubariki kila jambo lililosemwa na Serikali hata kama wanajua suala hili si la kweli ama linakinzana na maslahi mapana ya wapiga kura wao/wananchi.Hali hii ilizoeleka sana hata kufikia kuwaambukiza makada wa chama hicho kikongwe kusini kwa jangwa la shahara wakawa wanshangilia kila jambo la serikali hata kama halipaswi kuungwa mkono.Tumekuwa tukiona hata hapa JF makada wa CCM wamekuwa wakipinga threads zinazokosoa mwenendo wa serikali hususani muelekeo wa kiuchumi wa nchi na kuja na majibu mepesi kama; matajiri wameficha Pesa ,mara wasiofanya kazi ndo wanaolalamika kuhusu uchumi, mara mlizoea vya kunyonga na maneno mengine kama hayo.

Sasa, hali iliyojitokeza Bungeni kwa Siku hizi mbili kwa wabunge wa CCM kuanza kusema ukweli na kuungana na wabunge wa vyama vya upinzani kukosoa au kuirekebisha Serikali kunatia moyo na kuona kuwa Bunge lenye nguvu na lenye kujua wajibu wake linakuja Tanzania.

Lakini pamoja na kufurahishwa na michango ya wabunge hao wa CCM ambao wamechangia kwa uchungu na kupendekeza nini kifanyike ili tusonge mbele kiuchumi huku wakishangiliwa na wabunge wa kambi zote hawakusita kuonesha kuwa hali ya uchumi ni mbaya hadi Bungeni.Hili linanifanya nihisi mambo yafuatayo :-

1.Labda wabunge hawa wa CCM wanasukumwa na ukata uliowagusa wao binafsi pale Bungeni ndio maana wameungana na sisi wanyonge. Kama ni kweli watakuwa wamesukumwa na ukata basi ni maombi yangu kwa hali ya kiuchumi iendelee kuwa mbaya zaidi huko Bungeni ili waungane nasi makabwera katika kuisimamia Serikali kwa maslahi mapana ya nchi na si matumbo yao pekee.

2. Kama watakuwa wanasukumwa na dhamira ya dhati basi Mungu awabariki na kuwapa ujasiri zaidi wa kulitetea Taifa la Tanzania.

Ni rai yangu kwa wabunge wote wajitafakari upya na kujikumbusha wajibu wa Mbunge ni upi.Kazi yao ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali, wajue kuwa walikuwa wanatukwaza sana pale walipokuwa wanavaa nafasi ya kuitetea Serikali dhidi ya wananchi.

Mungu awatangulie wabunge wote muanze kuiona kweli na kusema ukweli ili tupate maendeleo tunayoyataka.

Mungu ibariki Tanzania.

Wamewahi kuwapo wabunge wa namna hii kwenye chama tawala. Kina marehemu Filikunjombe na pia Kangi Lugola. Shida kubwa hua ni kwenye kupiga kura wote huitikia ile sauti kama ya chura regardless ya mchango wao.
 
Tuseme mara ngapi jamani kuwa KAMWE Usimwamini mwanasiasa hata kama ni babako mzazi? Hawa utashangaa nao wapo wanapigania maslahi yao; na upepo ukibadilika nao wanabadilika. Si ajabu ni mapandikizi ya Lowassa na wanajua wanachokifanya. Expect nothing from a politician and you will never be disappointed!
Ewaaaaaaaaa! safi sana kwa kuliona hilo! mapandikizi ya Lowassa ni yale tu yanayonena ukweli! Lowassa ni mtu wa watu.
 
Sikatai wa aina hiyo wapo wengi, ila kuna baadhi (mfano huyu Bashe) wameenza hivi tokea mwanzo, au yule mbunge Kessy wa kule Rukwa, pamoja na kuzibwa midomo mara kwa mara bado kuna misimamo yake ameendelea kuisimamia.

IROKOS;
Ngoja tuingie kwenye kuzipiga zile kura kwa jambo nyeti la kitaifa. Spika aseme sasa ni kura za wazi. Hayupo mwenye ubavu huo. Sio Kessy wala Bashe. Wote wanakuwa nalo moja, walilotoka nalo kuleeee, Party Caucas!! Upo. tumewaona si mara moja si mara mbili. Wabunge wa ccm hawana utaifa ndani yao bali u Caucas tu. Hii ni mbaya mno!!! Wabunge maslahi tu hao, na wamewaloga wapiga kura wao kiasi kwamba wamechukua fikra zao na wanawawazia. Hakuna mpiga kura wa ccm mwenye uwezo wa kufikiri.
 
Hakuna mpiga kura wa ccm mwenye uwezo wa kufikiri.
Nimeipenda hii statement yako mkuu. Hata hivyo ni statement ya pupa kidogo kwa sababu inakiuka kanuni mojawapo muhimu sana katika mambo ya siasa: KAMWE USIMLAUMU MPIGA KURA !!!

Ukiona kura zako hazikutosha kaa chini na ufanye upembuzi yakinifu. Kwa nini hazikutosha? Mikakati yako ya ushindi ilikuwa sawa? Mgombea wako alikuwa sahihi kiasi kwamba hakuwachanganya wapiga kura? Sera zako je? Kampeni zilipigwaje? Kuna lolote ambalo ungebadilisha ili kupata ushindi? Baada ya hapo unakaa chini na kuanza kupanga mikakati ya uchaguzi ujao. Lakini ukikimbilia tu kulaumu wapiga kura ni wazi kuwa hujajifunza lolote wala kukomaa katika siasa na kusema kweli utaendelea kushindwa tu tena na tena.
 
Bunge ndio kazi yake. ..kulilia posho n.a. kujipendekeza hiyo kazi sijui nani aliwapa
 
Kwa sasa hakuna zambi ninayoogopa kuitenda kama kumuamin mwanasiasa.. huyu mtu ni zaid ya shetani.. mtu unataka kumsifia mbunge kuwa kabadilika hahahahaha shetani ananjia nyingi sana za kumlagai binadamu.
 
Back
Top Bottom