Bunge likiendelea na msimamo huu nchi hii itasonga mbele

Bunge likiendelea na msimamo huu nchi hii itasonga mbele

maendeleo kwa tanzania msahau sio kwa karne hii,nchi imetawaliwa na siasa katika kila taasisi watu hawajitambui hawajui wajibu wao wala nafasi zao katika jamii,siasa inaingizwa katika kila maamuzi muhimi ya kujenga nchi na kusuka mifumo yamaendeleo,

ili nchi iendelee kunatakiwa mifumo ya maendeleo ili kueka mifumo ya maendeleo ni lazima taasisi zijitambue na kujua wajibu wao na kueka siasa pembene na kuacha kuendeshwa kwa amri za watu wengine.

nchi hii mtu akisema ukweli anashikishwa adabu ili asijielewe na asiweze kutekeleza wajibu wake hapa maendeleo sio kwa karne hii,tanzania itakayoendelea hatutaiona sisi labda wajukuu wa wajukuu zetu
 
Wabunge wa ccm wapo kimaslahi, hawajawahi kutetea taifa letu zaidi ya "kuyasimamia matumbo" yao.

I can tell, hawa jamaa wameshikwa pabaya kama wengine wengi walivyoshikwa pabaya.

Wabunge wa ccm hawawezi kutetea nchi hii hata siku moja, unless serikali iwanyime 'kula' na kuwabana katika 'biashara' zao. Ni baadhi ya hawa wabunge tuliambiwa wanajihusisha na 'ngada', biashara haramu kama ujangili wa wanyama wetu, leo hii kaja mtu anayewabana, hawana pa kupumulia, unadhani wataacha kuiponda serikali yao?

...whatever the case, hata kama uchumi umedorora lakini bado hawa wamebanwa sana kufanya 'yale mambo yao'....
 
Habari wakuu,

Nimesikia michango ya wabunge wa CCM wakati wakichangia hotuba ya Waziri wa fedha ya mapendekezo ya Mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 na mwelekeo wa Bajeti.Katika michango ya baadhi ya Wabunge wa CCM haswa Ndg.Hussein Bashe (Mb) na Ndg. Ahmed Salum (Mb) nimetiwa moyo na michango ya wabunge hawa na kuona kuwa sasa Bunge linakwenda kujirejeshea heshima ambayo ilijipotezea.

Ninasema haya kwa kuwa tumezoea kuwaona wabunge wa CCM wakikubali na kubariki kila jambo lililosemwa na Serikali hata kama wanajua suala hili si la kweli ama linakinzana na maslahi mapana ya wapiga kura wao/wananchi.Hali hii ilizoeleka sana hata kufikia kuwaambukiza makada wa chama hicho kikongwe kusini kwa jangwa la shahara wakawa wanshangilia kila jambo la serikali hata kama halipaswi kuungwa mkono.Tumekuwa tukiona hata hapa JF makada wa CCM wamekuwa wakipinga threads zinazokosoa mwenendo wa serikali hususani muelekeo wa kiuchumi wa nchi na kuja na majibu mepesi kama; matajiri wameficha Pesa ,mara wasiofanya kazi ndo wanaolalamika kuhusu uchumi, mara mlizoea vya kunyonga na maneno mengine kama hayo.

Sasa, hali iliyojitokeza Bungeni kwa Siku hizi mbili kwa wabunge wa CCM kuanza kusema ukweli na kuungana na wabunge wa vyama vya upinzani kukosoa au kuirekebisha Serikali kunatia moyo na kuona kuwa Bunge lenye nguvu na lenye kujua wajibu wake linakuja Tanzania.

Lakini pamoja na kufurahishwa na michango ya wabunge hao wa CCM ambao wamechangia kwa uchungu na kupendekeza nini kifanyike ili tusonge mbele kiuchumi huku wakishangiliwa na wabunge wa kambi zote hawakusita kuonesha kuwa hali ya uchumi ni mbaya hadi Bungeni.Hili linanifanya nihisi mambo yafuatayo :-

1.Labda wabunge hawa wa CCM wanasukumwa na ukata uliowagusa wao binafsi pale Bungeni ndio maana wameungana na sisi wanyonge. Kama ni kweli watakuwa wamesukumwa na ukata basi ni maombi yangu kwa hali ya kiuchumi iendelee kuwa mbaya zaidi huko Bungeni ili waungane nasi makabwera katika kuisimamia Serikali kwa maslahi mapana ya nchi na si matumbo yao pekee.

2. Kama watakuwa wanasukumwa na dhamira ya dhati basi Mungu awabariki na kuwapa ujasiri zaidi wa kulitetea Taifa la Tanzania.

Ni rai yangu kwa wabunge wote wajitafakari upya na kujikumbusha wajibu wa Mbunge ni upi.Kazi yao ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali, wajue kuwa walikuwa wanatukwaza sana pale walipokuwa wanavaa nafasi ya kuitetea Serikali dhidi ya wananchi.

Mungu awatangulie wabunge wote muanze kuiona kweli na kusema ukweli ili tupate maendeleo tunayoyataka.

Mungu ibariki Tanzania.
Umesikiliza kupitia radio gan au television gan??
 
Maana mm nataman sana kusikiliza bunge ila kipind cha maswal na majibu tu kikiisha wanakata
 
Ningelikuwa mgeni wa wabunge wa ccm ningekuunga mkono. Wakiitwa kikaoni tu, kwisha kelele zao, Wapo wapi kina Kangi?? Bashe akiambiwa wamegundua si raia si atanyamaza kabla ya kupumzika?? Acheni kumpaisha, hajasema kuwazidi wengine.
Ukweli aliosema kila mtu anauona.
 
Lakini SHIMBA YA BUYENZE bunge ndiyo lilitakiwa kuwa hivi, hasa wabunge wa chama tawala. Hii ni tofauti na ilivyokuwa mwanzo, na inatakiwa waendelee hivi hivi kwani serikali pia itaongeza ufanisi katika kuandaa sera na kuzisimamia.

Siasa za Tanzania zimeshikiliwa na chama tawala na nafasi ya CCM ndani ya bunge imeanza kuonekana. Inatakiwa tufanye siasa za kisasa za kukosoana na kusimamia maslahi ya taifa.

Sidhani kama kuna kitu nyuma ya pazia, hata kama kipo! Serikali inatakiwa iwe makini na ichukue baadhi ya hoja za wabunge ambazo zina tija kwa taifa.
Nimeiandika hii nikiwa nimeghafilika. Nina bwana mdogo mmoja hivi kakosa mkopo japo ana divisheni wani nzuri sana na wazazi wake hawana uwezo kabisa kabisa. Mtoto wa mkulima ukimnyima elimu basi umemmaliza na daima atabakia katika tabaka la watwana daima dumu. Ndiyo maana nikasema MIANASIASA hii haitabiriki. Leo linatetea watu kesho na kesho kutwa likipata lilichokuwa linakitafuta basi linasahau ahadi zote. Nasayaga sana na gupinihala. Nilekejage nkoyi!
 
Serikali ishukru Mungu hakuna Bunge live otherwise pangechimbika
 
Ningelikuwa mgeni wa wabunge wa ccm ningekuunga mkono. Wakiitwa kikaoni tu, kwisha kelele zao, Wapo wapi kina Kangi?? Bashe akiambiwa wamegundua si raia si atanyamaza kabla ya kupumzika?? Acheni kumpaisha, hajasema kuwazidi wengine.
Ukweli aliosema kila mtu anauona.

Issue siyo ''Ukweli aliosema kila mtu anauona''...Issue ni kuuona ukweli na hali halisi na pia kuwa ujasiri wa kuyazungumza bungeni kama alivyofanya Bashe...
 
Wabunge wa CCM wameamua kufanya kazi zao ipasavyo. Tuliwaachia sana CHADEMA wakitamba. Sasa chadema wamekuwa watazamaji
Aisee, maoni haya ni yako mkuu au account iko hacked?
 
Wabunge wa CCM wameamua kufanya kazi zao ipasavyo. Tuliwaachia sana CHADEMA wakitamba. Sasa chadema wamekuwa watazamaji
Hahahaaa lizaaaa seriously wallah katika watu waliokatwa mishipa ya soni nyie jamaa mnaongoza mnaweza mkafariji mgonjwa huku mnalisha over dose na mkaona poa tu.
 
Wabunge wa CCM wameamua kufanya kazi zao ipasavyo. Tuliwaachia sana CHADEMA wakitamba. Sasa chadema wamekuwa watazamaji
Ila nawe ling'ombe haswaaaa,kwani huwezi changia bila kuisema chadema???
 
Kuna muda unaweza kulia kwa jinsi tunavyosahau haraka. Wanasiasa wetu wengi ni wanafiki. Acheni mihemko ya hotuba za hisia. Waulizeni wao walipopata nafasi walifanya nini? Sikatai kukosoa au kuhoji lakini kama huna unafiki na unajua historia ya siasa zetu unaweza kumzaba mtu kofi!
 
Ningelikuwa mgeni wa wabunge wa ccm ningekuunga mkono. Wakiitwa kikaoni tu, kwisha kelele zao, Wapo wapi kina Kangi?? Bashe akiambiwa wamegundua si raia si atanyamaza kabla ya kupumzika?? Acheni kumpaisha, hajasema kuwazidi wengine.
Ukweli aliosema kila mtu anauona.
Boss ukisoma vizuri uzi huu utaona nilivyoweka wazi wasiwasi wangu juu ya hali inavyoendelea Bungeni.Mimeonesha kuna uwezekano wanafanya vizuri baada ya maslahi yao kuguswa au wanasema kwa dhati wamechoshwa na uongo.

Kama watakuwa wanasema kimaslahi hii ni mbaya lakini kama watakuwa wameamua kuuona ukweli ni jambo jema na ndio maana nimemalizia uzi huu kwa kuwaombea waione kweli.
 
Nyie subiri mchango wa kibajaj tuone..
 
Issue siyo ''Ukweli aliosema kila mtu anauona''...Issue ni kuuona ukweli na hali halisi na pia kuwa ujasiri wa kuyazungumza bungeni kama alivyofanya Bashe...

IROKOS;
Nami ninasema; Isssue sio kuwa na ujasiri kusema, siwaamini maccm! Ni nguvu ya soda tu hiyo. Wakiitwa kule ukumbi wa Msekwa, wakirudi wanakuwa "Baridiiiiii" ka maji ya mutungi. Nimesema; Wako wapi kina Kangi???? Keleeeleeee mwisho Kimyaaaaa. Hatuwasikii teena
 
Back
Top Bottom