Bunge liitishe kikao cha dharura kujadili kufungwa kwa ubalozi wa Denmark 2024

Kama tulivyosikia Denmark ambae ni moja ya nchi mshirika mkubwa na mdau wa maendeleo wa nchi yetu "Development partners" wanafunga ubalozi wao Tanzania ifikapo 2024.

Denmark walianzisha ushirikiano wa kimandeleo na Tanzania mwaka 1963 miaka miwili baada ya nchi yetu kupata uhuru wake mwaka 1961.

Kupitia mfuko wake wa maendeleo ujulikanao kwa jina la DANIDA Denmark imekuwa mdau mkubwa ambae amekuwa akitoa fedha za maendeleo kwenye maeneo kama haki za binadamu, ukuzaji demokrasia, utawala bora, utulivu na usalama, vita dhidi ya ugaidi, misaada ya wakimbizi na mazingira.

Pia DANIDA imekuwa ikisaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Kupitia mfuko wake wa Danida Fellowship Centre nchi hiyo imekuwa ikifadhili shahada za uzimivu katika masuala mbalimbali kwa baadhi ya wanafunzi kutoka Tanzania na nchi zingine zinazoendelea.

Habari za kufungwa kwa ubalozi wake Denmark ni za kustua kwa wengi kwani zinagusa kila anehusika moja kwa moja na misaada yake kwa nchi zinazoendelea na pia wale wanohusika moja kwa moja na usimamizi wa mfuko huo kwa Tanzania, maofisa ubalozi ambao wengi wamezoea nchi yetu na hata kuzungumza kiswahili sanifu na pia watumishi wa kitanzania ambao wamekuwa wakifanya kazi ubalozi hapo.

Sababu kubwa ya Denmark kufunga ubalozi wake imesemwa kuwa ni kutaka kupata muda wa kujipanga upya na kutengeneza upya mikakati yake ya sera ya nje na mwelekeo wa mkakati mpya wa dunia au "New Global Stretegy".

Lakini pia ni suali la kuuliza je kwanini Denmark ije na uamuzi huo sasa?, je wamegundua kitu gani? na je, wataendelea kutoa msaada kwa Tanzania baada ya 2024?

Au je, wameona tunatumbua tena fedha zao ambazo kuna kipindi zilikuwa zikitumika ipasavyo?

Haya ni masuali ambayo yanapaswa kujibiwa na waziri mhusika wa mambo ya nje balozi Mulamula na maelezo hata ya alert tu kuwa Denmark kufunga ubalozi wao ulodumu nchini Tanzania tangu mwaka 1963.

Lakini cha msingi kwa sasa ningependa kushauri kwamba hili ni jambo la dharura, kuwa mdau wetu mkubwa wa maendeleo Denmark anafunga ubalozi wake ifikapo 2024.

Hivyo Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lingechukua hatua za kuitisha kikao cha dharura kujadili uamuzi huo wa Denmark na kwamba ni hatua zipi zitafuatwa kujaribu kutafuta kama Denmark inaweza kubadili msimamo wake huko mbele wa kuisaidia Tanzania kupitia njia zingine.

Waziri wa mambo ya nje anapaswa kutoa taarifa rasmi ya serikali bungeni kuelezea uamuzi huo wa Denmark.
Mawazo ya kichadema. Ovyo sana..eti bunge lijadili kwa nini denmark wafunge ubolozi. Kwanza wamesema wanafunga ofisi ya ubalozi sio kuvunja uhusiano. Ni maamuzi yao sisi hatuwezi lazimisha. Bila shaka baada ya hapo watawakilishwa na nchi nyingine. Siku uingereza wakisema wanafunga ubalozi sijui hao vibaraka wa chadema watasemaje. Wanaweza hata kusema serikali ijiuzulu ufanyike uchaguzi upya 😂😂. Wakongwe watakumbuka nchi hii iliwahi kuvunja uhusiano na uingereza kwa kuwasaidia walowezi wa rhodesia kwa miaka karibu au zaidi ya kumi na nchi ikaendelea kuwepi bila shida. Kushikwa kiwewe kutokana na uwezekano wa kukosa misaada ndio kitu kinawapa shida vibaraka. Misaada ambayo wala haijaisaidia nchi kutoka kwenye umaskini.
 
Back
Top Bottom