Bunge laumbuka kisa tozo ya miamala

Sijaona utata ila naona mantiki ya kile alichoongea ni sahihi tunahitaji kujitegemea isipokuwa uhakika wa hizo fedha zetu upo wapi..?

Mi sidhani Kama Kuna mtu anaweza kukataa kulipa hizo tozo swala ni hizo tozo zitumike kuleta maendeleo kweli na sio viongozi kujinufaisha matumbo yao tu.
Kabisa
 
Kauli ya Mhe. Inatoa picha ya Nini tutarajie huko tuendako...our house is not in order...tutafahamu mengi zaidi ukiwemo mtikisiko wa kisiasa...watch out
Naiona ccm ikiwa dhooofu chini ya mwenyekiti
 
Pesa za covid tuliambiwa zinajenga madarasa, tozo madarasa, kodi madarasa...hata haieleweki kipi ni kipi.

Tatizo letu halijawahi kuwa kutoa tozo ila matumizi ya tozo.

Wanatuhubiria deni ni stahimilivu kumbe ndani ya nafsi zao wanaujua ukweli kwamba hali ni mbaya.
 
Wacha waendelee kutuficha lkn siku tukianza kudaiwa itajulikana tu .

Ni sawa na pembe la ng'ombe tu halifichiki.
 
Mkiambiwa ni mazuzu muwe mnaelewa.............mazuzu wanachoweza kufanya ni kubomoa kwa mikono yao wenyewe nyumba wanayoitegemea kwa ajili ya kuishi wao na vizazi vyao, hiyo ndo kazi ya maana ambayo zuzu anaweza kufanya na anajisikia yupo very satisfied.....
 
Watanzania sasa wamepata uhakika wa nini bunge linafanya.

Kupitia spika wa bunge Job Ndugaye amesema kuwa tozo zote zilipitishwa na bunge kwa ulazima.

Watanzania watake wasitake miamala lazima itozwe tozo tu.
Hii kweli ni nchi huru inayo heshimu haki za binadamu.
View attachment 2060116
Nimeisikiliza hiyo clip zaidi ya Mara tano ili niweze kumuelewa mhe Spika na nimemuelewa, na ukweli ni kwamba anachokisema ni sahihi lakini pia hayo aliyoyasema yawe na dhamira ya kweli na ya siku zote !! Naamini tutavuka salama !!
 
Kuyaamini maneno ya huyu mzee wa fulsa ni kuikosea heshima akili yako
 
Sasa kama mmeamua kujenga madarasa kwa kutubanabana, iweje tena huyo mama anakopa? hizo anazokopa anapeleka wapi, au ndio hizo anazotumia kununulia hotel ya Ngorongoro wildlife kwa kichaka cha albawdy?
Hapo Sasa!! hivyi ni pesa ipi inajenga madarasa ya Corona au ya tozo?au tualiwa kekundu zinaenda kwenye account zao huko majuu?
 
Sijaona utata ila naona mantiki ya kile alichoongea ni sahihi tunahitaji kujitegemea isipokuwa uhakika wa hizo fedha zetu upo wapi..?

Mi sidhani Kama Kuna mtu anaweza kukataa kulipa hizo tozo swala ni hizo tozo zitumike kuleta maendeleo kweli na sio viongozi kujinufaisha matumbo yao tu.
Hapa ndo huwa nawashangaa Wana CCM. Hivi nyie mnamtetea Nani wakati mwananchi asiye na uhakika wa mlo wake anakamuliwa TOZO kwenye hela kidogo aliyotumiwa na mwanae halafu mnasema Hakuna asiyetaka kulipa TOZO? Hivi kweli watanzania hawa masikini wote wako tayari kukamuliwa na CCM au mnawalazimisha Kwa vile hata wakisema mnawanyonga?
 
Kuna mmoja alisema anafukiza Moshi ndani ya pango la wahuni na kwamba atatoka mmoja baada ya mwingine
Huo ndiyo ukweli na kuhakikisha hilo sasa hivi tune Radio one usikikize hotuba ya mwenyekiti utagundua kuwa hali siyo shwari
 
Back
Top Bottom