Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Ofisi ya Spika wa Bunge ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake.
DNjAyROXkAADM9U.jpg small.jpg

Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.

Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.

Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:

“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”

Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.

Imetolewa na: Ofisi ya Spika S.L.P. 941

DODOMA

Ofisiya Bunge S.L.P 941 DODOMA

Comments
 
Kwa hisani ya ofisi ya MAZWAZWA na VIKARAGOSI vyote vya ofisi hiyo pale mtaa wa lumumba.

View attachment 621949 Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.

Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.

Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapa chini....

Ofisi ya Spika ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake.

Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.

Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.

Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:

“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”

Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.

My Verdict,
Spika jana alisema hajapokea Barua ya Nyalandu lakini hakuzungumzia kabisa kuhusu Barua kutoka CCM. Leo Ofisi yake inaibuka na kudai kuna barua kutoka kwa Katibu wa CCM iliyokuja Mapema kuliko ya Nyalandu. Hapa nadhani kuna kitu hakiko sawa.
 
CCM ndio mwalimu wa siasa hapa nchini na Afrika kwa ujumla wake kumbuka hilo.
Hoja yako haina tofauti na walimu waliofundisha Rais kuanzia shule ya msingi mpaka chuo. Mwisho wa siku wamebaki kuwa walimu ila wameongozwa na mwanafunzi wao. Sasa chukua mfano huo kisha uvalishe nguo ya Ccm na Cdm, uniambie yupi afatwe kwa sasa? Mwalimu aliyemfundisha rais, ambaye hana uhakika hata wa mafao yake baada ya kustaafu au rais anayeongoza nchi kwa sasa na mwenye hatma ya maisha ya mwalimu aliyemfundisha?
 
Back
Top Bottom