Bunge la Ulaya(EU) lajadili hali ya kisiasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
Umoja wa Ulaya(EU) wamwambia Rais wa Tanzania mama Samia Suluhu amwachie huru kutoka jela kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA mheshimiwa Freeman Mbowe.

============


Mbowe EU Samia.JPG

Mwenyekiti wa kamati wa mambo ya nje kwenye Bunge la Ulaya, David James McAllister amesema anawasiliana na watu wengi nchini Tanzania ambapo amesema wapo kwenye hali ambayo viongozi, wanachama na wafuasi wa upinzani wanakumbana na udhalilishaji, kushikiliwa kinyume cha sheria na vitisho.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mambo ya Afrika kutoka umoja wa Ulaya, Laranjinha Rita amesema kuna sababu za matumaini Tanzania ambapo miezi ya karibuni kumekuwa na mwanzo mzuri kwa Rais Samia nyumbani na kimataifa ambapo ametambulisha baadhi ya mabadiliko.

Laranjinha amemueleza Rais Samia kwenye uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari na mabadiliko hayo yamepokelewa vizuri na jamii ya kimataifa. Pia ameongelea ruhusa ya kurudi shuleni kwa wanafunzi waliopata ujauzito.

Laranjinha amesema pamoja na hatua zilizofikiwa kuna mapungufu machache ikiwemo demokrasia ya vyama vingi ambapo hakuna uwakilishi wa upinzani kwenye bunge, mwenyekiti wa chama cha upinzani kushikiliwa na umoja wa ulaya itaendelea kufatilia kwa karibu.

 
Kwani hawajui kwamba Tanzania ni nchi huru? Wajadili haki za binadamu Ulaya ndio eneo lao. Wana mengi ya kujadili sio kujiingiza mambo ya nchi zingine.
 
Hao wataonesha makucha yao Kama hushirikiani nao lakini kama umefungulia milango yao Wala hawana muda na wewe
 
Hawa mabwana wa lissu naona Wana waya waya,na wamejua bwana yao anaenda kuangukia pua wanaanza kuwashwa
 
Amwachie kwa Sheria ipi?,mahakama ni muhimili waache ufanye kazi zake kwa uhuru
Tatizo mjadala kuvamiwa na mbumbumbu kama wewe. Kwani mahakama ndiyo imemfungulia kesi Mbowe? Na wao hawaiambii mahakama wanaiamnia Executive iliyo chini ya Rais kupitia DPP kuwa kesi yenu ni ya kijinga kwa nini mnaisumbua mahakama?
Toa kesi ya kijinga hiyo kama alivyotoa kesi zile za kina Rwegamalira za uhujumu wa kutunga.
Umeelewa wewe ngumbaru?
 
Back
Top Bottom