Bunge la Tanzania umekuwa muhimili mbovu na usio na tija wala faida kwa Taifa

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Bunge ni chombo ambacho kama kingekuwa kinafanya kazi yake ipasavyo hakika Tanzania ingekuwa mbali sana kwa sasa. Lakin Bunge la Tanzania ni miongoni mwa mabunge ya hovyo na hasara kwa Taifa, halina msaada wala mchango wowote ule kwa taifa hili.

Bunge linatia hasara Serikali kila mwaka. Bunge linakula posho bila michango chanya kwa taifa zaidi ya mipasho na malumbano ya kijinga. Kwa Tanzania bunge ni chombo cha kula posho tu na kupiga meza hakuna ambacho bunge linaweza kufanya chenye tija kwa taifa hili.

Bunge linaamuliwa mambo ya kufanya, Bunge haliwezi kujisimamia katika maamuzi yake lenyewe. Bunge halieleweki lina simamia nini, lipo kama ishara ya Bunge katika taifa. Maamuzi ya Bunge yanaweza kupindishwa hata na Mkuu wa Wilaya au Mkoa na ikiwezekana hata Mwenyekiti wa chama wilaya anaweza kulitunishia misuli Bunge.

Bunge la hivi la nini wakati halina faida kwenye nchi hata kwa 10%? Bora livunjwe pesa za posho na marupurupu mengine ziende kupeleka huduma kwa wananchi maana halina faida na halijui majukumu ya Bunge.

Si spika wa Bunge wala mwenyekiti wa Bunge, si Naibu wala Katibu na wabunge wote wanaojua umuhimu wa Bunge kuwepo.

Nasema hawajui tena hawajui wapo pale kula posho maana bado matatizo katika jamii yapo kwa kiwango kile kile kila mwaka mf.

1. Njia ni za msimu wa kiangazi tu masika hazipitiki na ni tangu uhuru

2. Maji bado shida sehemu kubwa ya nchi tangu uhuru

3. Umeme bado ni shida kwa wiki mnautumia siku tatu au nne tena kwa masaa

4. Huduma za afya na dawa bado shida palepale tangu uhuru

5. Elimu ndio kabisa ipo mahututi

Bunge linasema hivi na kuamua hivi lakini Serikali inafanya hivi na kuamua vile. Bunge hili la nini na linatumia pesa nyingi kujiendesha tena bila faida? Bunge lifutwe na lisiwepo kabisa, halina faida bunge hili.

Nawasilisha
 
Hakuna Bunge Tanzania labda kuna mijitu Mibunge yenye uchu wa hela na kumtukuza mfalme
 
Naunga mkono hoja yako mkuu haina haja, linapoteza muda na kodi zetu.....bunge ni kichaka cha ccm
 
Mulhat Mpunga
Mkuu mijitu mingine inaudhi sijui wanatumia nini kufikiri?
Maana kwa mtu mwenye akili timamu huwezi sema eti tuna Bunge.
Bunge ambalo kazi kuchukua posho na kupga vigelegele hata kichaa anaweza
 
Naona dalili wabunge kubakizwa 2 kila mkoa.CAG report mkuu kafanya shortcut ita wakuu mihimili yote, chukua hatua maamuzi issue kubwa mengineyo PM kayafanyie kazi.Sijui bunge lina kazi gani hapo?! Kapora haki kikatiba bunge simamia serikali
 
.
Hakuna Bunge Tanzania labda kuna mijitu Mibunge yenye uchu wa hela na kumtukuza mfalme
Lifutwe tu ni ujinga
wabunge wamelizoea bunge tena wamelifanya ni sehemu ya kupatia umaarufu madhumuni ya bungr kuwepo hayapo, kila mbunge akienda bungen anawaza leo jikamchambe fulani na mwingine naye anawaza leo nikamzodoe fulani spka na naibu na wanawaza leo mikamkomeshe fulani yaani bunge si bunge tena limejaa wahuni na wasaka tonge hata taifa hawalifikiriii kabisa.
 
Back
Top Bottom