Bunge la Tanzania ndilo linakaa vikao Muda mrefu kwa Dunia nzima

Bunge la Tanzania ndilo linakaa vikao Muda mrefu kwa Dunia nzima

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,504
Reaction score
14,131
Nimetumia muda mwingi kufiatilia vikao vya mabunge ya nchi nyingi Duniani, Mabunge ja Nchi za Jumuia ya Madola na oia Mabunge ya nchi zingine zikiwemo za West Africa, North Africa, Asia na hata South America.

Nilichogundua Bunge la Tanzania lina spendi muda mrefu sana kwenye kinachoitwa kujadili Bajeti. Bajeti yenyewe unakuta ni usanii mtupu na haina tija kwa raia.

Bunge kutumia miezi 3 Mfululizo wakijadili kinachoitwa Bajeti ni muda mrefu sana.

Sijui alieasisi huu mfumo wa Bunge kukaa zaidi ya miezi 3 wakijadili bajeti. Wakati huo wakitumia Billions of Money kwa huo muda wote.

Kuna mantiki gani wanapitisha Bajeti ya kila wizara then wanakuja tena kupitisha bajeti ya Jumla.

Kwa sababu bajeti inayosomwa na Waziri wa Fedha ni majumuisho ya Bajeti za Wizara zote sasa basi kuna maana gani kutumia muda kupitisha bajeti ya kila wizara na baadae waje tena kukaa wapitishe ya jumla yake, maana yake kama ya kila wizara imepitishwa basi ya jumlaa kuu inakuwa imepitishwa automatic.

Bunge lina mchango mkubwa sana kwenye kukuza umasikini nchi hii na pia kwenye matumizi makubwa ya pesa za Umma.
 
Ni utapiamlo wa akili kuamini kuwa Tanzania ina Bunge😁😁😁

 
Bajeti ya siku 365 inajadiliwa kwa siku 90
Walijiwekea mchongo wa kupiga hela, kuna haja ya kufanyia narekebisha wa muundo mzima wa Bunge maana imagine double standard ngapi zimefanyika na hakuna wa kumwajibisha mtu. Ikiwezekana wabunge wawe ni kama wafanyakazi wa mkataba WA miaka mitano walipwe mishahara Tu Kwa kazi ambayo ofisi zake zipo Dodoma
 
Toa uthibitisho wa muda wa hayo mabunge mengine, mfano bunge la Kenya huwa linakaa siku XXX, Algeria siku YYY na kadhalika.

Hapo ndiyo tutaweza kuchangia vizuri.
 
Duuh kumbe?! [emoji15]

Sasa hayo si yatakuwa matumizi mabaya ya rasilimali za Umma?!

Fedha na muda?!
 
Je ukijumlisha na vile vikao vingine vya Mwezi Januari na October if not mistaken itakuwa jumla ni miezi mingapi katika kila mwaka wenye miezi 12 ? [emoji2369][emoji2369]

Tunachambua na kunyumbulisha [emoji442][emoji441]
 
Tuanzie kwa mabunge ya E.A.C countries wao wenzetu wanakutana Kwa namna gani kwa muda gani ?
 
Watapiga kelelee mwisho"muheshimiwa supika naunga mkono hoja aslimia 150🤭"
 
Back
Top Bottom