Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Jana akiwa Bandarini jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alisema huko nyuma kulikuwa na tabia ya bunge kutunga sheria halafu ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kabla ya kuipeleka kwa Rais kusainiwa,wao wanaibadili na kupeleka tofauti na iliyopitishwa na bunge.Akatolea mfano wa sheria ya mafuta ya kupikia kutoka nje iliyotumgwa na bunge,akasema iliyotungwa na bunge siyo ile aliyopelekewa Rais na ofisi ya mwanasheria mkuu.
Kama hii ni kweli,basi ni hatari sana na kama tungekuwa nchi "Serious kwenye masuala serious" bunge lingetoa hoja ya kuundwa kamati teule ya kupitia sheria zote na kuchunguza kama kile ambacho huwa wanachopitisha je ndicho kinachopelekwa kwa Rais ili akisaini?vinginevyo haija haja ya kuwa na bunge!.