Ukweli ni kuwa Bunge liko chini ya Waziri Mkuu na Mahakama iko chini ya Waziri wa Katiba na Sheria, na Wote wako chini ya Rais wa JMT

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,011
142,043
Anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo wengine wanabaki kuwa wanenguaji tu kwenye burudani

Bajeti ya Bunge iko ofisi ya Waziri mkuu kama unabisha angalia nani huwa anapanga tarehe za mikutano ya Bunge

Bajeti ya Mahakama iko Wizara ya Katiba na Sheria

Ndio Shujaa Magufuli akasema Mhimili ni mmoja tu tena umejichimbia chini sana

Jumaa Mubarak!
 
Upo sahihi mkuu mhimili ni mmoja tu bunge na mahakama ni idara chini ya mhimili ndio maana magufuli aliweza kuliagiza bunge nini cha kufanya na mahakama kuliteulia majaji hata wasio na viwango.
 
Na kwakuwa mnayajua haya, sijui kwanini huwa mnaenda mahakamani!
Mahakamani kupata haki labda kwa kesi za wizi wa kuku tena ni raia kapuku dhidi ya raia kapuku.

Kesi hiyo hiyo ikiwa ni raia kapuku dhidi ya kibopa sahau kupata haki hata kibopa akiwa mkosaji.

Kuhusu kesi za serikali dhidi ya wananchi mahakamani tena zilizokaa kisiasa sahau kabisa ushindi kwa wananchi.

Unafkiri Rostam aliropoka kwa bahati mbaya kuhusu majaji wetu?
 
Anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo wengine wanabaki kuwa wanenguaji tu kwenye burudani

Bajeti ya Bunge iko ofisi ya Waziri mkuu kama unabisha angalia nani huwa anapanga tarehe za mikutano ya Bunge

Bajeti ya Mahakama iko Wizara ya Katiba na Sheria

Ndio Shujaa Magufuli akasema Mhimili ni mmoja tu tena umejichimbia chini sana

Jumaa Mubarak!
Hiki sio kitu cha kujivunia reshuffling ya katiba ni muhim san! NB: kwa wenye akili tuu!!
 
Serikali haiwezi kufanya mabadiliko ya mifumo inayoiweka madarakana.

Mwalimu Nyerere alishatuomba radhi kabla ya kututoka, kuwa haikuwa nia yake kutengeneza taifa lenye watu waoga na serikali dhalimu.
 
Anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo wengine wanabaki kuwa wanenguaji tu kwenye burudani

Bajeti ya Bunge iko ofisi ya Waziri mkuu kama unabisha angalia nani huwa anapanga tarehe za mikutano ya Bunge

Bajeti ya Mahakama iko Wizara ya Katiba na Sheria

Ndio Shujaa Magufuli akasema Mhimili ni mmoja tu tena umejichimbia chini sana

Jumaa Mubarak!
Magufuli aliweka wazi nadharia hii siku alipojibu swali la Pasco kuwa kuna mhimili mmoja umejichimbia chini sana na hata hiyo mihimili mingine miwili inautegemea mhimili uliojichimbia kujiendesha. Na nadharia hii inapata uhalali kutokana na ubovu wa Katika yetu inayompa Rais madaraka ya umungu mtu.
 
Na kwakuwa mnayajua haya, sijui kwanini huwa mnaenda mahakamani!
Watu wanaenda mahakamani ili kuweka rekodi kuwa pamoja na udhalimu wa mfumo uliopo wapo waliouona na kuupinga,ipo siku mambo yatabadilika hivyo tutakuwa na mahali pa kuanzia
 
Ukiwa na kesi dhidi ya Serikali basi jua kuwa una wakati mgumu kupata haki...
Labda ziwe kesi ndogo kama za kazi au mambo madogo madogo..

Lakini kesi dhidi ya Serikali mambo makubwa... Jua kwamba una hali mbaya sana katika kupata haki..
Labda upeleke mahakama ya afrika mashariki au AU au za kimataifa
 
Back
Top Bottom