Bunge halitungi Sheria

Bunge halitungi Sheria

Bunge ndiyo linalotunga Sheria. Ukitoa maelezo kuonesha kuwa bunge halitungi Sheria, jua unajiongoza vibaya.

Mswada kwa lugha nyepesi ni mapendekezo. Kwa ivo mapendekezo siyo Sheria.

Mapendekezo yawe ya serikali ama ya mbunge binafsi, ili yawe Sheria ni lazima yapitie hatua kadhaa ndani ya bunge.

Huo mchakato wa kuyageuza mapendekezo kuwa Sheria ndiyo utungaji wenyewe wa Sheria.

Kama mbunge ama Serikali wakaleta mapendekezo Yao (Mswada) na Bunge wakayakataa mapendekezo hayo, basi hayawezi kuwa Sheria.

Na ndiyo maana Rais hutia Saini Sheria zilizotoka bungeni na siyo miswada iliyopelekwa bungeni.

Sasa hoja ya kiwango cha Elimu za wabunge ni jambo jingine kabisa lisiloondoa mamlaka ya kikatiba ya bunge kutunga Sheria.
 
Mfumo haujakaza wasomi kugombea na kuwashinda hao kina Lusinde... wananchi ndio wamepeleka wajinga wenzao wakawawakilishe!
Lakini unawezaje kupima ujinga wa mtu kwa kutumia kiwango cha usomi? Kati ya mwenye shahada ya uchumi na mwenye shahada ya kiswahili ni nani kati ya hao mwenye elimu kuliko mwingine!?
 
Bunge ndiyo linalotunga Sheria. Ukitoa maelezo kuonesha kuwa bunge halitungi Sheria, jua unajiongoza vibaya.

Mswada kwa lugha nyepesi ni mapendekezo. Kwa ivo mapendekezo siyo Sheria.

Mapendekezo yawe ya serikali ama ya mbunge binafsi, ili yawe Sheria ni lazima yapitie hatua kadhaa ndani ya bunge.

Huo mchakato wa kuyageuza mapendekezo kuwa Sheria ndiyo utungaji wenyewe wa Sheria.

Kama mbunge ama Serikali wakaleta mapendekezo Yao (Mswada) na Bunge wakayakataa mapendekezo hayo, basi hayawezi kuwa Sheria.

Na ndiyo maana Rais hutia Saini Sheria zilizotoka bungeni na siyo miswada iliyopelekwa bungeni.

Sasa hoja ya kiwango cha Elimu za wabunge ni jambo jingine kabisa lisiloondoa mamlaka ya kikatiba ya bunge kutunga Sheria.
Rais anasaini sheria au Rais husaini Muswada wa sheria?
 
Waziri wa fedha kaenda na mswada wa hela zikikaa bank miezi 6 zitozwe kodi hiyo itapitishwa Bunge letu lipo tu kukamilisha miswada inayoenda Bungeni ingawaje kwa wabunge makini wao ndio ilikua kazi yao ya kutunga hizo sheria..sheria nyingi zimepitishwa na kusainiwa huku wabunge hawajui kitu baadae wananchi wakipiga kelele zinabadilishwa tena kama kiwango cha makato ya kodi kwenye Mpesa.
 
Lakini unawezaje kupima ujinga wa mtu kwa kutumia kiwango cha usomi? Kati ya mwenye shahada ya uchumi na mwenye shahada ya kiswahili ni nani kati ya hao mwenye elimu kuliko mwingine!?
Allen unawezaje kuweka fani tofauti na kutaka kufananisha mkuu..
 
Elimu ya mtu inaweza isikupe uhakika wa kiwango ya akili, ila inakupa mtu aliyewekeza kwenye kujiongezea maarifa. Inawezekana pia kuna mtu hakwenda shule sio kwa kuwa hana akili, ila ni mazingira tu magumu
 
Rais anasaini sheria au Rais husaini Muswada wa sheria?
Sheria. Kwake unakuwa ni mswada kwa kuwa yale huwa ni mapendekezo ya bunge kwake.

Hii ni katika ile ya kuweka msawaziko wa kiutendaji (Checks and balances) kati ya mihimili ya serikali.

Ili utungaji wa Sheria mchakato wake ukamilike ni lazima Rais asaini mapendekezo ya bunge (mswada) kwa kuwa tawi la utawala (Executive) ndilo husimamia Sheria.

Kwa pembeni huwepo mhimili wa mahakama ambao kazi yake ni kuzitafsiri Sheria na wakati mwingine kuzibadilisha au kuzibatilisha!
 
Allen unawezaje kuweka fani tofauti na kutaka kufananisha mkuu..
Nimefanya makusudi. Maana kama kusoma ndiyo kigezo cha kuwa mbunge Bora, basi pia tujue kusoma kupi ndiyo usomi.

Maana anaweza kuchaguliwa nguli wa fizikia akachemka, watu wakasema bora tungechagua nguli wa Jiografia.

Kwa ivo tukubaliane ni usomi upi utatupa wabunge Bora! Lakini kitaalamu Elimu (Literacy) ni nini? Kamusi zote za kiingereza zinasema Literacy ni uwezo wa mtu kujua kusoma na kuandika. Mjadala upo wazi.
 
Elimu bora ni msingi wa vitu vingi sana mimi huwa nafatilia pia Bunge la SA ukimsikiliza Waziri wao wa fedha au Mwanasheria wa Serikali unaridhika kwa kinachojadiliwa hata yule Malema aliambiwa ili awe na hoja Bungeni aende shule na alifanya hivyo ila kama unaamini shule sio kigezo cha maendeleo endelea kuamini hivyo mkuu..
 
Kuna mahali nimesema shule siyo msingi wa maendeleo? Shule ni nini? Maana neno shule tumelitohoa toka kwenye lugha ya kijerumani "Schule" Sasa shule ni nini?

Hakuna jamii itakayoendelea bila ya watu wake kujielimisha. Lakini jadili hoja hii kwa muktadha wa kutafuta wabunge wetu kuwa dhaifu na si kuijumlisha jamii nzima ya kitanzania kwenye mjadala huu.
 
Back
Top Bottom