Bunge halitungi Sheria

Bunge halitungi Sheria

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
280
Reaction score
173
Kama nitakua nimekosea mtanielewesha, maana ninachofahamu mimi ni kwamba; Bunge linapelekewa Mswada wa sheria, kisha wabunge wanajadili na baadae kupitisha Mswada ili ukasainiwe na Rais, na sio kwamba Bunge ndio linauandaa huo Mswada wa sheria.

Kwa sababu huwa naona Mswada hupelekwa Bungeni, aidha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mawaziri wa Wizara husika.

Kwa maana hiyo; kwanini huwa tunasema Bunge linatunga sheria? Wakati kazi yake ni kujadili tu na kufanya marekebisho madogo, ambayo hata hayo marekebisho haliyafanyi Bunge, bali hupendekeza tu yafanyike?

Kwanini sasa tusitumie maneno; BUNGE HUPITISHA MSWADA WA SHERIA, BADALA YA BUNGE HUTUNGA SHERIA?
 
Nazani ume jielekeza vibaya Hata bunge lina tunga sheria ,kuna miswada inayo pelekwa na Serikali na kuna miswada ya mtu binafsi inayo pelekwa bungeni kupitia Mbunge na kazi inabaki kwa parliamentary draftsman aki shirikiana na ofisi ya AG ku draft , inshort ni somo refu .

Conclusion , Bunge lina tunga sheria
 
Upo sahihi, hata kwa akili ya kawaida, watu wanaojua kusoma na kuandika tu kama msukuma na yule kenge mwenzetu wanawezaje kutunga sheria ambazo hutumika katika mahakama zetu na watu professional kama mahakimu, mawakili nk.

Bunge ni muhuri tu wa kuidhinisha sheria kandamizi zinazowakweza watawala na kuwamaskinisha watawaliwa.
 
Tofautisha kati ya Bunge kutunga sheria, na wabunge wetu kutotunga sheria.

Bunge lina hiyo nguvu ya kupitia, kufanya mabadiliko na kupitisha muswada. Tatizo tulilonalo, ni wabunge wetu kuwa mateka wa serikali
 
Nazani ume jielekeza vibaya Hata bunge lina tunga sheria ,kuna miswada inayo pelekwa na Serikali na kuna miswada ya mtu binafsi inayo pelekwa bungeni kupitia Mbunge na kazi inabaki kwa parliamentary draftsman aki shirikiana na ofisi ya AG ku draft , inshort ni somo refu .

Conclusion , Bunge lina tunga sheria
Sasa Rais atasainije muswada ambao unalenga kumwajibisha yeye mwenyewe kisheria!! Buge halitungi sheria, linatumika tu na kutupiliwa mbali.
 
Mswada hauwi Sheria mpaka ujadiliwe, upitishe na usainiwe na Bunge.

Bunge linauwezo wa kuondoa au kuongeza kifungu au vifungu kwenye huo mswada.
Na lina uwezo wa kuukataa kabisa huo mswada.
 
Point of correction.
Mswada unakua sheria baada ya kusainiwa na Rais na sio Bunge.
Ninachouliza mimi sasa; huo Mswada wa sheria unaandaliwa na Bunge?
 
Nazani ume jielekeza vibaya Hata bunge lina tunga sheria ,kuna miswada inayo pelekwa na Serikali na kuna miswada ya mtu binafsi inayo pelekwa bungeni kupitia Mbunge na kazi inabaki kwa parliamentary draftsman aki shirikiana na ofisi ya AG ku draft , inshort ni somo refu .

Conclusion , Bunge lina tunga sheria
Nimekupata, na kama ndio hivyo, basi Miswada inayopelekwa na wabunge ni michache sana kulinganisha na inayopelekwa na Serikali. Kwa sababu mara nyingi inapotokea kuna sheria inaonekana kupitwa na wakati au vinginevyo, huwa nasikia wabunge wakiiomba Serikali ilete Muswada wa mabadiliko ya sheria hiya ili ijadiliwe na waipitishe, kwa nini wao wenyewe wasipeleke mpaka wanaitaka serikali ifanye hivyo?
 
Tofautisha kati ya Bunge kutunga sheria, na wabunge wetu kutotunga sheria.

Bunge lina hiyo nguvu ya kupitia, kufanya mabadiliko na kupitisha muswada. Tatizo tulilonalo, ni wabunge wetu kuwa mateka wa serikali
Sasa kuna Bunge bila wabunge mkuu?
 
Nazani ume jielekeza vibaya Hata bunge lina tunga sheria ,kuna miswada inayo pelekwa na Serikali na kuna miswada ya mtu binafsi inayo pelekwa bungeni kupitia Mbunge na kazi inabaki kwa parliamentary draftsman aki shirikiana na ofisi ya AG ku draft , inshort ni somo refu .

Conclusion , Bunge lina tunga sheria
Miswada binafsi ni nadharia tu. In practice inapogwa chini. Kinadharia bunge linatunga sheria. Lakini in practice ni serikali
 
Sasa Rais atasainije muswada ambao unalenga kumwajibisha yeye mwenyewe kisheria!! Buge halitungi sheria, linatumika tu na kutupiliwa mbali.
Ndio maana tuna taka katiba mpya , pia Unajua kama mahakama ina nguvu za kukataa sheria ilio pitishwa bungeni na kusainiwa na Rais na kuli elekeza bunge lifanyie marekebisho sheria iyo .
 
Nimekupata, na kama ndio hivyo, basi Miswada inayopelekwa na wabunge ni michache sana kulinganisha na inayopelekwa na Serikali. Kwa sababu mara nyingi inapotokea kuna sheria inaonekana kupitwa na wakati au vinginevyo, huwa nasikia wabunge wakiiomba Serikali ilete Muswada wa mabadiliko ya sheria hiya ili ijadiliwe na waipitishe, kwa nini wao wenyewe wasipeleke mpaka wanaitaka serikali ifanye hivyo?
Kuna aina nyingi za sheria mala nyingi izo ni huwa ambazo zipo na zili letwa na serikali kupitia wizara husika ivyo wabunge wanakua wanaomba serikali ilete marekebisho wayapitie zinaitwa ammendment bill .
 
Kwa sababu Wabunge vilaza ,darasa la 7 anajua nini kuhusu sheria ?
Miswada binafsi ni nadharia tu. In practice inapogwa chini. Kinadharia bunge linatunga sheria. Lakini in practice ni serikali
 
Sasa kuna Bunge bila wabunge mkuu?
Ndio maana nikasema Bunge linatunga sheria, tatizo letu tuna wabunge wa hovyo ambao hawatimizi majukumu yao... I mean, kama usipotumia kisu kama kinavyotakiwa, kosa ni lako tena, sio la kisu.

Binafsi naamini tuna tatizo la watu kuliko hata mifumo... Bunge letu lina mpaka nguvu za kumtoa Rais!
 
Point of correction.
Mswada unakua sheria baada ya kusainiwa na Rais na sio Bunge.
Ninachouliza mimi sasa; huo Mswada wa sheria unaandaliwa na Bunge?
Ndio una andaliwa na bunge kupitia ofisi ya Mwandishi wa Sheria wa Bunge,Serikali ina peleka mapendekezo ila anae draft ni ofisi za bunge then ndio una pelekwa bungeni uka jadiliwe na wabunge wana uwezo wa kuukataa mswada huo .
 
Kama nitakua nimekosea mtanielewesha, maana ninachofahamu mimi ni kwamba; Bunge linapelekewa Mswada wa sheria, kisha wabunge wanajadili na baadae kupitisha Mswada ili ukasainiwe na Rais, na sio kwamba Bunge ndio linauandaa huo Mswada wa sheria.

Kwa sababu huwa naona Mswada hupelekwa Bungeni, aidha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mawaziri wa Wizara husika.

Kwa maana hiyo; kwanini huwa tunasema Bunge linatunga sheria? Wakati kazi yake ni kujadili tu na kufanya marekebisho madogo, ambayo hata hayo marekebisho haliyafanyi Bunge, bali hupendekeza tu yafanyike?

Kwanini sasa tusitumie maneno; BUNGE HUPITISHA MSWADA WA SHERIA, BADALA YA BUNGE HUTUNGA SHERIA?
LInatunga sheria ndio kazi yake kuu na raisi anapelekewa kuzipitisha ili zianze kutumika rasmi kama akiridhika nazo
 
Kuna aina nyingi za sheria mala nyingi izo ni huwa ambazo zipo na zili letwa na serikali kupitia wizara husika ivyo wabunge wanakua wanaomba serikali ilete marekebisho wayapitie zinaitwa ammendment bill .
Bunge lenyewe haliwezi kuyafanya hayo marekebisho?
 
Ndio maana nikasema Bunge linatunga sheria, tatizo letu tuna wabunge wa hovyo ambao hawatimizi majukumu yao... I mean, kama usipotumia kisu kama kinavyotakiwa, kosa ni lako tena, sio la kisu.

Binafsi naamini tuna tatizo la watu kuliko hata mifumo... Bunge letu lina mpaka nguvu za kumtoa Rais!
Tatizo linabaki palepale kwenye mfumo, maana mfumo ndio unaotuletea hao wabunge ambao sifa ni kujua kusoma na kuandika tu
 
Ndio una andaliwa na bunge kupitia ofisi ya Mwandishi wa Sheria wa Bunge,Serikali ina peleka mapendekezo ila anae draft ni ofisi za bunge then ndio una pelekwa bungeni uka jadiliwe na wabunge wana uwezo wa kuukataa mswada huo .
Sawasawa
 
Back
Top Bottom