Mbunge Salome Makamba ametaka serikali kuwalinda wateja wa simu za mkononi ambao wanabanwa na mikataba isiyo ya usawa, kuwalazimisha kutumia salio za vifurishi huku walaji hao wakiwa hawana mtetezi wa kuuliza makampuni ya simu dhima na sababu ya kulazimisha walaji kutumia vifurushi vilivyosalia .
Mbunge huyo amesema suala la kulazimisha wateja kumalizia salio halipo ktk nchi zingine zilizoendelea na kutaka TCRA / Ombudsman yaani ofisi ya kushugulikia malalamiko ya wateja wa simu za mkononi Tanzania kuwanusuru na adha hiyo ya kuburuzwa kwa kisingizio mkataba unawabana walioingia wakati wateja hawana nguvu kupingana na makampuni hayo makubwa ya simu.
... ukitaka lisi-expaye hiyo option mbona ipo? Nenda na utaratibu wa muda wa maongezi badala ya bundle. Unapewa offer halafu unampangia masharti mtoaji!
Watajibu pale ambapo na wenyewe wataona madhara, kama mtu ana mshahara wa milioni 5, anaweza kuiba mali ya umma bila kushtukiwa, mabilioni na mabilioni, kwa nn aongee. Hana sababu ya kuongea. Ni mwanafalsafa tu ndo anaweza kua true kwenye haya mambo. Ila viongozi wote ni wafanya biashara