Bundi CHADEMA kapewa kigoda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bundi CHADEMA kapewa kigoda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jun 29, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hayumkini ni nadra sana kwa mtu mwenye akili timamu ukiambiwa hatari inakuja huwezi kuwa kama tomaso ambaye mpaka aliposhika ndo akasadiki hakika huyo alikuwa Masihi.

  Taifa la leo hatuhitaji waleta mabadiliko matomaso wanaosubiri kushika ndio wasadiki kwa kile walichokiona, CDM bundi anaunguruma kwa kasi sana, unafiki na kukosekana kwa mipango, umaarufu binafsi na uzandiki vinakitafuna chama.

  Mgongano wa misimamo katika agenda za Chama na kukosa mwelekeo katika masuala ya kiutendaji yanatulazimisha kupaza sauti zetu na kufungua jicho la tatu kutazama kwa kina ni nini kinatayarishwa hapa na wapi tunakwenda.

  Kuruhusu mamluki kubeba bendera kusaka ridhaa ya watanzania kwa kisingizio ati wamegundua kutokuwa na mfumo wa utawala mzuri walipotoka athari zake sasa zinaonekana.

  Tuliyatilia mashaka haya muda mrefu bado matomaso wakafumba macho na kushabikia upepo sasa kwa hali tuliyopo tunahitaji kuthubutu kusema Bundi lazima aondoshwe kwa namna yoyote CDM.


  Kuna haja ya kujipanga upya, kauli za hamaki na maazimio ya kukurupuka bila kutathimini athari zake yanazidi kukiweka chama njia panda.

  Ujira wa Mwia ni mfano mzuri, huyu alikuwa wapi kama keli kilifanyika kikao cha chama kujadili haya. Tunakwenda kule kule kwa chama dola kusutana kila siku katika vyombo vya habari kama wanapeana mipasho ya Taarab.

  Atakayeendelea kushabikia ujinga nafasi na muda ni wake lakini hapa tunapaza sauti kwa mapenzi mema kabisa kwa mustakbali wa watoto na wajukuu wetu, hatuchangi mawazo katika forum kama kijiwe cha kahawa tunajaribu kutafuta mustakabli mzuri wa Tanzania yetu ya baadeye.

  Come on guys! wake up, kuna tatizo hapa limefichika linahitaji kushighulikiwa haraka chama kimepoteza stability.
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  yeah,,true its a problem. nadhani wenyewe wanaliona na kulichukulia kwa umakini mkubwa. lets wait and see!
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Title ya thread yako ni nzito ukilinganisha na content. Ki msingi umeilaumu Chadema kutokana na matendo ya Shibuda. Hapo umekosea sana, umekurupuka. Tafakari yafuatayo
  1. Chadema ni taasisi iliyokaa kimfumo. Ukileta upuuzi kwenye taasisi iliyokaa kimfumo mfumo utaku-phase out automatically
  2. Kama chama kilichojijenga ambacho msingi wake ni watu watu kama Shibuda hukijenga chama na hakika hakitasambaratika
  3. Dhamira, malengo na nia binafsi walizonazo viongozi na wanachama wa chadema haviwezi kukiteteresha chama
  4. Kadiri CCM wanavyo perform poorly na chadema kubainisha mapungufu hayo kisayansi ndivyo credibility ya chadema inavyopaa
  5. Ipo project inayofadhiliwa kwa nguvu zote na CCM ya kuhakikisha Chadema inakufa lakini kutokana na sababu ya 1 hapo juu yote hayo yamebainika na chama linasogea.
  Yapo mapungufu katika kuipresent hoja ya posho na nadhani chadema hawakujipanga kama chama toka mwanzo na kwenye hilo wameteleza kidogo lakini huwezi ku conclude eti bundi amepewa kigoda(amekaribishwa) chamani.
   
 4. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Na mashaka kama wanalitazama hili kwa tahadhari mkuu maana bado hata kauli za leo za viongozi zinatatanisha hapa ni pa kujipanga na si matamko ya hamaki.
   
 5. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Thats all about art...unadhani bila hiyo heading ungefungua kusoma hapo ndipo tofauti yangu na wewe...Taaluma zinapishana.

  Turejee katika hoja, soma kwa umakini hiyo thread... maelezo yaliyopo hapo yana ujembe mzito wa mtu anayesoma kwa kutafakari na jicho la tatu na wala si husky reader.

  Hata hivyo finally umetoa mawazo mkuu...Tunathubutu kusema bila uoga, suala la Taasisi sitaki kulisikia, maana mie si wa kuhubiriwa uimara wa CDM nataka tusafishe uozo huu uliopo kwa sasa.
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kama lengo la kuweka title ya hivyo ili watu wafungue waisome basi na wewe umeteleza. Ume-water down fikra zangu juu yako kuhusu dhamira yako kwa chadema. Title yako imekaa kiudaku udaku.Nikukumbushe tu kuwa wewe sio wa kwanza kutaka kuuaminisha uma kuhusu huyo Bundi. Yaliandikwa, yakaandikwa lakini hadi sasa bundi hasikiki. Lakini hilo halimanishi kuwa chadema hakukuwa na migogoro au kupishana ki mtazamo. Hi huo utaasisi ambao unaupuuza sasa uliofanikisha chadema kuvuka vigingi vizito na vikali. Ni mwehu pekee anayeweza kuignore mfumo wa kiutawala na wa kitasisi wa chadema. Nikuhakikishie, chadema inamfumo mkali wa kiintelijensia ambapo threat yoyote kwa chama huwa detected haraka na hushughulikiwa accordingly. Mifano ipo na wengine wanafahamika.Lakini njia na taratibu zinazotumiwa na chdm kutatua migogoro ya ndani ni thabiti.Pamoja na hayo yote bado chadema inagroom vijana kitaasisi kuja kuwa viongozi madhubuti wa chama na taifa baadae.Hiyo ndio taasisi, na taasisi ya namna hiyo haifi! Mtaendelea kutoa dua la kuku kila siku. Hakuna bundi chadma
   
 7. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyu mkuu amejiunga JF 10/6/11 yaani siku 19 tu zilizopita, anapost 184 na amejishukuru mara 40 kwenye post 23!!

  Lakini kitu gani hasa kinamfanya huyu mkuu aweweseke namna hii? raia wa nchi hii wamefaidikaje na miaka 50 ya ccm madarakani?

  1. Umeme
  kwenye hii dunia ya karne ya 21 ya sayansi na technologia, vijiji vingapi vya nchi yetu vina umeme?

  2. Afya
  ni aibu kubwa hadi leo baadhi ya wake zetu kudhulika kwenye uzazi, matitizo kama ya Fistula (VVF) yalishasahauliwa kabisa kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea, actually ni mojawapo ya vipimo ya nchi fukara isiyoweza kuwapatia wananchi wake huduma za afya. Hapo hujaongezea na kipindupindu, surua, malaria, TB, utapia mlo nk magonjwa ya umasikini ambayo yanaendelea kushamiri tanzania miaka 50 ya kujitawala, Hospitali mbovu, chafu, zisizo na vifaa vya kisasa? madaktari uchwara kitaaluma (daktari aliyesoma Muhimbili ni daktari UPE, yaani ni kama wale walimu wa UPE wakati wa mwalimu)

  3. Elimu
  tujilinganishe na majirani zetu Kenya na Uganda. Sisi tuna elimu mdundiko

  4. Usafiri
  reli?, ndege?, barabara za lami? viwanja vya ndege? meli? usafiri wa mijini? ustaarabu wa kupanda vyombo haba vya usafiri yaani watu wazima kupigana vikombo wakati wa kuingia kwenye madaradara au mabasi? utumiaji wa magari mitumba na uchafuzi wa hewa mijini (air pollution)? wachache wanaweza kununua magari mapya? Mkuu naomba uwambie ccm waache mara moja kukiita kiwanja cha ndege mwanza International Airport, pamoja na kwamba watanzania ni mazezeta lakini uzezeta mwingine kama huu wa kukiita hiki kiwanja cha mwanza international airport unavuka mipaka.

  6. Maji
  Haa haaa haaa haaaa! pamoja na kuwepo mito, maziwa, bahari na mvua zinazo sababisha mafuriko, nchi haiwezi kutoa huduma ya maji bora hata kwenye makao makuu yake? Haa Haaa Haaaaaa Haa aha!!!!!!!! achilia mbali vijijini. rafiki yangu kijijini kwao ni pembeni mwa ziwa victoria, mwezi uliopita alitumia millioni 2 kuchimba kisima nyumbani kwao???? sasa anatafua solar ya umeme na pump ya maji, jamani ile kitu inayoitwa serkali iko wapi?

  5. Makazi ya watu
  unplanned, mitaa ya vumbi na matope isiyo na taa? Hakuna sewage system, kila mwenye kujenga nyumba anajenga septic tanks na kuishi na mavi yake mwenyewe uani kwake

  6. wafanyakazi wa serkalini
  wavivu? wana elimu duni, hawajui wanachofanya? hawalipwi mishahara inayokidhi mahitaji yao ya kimaisha? kila mfanyakazi wa serkali ni potential thief?

  7. viongozi wa ngazi za juu serkalini (raisi, mawaziri, makatibu wakuu nk)
  elimu duni (elimu ya tanzania), uwezo mdogo, hawajui walitendalo

  8. Maisha ya mwananchi wa kawaida kijijini
  Ni jehanamu, hakuna anayejali, ujanja ni kukimbilia mijini na kuwa machinga wenyewe wanasema "tutabanana humu humu"?

  Mkuu sababu gani hasa inakufanya uwachukie wale ambao wanajaribu kubadilisha hii hali angalau iwe nafuu kwa watu? Future ya nchi hii ipo namna hii:
  1. As long as ccm wako madarakani hali na maisha ya watanzania yatabakia ama kama yalivyo au kudidimia zaidi
  2. vyama vingine vikipata nafasi ya kuunda serkali vinaweza kurekebisha kasoro za ccm na kuinua maisha ya watu au vinaweza kuwa worse than ccm.

  Sasa hapa ndipo panapo hitaji maarifa yaani uogope kuchukua hatua na uendelee kudumaa na kudumaa zaidi au uchukue hatua ambayo inaweza kukuinua au kukuangamiza kabisa. The future belongs to the brave and those who dare to take risk. Hata kwenye biblia bwana Yesu alitoa mfano ya taranta, yule mtumishi aliyepewa taranta moja akaogopa kuitumia na kuishia kuifukia ili mkuu wake atakaporudi amkabidhi talanta ileile alilaaniwa kwa kufanya hivyo siku mkuu wake aliporudi, alinyanganywa taranta na akapewa yule ambaye alichukua risk ya kuzifanyia biashara talanta za mkuu na kutengeneza faida.
   
 8. Fungo N.

  Fungo N. JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umeeleweka mkuu no coment at all.
   
 9. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu umekwenda off the point, sihitaji hizo data nachojaribu kukifanya hapa tunahitaji CDM imara na si mafungu na ufa unajionyesha dhahiri hayo yote uliyoyaorodhesha hapo juu yatasimamiwa na nani kama CDM itabaki mapande.

  Jana Mwenyekti katangaza kufukuzwa kwa Shibuda, ina maana hatuna vikao wala suala la posho halikujadiliwa.

  Pili nikikukumbushe JF si Tanzania wala si CDM wala si Siasa, so kuiujnga mapema au kuchelewa hakupimi ufahamu na uelewa wa mambo simama katika hoja Mkuu
   
 10. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unazunguka nje ya Hoja ya msingi ambayo tunahitaji kuishughulikia, for your information CDM tumeisimaisha sisi (Sihitaji unihoji kivipi). hili linaloendelea sasa ni siasa chafu na litakidhoofisha chama. Tusimame imara kunusuru huyu Bundi na hatuwezi kuchoka kulisema hili mpaka kutabadilika
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kumbe unaleta hoja ya nguvu?! Endelea kulisema
   
 12. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena vyema. Hapo penye wekundu kama mtu hakubali kwamba ndio hali halisi ndani ya CHADEMA na kuifanyia kazi haraka basi huyo mtu haitakii mema CHADEMA. Minyukano yenye nia ovu ya kujenga umaarufu binafsi ni bundi anyeonekana mchana kweupeee ndani ya CHADEMA.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hii ndo hoja ya nguvu sasa, unaposema CDM mmeisimamisha nyie, maana yake unafahamu zaidi kuliko sisi wengine wote, Kiuhalisia unatuambia tusikubishie wala kuihoji dhamira wala maudhui ya hoja yako.

  Sasa mkuu, si uende kuwaeleza hao mlioisimamisha nao CDM ili kuishughulikia? (by the way, CDM ilishawahi kuwa down lini?) hapa utasema mimi sijui kwa sababu wewe unahusika sana?!!
   
 15. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unaweza kutafsiri unavyoweza Mkuu...Ila hoja yangu inaeleweka wala sihitaji wewe kuipima uzito wala wepesi maana sijui utatumia nyenzo gani. Na bahati mbaya huwa sijui malumbano napenda hoja.
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,073
  Likes Received: 6,536
  Trophy Points: 280
  Kila penye mafanikio maneno maneno hayatakosekana.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nakuunga mkono. Unajua kuna watu wanadhani CHADEMA ni chama chao. CHADEMA ni chama cha watanzania wote na ikichukua madaraka itaongoza wananchi wote wa Tanzania. Kwa hiyo watanzaia wote wana haki na wajibu wa kujadili mambo yanayoendelea nadani ya CHADEMA kwa kuwa CHADEMA kwa sasa ndio inaunda serikali mbadala ya CCM.

  Kuhusu mtu kijiunga JF hivi karibuni hiyo si hoja kwani JF kujiunga zamani ndio kunamfanya mtu awe na hoja za kuwasilisha hapa jamvini mbona kuna watu walijiunga wakati wa Jambo Forum lakini badala ya kuleta hoja wanaleta vioja.

  Amini usiamini Posho zitaivuruga CHADEMA kama hawataliangalia jambo hili kwa makini. Niliwahi kusema humu kwamba Posho inatugawa na kweli sasa imeonekana dhahiri kwamba posho imemgawa Shibuda na mimi kwa imani yangu ni kwamba shibuda hayuko peke yake. Ni vyema mambo yakajadiliwa kichama na siyo kuanza kupiga makelele kama CCM kuwa huyu tunamfukuza.
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  "Kutokana na tukio la jana (juzi) bungeni, Shibuda kutusaliti katika suala la posho za vikao, taratibu za kisheria zitafuata mkondo wake kwani utovu wa nidhamu haukubaliki katika kambi yetu, hata katika chama chetu,"alisema Mbowe na kuongeza:

  "Suala la posho si la mtu binafsi, lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chetu na kama kuna kiongozi hafahamu hili basi hakustahili kugombea ubunge kwa sababu naamini Ilani ya Uchaguzi, Shibuda anayo."

  "Posho zilijadiliwa na kupitishwa katika vikao maalumu vya chama, kwa hiyo kama Katiba yetu ya chama inavyotuongoza, Shibuda alitakiwa kulipinga katika vikao hivyo sio kutoka nje ya kikao na kuanza kupingana na maamuzi yake,"alisema Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.


  Akinukuu kifungu katika Katiba ya chama chake kinachoeleza maadili ya viongozi, Mbowe alisema, "Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye kanuni."
   
 19. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwenye hii mistari umeongea cha maana sana!
   
 20. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hawa ni kama watu ambao kwa jirani kuna sherehe wote wanahamia huko wakija kurudi kwao wameibiwa kila kitu, hawa ndo CCM wamejisahau na nini waliahidi kwa wananchi matokeo yake wao wamekalia kuitazama chadema watakaposhtuka hawana walilolifanya. mi nilitegememea humu wawe wanatushinda kwa hoja kama vile kuzungumzia mikakati ya kuboresha maisha ya wananchi. Yahani ufikiri na ufahamu wa CCM ndo kikomo chao wakiongozwa na handsome wao? Taifa la sasa halidanganyiki tena wandugu na jinsi mnavyochelewa kupambana na JF ndo tunavyozidi kujongea ikulu. Nasema 2015 no CCM again (chama cha magamba) they must go out no way they can remain.


   
Loading...