Huyu mkuu amejiunga JF 10/6/11 yaani siku 19 tu zilizopita, anapost 184 na amejishukuru mara 40 kwenye post 23!!
Lakini kitu gani hasa kinamfanya huyu mkuu aweweseke namna hii? raia wa nchi hii wamefaidikaje na miaka 50 ya ccm madarakani?
1. Umeme
kwenye hii dunia ya karne ya 21 ya sayansi na technologia, vijiji vingapi vya nchi yetu vina umeme?
2. Afya
ni aibu kubwa hadi leo baadhi ya wake zetu kudhulika kwenye uzazi, matitizo kama ya Fistula (VVF) yalishasahauliwa kabisa kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea, actually ni mojawapo ya vipimo ya nchi fukara isiyoweza kuwapatia wananchi wake huduma za afya. Hapo hujaongezea na kipindupindu, surua, malaria, TB, utapia mlo nk magonjwa ya umasikini ambayo yanaendelea kushamiri tanzania miaka 50 ya kujitawala, Hospitali mbovu, chafu, zisizo na vifaa vya kisasa? madaktari uchwara kitaaluma (daktari aliyesoma Muhimbili ni daktari UPE, yaani ni kama wale walimu wa UPE wakati wa mwalimu)
3. Elimu
tujilinganishe na majirani zetu Kenya na Uganda. Sisi tuna elimu mdundiko
4. Usafiri
reli?, ndege?, barabara za lami? viwanja vya ndege? meli? usafiri wa mijini? ustaarabu wa kupanda vyombo haba vya usafiri yaani watu wazima kupigana vikombo wakati wa kuingia kwenye madaradara au mabasi? utumiaji wa magari mitumba na uchafuzi wa hewa mijini (air pollution)? wachache wanaweza kununua magari mapya? Mkuu naomba uwambie ccm waache mara moja kukiita kiwanja cha ndege mwanza International Airport, pamoja na kwamba watanzania ni mazezeta lakini uzezeta mwingine kama huu wa kukiita hiki kiwanja cha mwanza international airport unavuka mipaka.
6. Maji
Haa haaa haaa haaaa! pamoja na kuwepo mito, maziwa, bahari na mvua zinazo sababisha mafuriko, nchi haiwezi kutoa huduma ya maji bora hata kwenye makao makuu yake? Haa Haaa Haaaaaa Haa aha!!!!!!!! achilia mbali vijijini. rafiki yangu kijijini kwao ni pembeni mwa ziwa victoria, mwezi uliopita alitumia millioni 2 kuchimba kisima nyumbani kwao???? sasa anatafua solar ya umeme na pump ya maji, jamani ile kitu inayoitwa serkali iko wapi?
5. Makazi ya watu
unplanned, mitaa ya vumbi na matope isiyo na taa? Hakuna sewage system, kila mwenye kujenga nyumba anajenga septic tanks na kuishi na mavi yake mwenyewe uani kwake
6. wafanyakazi wa serkalini
wavivu? wana elimu duni, hawajui wanachofanya? hawalipwi mishahara inayokidhi mahitaji yao ya kimaisha? kila mfanyakazi wa serkali ni potential thief?
7. viongozi wa ngazi za juu serkalini (raisi, mawaziri, makatibu wakuu nk)
elimu duni (elimu ya tanzania), uwezo mdogo, hawajui walitendalo
8. Maisha ya mwananchi wa kawaida kijijini
Ni jehanamu, hakuna anayejali, ujanja ni kukimbilia mijini na kuwa machinga wenyewe wanasema "tutabanana humu humu"?
Mkuu sababu gani hasa inakufanya uwachukie wale ambao wanajaribu kubadilisha hii hali angalau iwe nafuu kwa watu? Future ya nchi hii ipo namna hii:
1. As long as ccm wako madarakani hali na maisha ya watanzania yatabakia ama kama yalivyo au kudidimia zaidi
2. vyama vingine vikipata nafasi ya kuunda serkali vinaweza kurekebisha kasoro za ccm na kuinua maisha ya watu au vinaweza kuwa worse than ccm.
Sasa hapa ndipo panapo hitaji maarifa yaani uogope kuchukua hatua na uendelee kudumaa na kudumaa zaidi au uchukue hatua ambayo inaweza kukuinua au kukuangamiza kabisa. The future belongs to the brave and those who dare to take risk. Hata kwenye biblia bwana Yesu alitoa mfano ya taranta, yule mtumishi aliyepewa taranta moja akaogopa kuitumia na kuishia kuifukia ili mkuu wake atakaporudi amkabidhi talanta ileile alilaaniwa kwa kufanya hivyo siku mkuu wake aliporudi, alinyanganywa taranta na akapewa yule ambaye alichukua risk ya kuzifanyia biashara talanta za mkuu na kutengeneza faida.