Bundi CHADEMA kapewa kigoda

CDM ni chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo hawaezi kubabaika na hayo maneno demokrasia hamzuii mtu kuongea anachokiamini ndio maana kina sitta na mwakyembe wanapinga ufisadi waziwazi
 
Ni heri ya Ubundi wa Chadema kuliko unguruwe wa CCM, maana wametafuna mihogo yote, viazi vyote na wameuza kila kitu handsome hana cha kusema siku hizi kabisa. No way they can remain in 2015 they must go out to restart a fresh. Chadema is comited and hakuna njia yoyote unaweza kutudanganya na propaganda za kujivua magamba alihali no electricity, no water no madawati shuleni na unatuletea tabasamu kila siku lol tumekuchoka umeshazeeka. CCM sasa imezeekaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Hayumkini ni nadra sana kwa mtu mwenye akili timamu ukiambiwa hatari inakuja huwezi kuwa kama tomaso ambaye mpaka aliposhika ndo akasadiki hakika huyo alikuwa Masihi.

Taifa la leo hatuhitaji waleta mabadiliko matomaso wanaosubiri kushika ndio wasadiki kwa kile walichokiona, CDM bundi anaunguruma kwa kasi sana, unafiki na kukosekana kwa mipango, umaarufu binafsi na uzandiki vinakitafuna chama.

Mgongano wa misimamo katika agenda za Chama na kukosa mwelekeo katika masuala ya kiutendaji yanatulazimisha kupaza sauti zetu na kufungua jicho la tatu kutazama kwa kina ni nini kinatayarishwa hapa na wapi tunakwenda.

Kuruhusu mamluki kubeba bendera kusaka ridhaa ya watanzania kwa kisingizio ati wamegundua kutokuwa na mfumo wa utawala mzuri walipotoka athari zake sasa zinaonekana.

Tuliyatilia mashaka haya muda mrefu bado matomaso wakafumba macho na kushabikia upepo sasa kwa hali tuliyopo tunahitaji kuthubutu kusema Bundi lazima aondoshwe kwa namna yoyote CDM.

Kuna haja ya kujipanga upya, kauli za hamaki na maazimio ya kukurupuka bila kutathimini athari zake yanazidi kukiweka chama njia panda.

Ujira wa Mwia ni mfano mzuri, huyu alikuwa wapi kama keli kilifanyika kikao cha chama kujadili haya. Tunakwenda kule kule kwa chama dola kusutana kila siku katika vyombo vya habari kama wanapeana mipasho ya Taarab.

Atakayeendelea kushabikia ujinga nafasi na muda ni wake lakini hapa tunapaza sauti kwa mapenzi mema kabisa kwa mustakbali wa watoto na wajukuu wetu, hatuchangi mawazo katika forum kama kijiwe cha kahawa tunajaribu kutafuta mustakabli mzuri wa Tanzania yetu ya baadeye.

Come on guys! wake up, kuna tatizo hapa limefichika linahitaji kushighulikiwa haraka chama kimepoteza stability.
 
Mkuu mimi nakuunga mkono. Unajua kuna watu wanadhani CHADEMA ni chama chao. CHADEMA ni chama cha watanzania wote na ikichukua madaraka itaongoza wananchi wote wa Tanzania. Kwa hiyo watanzaia wote wana haki na wajibu wa kujadili mambo yanayoendelea nadani ya CHADEMA kwa kuwa CHADEMA kwa sasa ndio inaunda serikali mbadala ya CCM.

Kuhusu mtu kijiunga JF hivi karibuni hiyo si hoja kwani JF kujiunga zamani ndio kunamfanya mtu awe na hoja za kuwasilisha hapa jamvini mbona kuna watu walijiunga wakati wa Jambo Forum lakini badala ya kuleta hoja wanaleta vioja.

Amini usiamini Posho zitaivuruga CHADEMA kama hawataliangalia jambo hili kwa makini. Niliwahi kusema humu kwamba Posho inatugawa na kweli sasa imeonekana dhahiri kwamba posho imemgawa Shibuda na mimi kwa imani yangu ni kwamba shibuda hayuko peke yake. Ni vyema mambo yakajadiliwa kichama na siyo kuanza kupiga makelele kama CCM kuwa huyu tunamfukuza.

Mleta hoja niyo anataka kutuaminisha CDM ina watu wao.....yeye akiwemo kwasababu anasema amehusika kukisimamisha...na anasema tusimuulize kivipi.

Lakini mambo haya si mara ya kwanza kutokea, issue ya ZITTO ilisemwa sana na watu wakaenda mbali zaidi na kusema bwana ZITTO amepewa mlungula na mapacha watatu ili aidhoofishe CDM. yako wapi sasa?

My point is, kuna taratibi za kushughulikia mambo haya, viongozi wa kambi ya upinzani (Mbowe, Zitto na Lisu) wote wamesema vizuri sana kuhusu jambo hili - Gazeti la mwananchi amabalo mtoa hoja hapa kaanzishia thread tofauti.

Wasiwasi unatoka wapi? Kambi ya upinzani inatakiwa kumshughulikia kwanza, then wakiona kuna ulazima basi, Chama kitajulishwa na taratibu za kinidhamu zitafuata.
 
CDM ni chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo hawaezi kubabaika na hayo maneno demokrasia hamzuii mtu kuongea anachokiamini ndio maana kina sitta na mwakyembe wanapinga ufisadi waziwazi
What has bold red got to do with bold black??
 
Ni heri ya Ubundi wa Chadema kuliko unguruwe wa CCM, maana wametafuna mihogo yote, viazi vyote na wameuza kila kitu handsome hana cha kusema siku hizi kabisa. No way they can remain in 2015 they must go out to restart a fresh. Chadema is comited and hakuna njia yoyote unaweza kutudanganya na propaganda za kujivua magamba alihali no electricity, no water no madawati shuleni na unatuletea tabasamu kila siku lol tumekuchoka umeshazeeka. CCM sasa imezeekaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

You made me laugh Yutong
 
Mleta hoja niyo anataka kutuaminisha CDM ina watu wao.....yeye akiwemo kwasababu anasema amehusika kukisimamisha...na anasema tusimuulize kivipi.
Lakini mambo haya si mara ya kwanza kutokea, issue ya ZITTO ilisemwa sana na watu wakaenda mbali zaidi na kusema bwana ZITTO amepewa mlungula na mapacha watatu ili aidhoofishe CDM. yako wapi sasa?

My point is, kuna taratibi za kushughulikia mambo haya, viongozi wa kambi ya upinzani (Mbowe, Zitto na Lisu) wote wamesema vizuri sana kuhusu jambo hili - Gazeti la mwananchi amabalo mtoa hoja hapa kaanzishia thread tofauti.

Wasiwasi unatoka wapi? Kambi ya upinzani inatakiwa kumshughulikia kwanza, then wakiona kuna ulazima basi, Chama kitajulishwa na taratibu za kinidhamu zitafuata.

Mkuu usiwe na litle translation ya mambo hebu kunitendea haki Link statment hiyo na hoja iliyotangulia
 
Chadema mpka sasa unaona wamekufanyia nini? Angalia sehemu zote cdm wanazoongoza maendeleo yalivyo duni! mifano halisi unayo, angalia Karatu na Kigoma kulivyo na maendeleo duni!
 
Mimi nafahamu kwamba katika kundi la watu hamuwezi kukubaliana wote na kuna hii demokrasia ya wengi wape yote. Yaani wakiwa wengi hata kwa asilimia 50.1 basi wanachukua kila kitu. Wasiwasi wangu ni kwamba katika hilo la kupinga posho siamini kama Shibuda yuko peke yake. Pia tuliwahi kusoma kwenye Gazeti la Mwananchi kwamba kikao kilivunjika sasa maamuzi yalitoka wapi?
 
Kuna jambo hapa linahitaji mabadiliko tena ya kutulia hasa kwa kujipanga Mkuu na wala si kupiga makofi kwa kila jambo. hiyo kasumba ipo mtaa wa pili. Tumekubali kusimamia ukweli haimaanishi tuogope kusema hili sawa na hili hapana ati bwana mkubwa atachukia.

Hii forum ni msaada mkubwa na ndio eneo pekee sauti yetu ya NO itasikika. Tunahitaji mabadiliko hapa BRIGGITA kama umesoma comment hii ya KIMBUNGA na si kushabikia. Ushabiki hauna nafasi katika Modern Politics, hutufai hufai tu, umekosea hakuna salia Mtume tutakwambia urekebishe maana viongozi wanawakilisha utashi na matakwa yetu sio mitazmo yao.

Wakitaka mitazamo yao iwe mbele na matakwa yetu nyuma, watarudi huku katika vikao na masanduku ya Hiari.. tutawasaidia kujiuliza wapi walikosea.
 
Chadema mpka sasa unaona wamekufanyia nini? Angalia sehemu zote cdm wanazoongoza maendeleo yalivyo duni! mifano halisi unayo, angalia Karatu na Kigoma kulivyo na maendeleo duni!
Point of correction, CDM kazi yao sio kuleta maendeleo, wanachoweza fanya wao ni kusimamia na kuhoji kwa niaba ya wananchi. Serikali iliyopo madarakani na wananchi ndo wanaoleta hayo maendeleo. CDM hawana TRA ya kukusanya mabilioni kila mwezi, pesa ambazo wanaweza kuwa na nguvu nazo kwenye halmashauri perhaps ni kidogo mno ukilinganisha na mahitaji.
 
Title ya thread yako ni nzito ukilinganisha na content. Ki msingi umeilaumu Chadema kutokana na matendo ya Shibuda. Hapo umekosea sana, umekurupuka. Tafakari yafuatayo
1. Chadema ni taasisi iliyokaa kimfumo. Ukileta upuuzi kwenye taasisi iliyokaa kimfumo mfumo utaku-phase out automatically
2. Kama chama kilichojijenga ambacho msingi wake ni watu watu kama Shibuda hukijenga chama na hakika hakitasambaratika
3. Dhamira, malengo na nia binafsi walizonazo viongozi na wanachama wa chadema haviwezi kukiteteresha chama
4. Kadiri CCM wanavyo perform poorly na chadema kubainisha mapungufu hayo kisayansi ndivyo credibility ya chadema inavyopaa
5. Ipo project inayofadhiliwa kwa nguvu zote na CCM ya kuhakikisha Chadema inakufa lakini kutokana na sababu ya 1 hapo juu yote hayo yamebainika na chama linasogea.
Yapo mapungufu katika kuipresent hoja ya posho na nadhani chadema hawakujipanga kama chama toka mwanzo na kwenye hilo wameteleza kidogo lakini huwezi ku conclude eti bundi amepewa kigoda(amekaribishwa) chamani.

Tafadhali tuthibitishie hiyo project inaitwaje na Project Manager wake ni nani na Mkataba ulisainiwa lini.
 
Chadema mpka sasa unaona wamekufanyia nini? Angalia sehemu zote cdm wanazoongoza maendeleo yalivyo duni! mifano halisi unayo, angalia Karatu na Kigoma kulivyo na maendeleo duni!
Common sense ain't common
 
Ni heri ya Ubundi wa Chadema kuliko unguruwe wa CCM, maana wametafuna mihogo yote, viazi vyote na wameuza kila kitu handsome hana cha kusema siku hizi kabisa. No way they can remain in 2015 they must go out to restart a fresh. Chadema is comited and hakuna njia yoyote unaweza kutudanganya na propaganda za kujivua magamba alihali no electricity, no water no madawati shuleni na unatuletea tabasamu kila siku lol tumekuchoka umeshazeeka. CCM sasa imezeekaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Hiyo ya ku-go out ni ndoto za Alnacha, bado CCM itaendelea kukutawala hata ukiongea kwa jazba. na Rais wa Tanzania mwaka 2015 ni Edward N. Lowasa.
 
Kuna jambo hapa linahitaji mabadiliko tena ya kutulia hasa kwa kujipanga Mkuu na wala si kupiga makofi kwa kila jambo. hiyo kasumba ipo mtaa wa pili. Tumekubali kusimamia ukweli haimaanishi tuogope kusema hili sawa na hili hapana ati bwana mkubwa atachukia.

Hii forum ni msaada mkubwa na ndio eneo pekee sauti yetu ya NO itasikika. Tunahitaji mabadiliko hapa BRIGGITA kama umesoma comment hii ya KIMBUNGA na si kushabikia. Ushabiki hauna nafasi katika Modern Politics, hutufai hufai tu, umekosea hakuna salia Mtume tutakwambia urekebishe maana viongozi wanawakilisha utashi na matakwa yetu sio mitazmo yao.

Wakitaka mitazamo yao iwe mbele na matakwa yetu nyuma, watarudi huku katika vikao na masanduku ya Hiari.. tutawasaidia kujiuliza wapi walikosea.
Mkuu, mimi sishabikii chochote hapa, ninachosema ni kwamba, tusiwe wepesi wa kufanya conclusion kuwa pale pana moto kwasababu kuna moshi, labda wanafuta bange...just joking...anyway, Mkuu wewe unafahamu maswala ya nidhamu ndani ya chama hayashughulikiwi kwa kutoa taarifa kila siku kwenye vyombo vya habari, haya ni mambo nyeti, na wazee wa Magamba wanakuwa macho wazi na resources zipo ready for destruction.

Mimi binafsi napata shida kumuelewa Shibuda, hata alipokuwa CCM - nafikiri ni type ya wale watu wanaopenda kuonekana kwa ku-stand out just for the show.

Lakini pia, kwa sababu mimi binafsi sina taarifa za uhakika kuhusu vikao vilivyofanywa kuhusu posho (japokuwa, kuna kila sababu ya kuamini kilichosemwa na kambi ya upinzani bungeni...especially kwenye budget aliyoisoma Mh Zitto kuwa nsiyo msimamo - sio msimamo tu bali ni sera ya CDM) napenda nisiwe mteteaji wala mlalamikatji, na hasa mapema kiasi hiki.

Sikubaliani na baadhi ya watu wanaosema swala la posho halikupewa mkakati mzuri, sio kweli, swala la posho lipo kwenye ilani, na limeingizwa kwenye budget ya kambi rasmi ya upinzani bungeni. Swala la Mh. Zitto kujitokeza waziwazi hilo ni swala lake binafsi.
 
hapa anae bisha ubishi atakufa nao,nikweli Cdm tunapenda umaarufu wa mtu mmoja mmoja,hii ni mbaya bora tukae tuyajenge,kumfukuza bila kujua mianya mingine this is aproblem,tumfanyie intelegensia then tukishagundua anadhamira ipi ndo tufanye maamuzi,nikweli katiba ya Cdm inambana je yey mwenyewe mtizamo wake ni upi?nimegundua sisi utashi wetu ni wa watu nasio chama,eti kisa kasema nani basi sahihi je angesimama huyo shibuda akasema tunamsimamisha mayb zito au mbowe hizo hoja zingekuaje leo humu ndani.ok waliobun kuanzisha hiki chama naamini for first day hawafiki10 but now sio cha kwao ni cha watanzania wote wenye mapenzi na sera za cham,even M/kiti sio chake kawekwa na wananchi so leo anatokea mtu nakudai tumeanzisha au ni chama changu tunamshaa,kakaLa msingi tuzibe mianya yahao mabundi wanaojimojipenye...za
 
Mkuu mbona unatoka povu bila vituo mkuu!!!
Umemsikia Mh. Mbowei amesema nini? umemsikia Mh. Zitto amesema nn? Umemsikia Mh. Lisu amesema nini?

taratibu bana!!
 
Ukitaka kumjua binaadamu tabia yake halisi mpe vitu viwili ktk maisha yake
1-Mpe mali
2-Mpe Uongozi
Sidhani kama ni sahihi kukilaumu chama cha Chadema kwa kosa la mtu mmoja(Shibuda)kuwa tofauti na msimamo wa chama lkn kwa watakaotaka kuikosoa Chadema hawatakosa maneno ya kusema.Tusubiri kikao cha chama kitakuja na maamuzi gani.Mungu ibariki Tanzania wabariki na watu wake,pia pia kibariki Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema
 
Mkuu usiwe na litle translation ya mambo hebu kunitendea haki Link statment hiyo na hoja iliyotangulia
Hivi bado hujaligunduwa tu kosa lako? kama hujaligunduwa ngoja mimi nikueleze, kosa lako mkuu ni kuongea ukweli kwenye hii thread yako, maana wapo wanaoamini kwamba CHADEMA ni malaika hawawezi kufanya makosa.
Huyu Shibuda hapaswi kumaliza hili bunge la bajeti bungeni akiwa mbunge, avuliwe uanachama mara moja na jimbo liwe wazi watu waende kwenye uchaguzi mpya, ni unafki uliopitiliza kuwaambia CCM kwamba hawezi kufanya maamuzi magumu wakati nyinyi wenyewe mna mwehu mmoja tu kama Shibuda na mnashindwa kuchukuwa maamuzi mepesi kabisa?

Kwa hili sitawaelewa CHADEMA, nashukuru la Arusha chama jana kimetoa tamko lake la kutotambuwa muafaka na imeundwa tume ya kuchunguza, lakini laShibuda haliitaji tume ni kumfukuza arudi CCM, huyu sio mpiganaji yeye shida yake ilikuwa ni ubunge tu si kitu kingine.
 
Mkuu kuchukua hatua kwa taratibu za chama ni sahihi ila uoga wangu ni hapo anapojitokeza Mwenyekiti na Naibu Katibu Mkuu na kusema Shibuda ni Muasi na atafukuzwa. Si tusubiri vikao vikae vitoe tamko. Mimi bado naamini kuwa swala la posho ni bomu ambalo limetua CHADEMA na Shibuda hayupo peke yake hivyo ni vyema tukasubiri maamuzi ya Chama na si kauli za viongozi. Kiongozi mzuri anayejua uongozi akiulizwa swala kama hilo ni vizuri kusema tutalizungumza katika vikao vya Chama kwa kuwa Kiongozi hana madaraka ya kumfukuza mwanachama kama afanyavyo kwa mchungaji wa ng'ombe wake nyumbani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom