GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Hayumkini ni nadra sana kwa mtu mwenye akili timamu ukiambiwa hatari inakuja huwezi kuwa kama tomaso ambaye mpaka aliposhika ndo akasadiki hakika huyo alikuwa Masihi.
Taifa la leo hatuhitaji waleta mabadiliko matomaso wanaosubiri kushika ndio wasadiki kwa kile walichokiona, CDM bundi anaunguruma kwa kasi sana, unafiki na kukosekana kwa mipango, umaarufu binafsi na uzandiki vinakitafuna chama.
Mgongano wa misimamo katika agenda za Chama na kukosa mwelekeo katika masuala ya kiutendaji yanatulazimisha kupaza sauti zetu na kufungua jicho la tatu kutazama kwa kina ni nini kinatayarishwa hapa na wapi tunakwenda.
Kuruhusu mamluki kubeba bendera kusaka ridhaa ya watanzania kwa kisingizio ati wamegundua kutokuwa na mfumo wa utawala mzuri walipotoka athari zake sasa zinaonekana.
Tuliyatilia mashaka haya muda mrefu bado matomaso wakafumba macho na kushabikia upepo sasa kwa hali tuliyopo tunahitaji kuthubutu kusema Bundi lazima aondoshwe kwa namna yoyote CDM.
Kuna haja ya kujipanga upya, kauli za hamaki na maazimio ya kukurupuka bila kutathimini athari zake yanazidi kukiweka chama njia panda.
Ujira wa Mwia ni mfano mzuri, huyu alikuwa wapi kama keli kilifanyika kikao cha chama kujadili haya. Tunakwenda kule kule kwa chama dola kusutana kila siku katika vyombo vya habari kama wanapeana mipasho ya Taarab.
Atakayeendelea kushabikia ujinga nafasi na muda ni wake lakini hapa tunapaza sauti kwa mapenzi mema kabisa kwa mustakbali wa watoto na wajukuu wetu, hatuchangi mawazo katika forum kama kijiwe cha kahawa tunajaribu kutafuta mustakabli mzuri wa Tanzania yetu ya baadeye.
Come on guys! wake up, kuna tatizo hapa limefichika linahitaji kushighulikiwa haraka chama kimepoteza stability.