Bulgur Wheat Syndrome! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bulgur Wheat Syndrome!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by mayenga, May 9, 2011.

 1. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,751
  Likes Received: 547
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nazungumza na mzee mmoja, ambaye ni mtu mwenye heshima yake katika jamii na anao umarufu wa haja. Mada yetu ilikuwa ni kuhusu maendeleo ya taifa hili na fikra za watanzania hasa viongozi wa wakati huo.

  Mzee huyo ambaye katika kipindi hicho cha uhuru alikuwa shuleni anaeleza mwamko na uelewa mkubwa wa watanzania waliokuwa nao. Matokeo ya fikra pevu za Viongozi wetu zilimfanya Rais wa Marekani kipindi hicho Reagan kuitembelea Tanzania.

  Baada ya Rais huyo kutoa sifa lukuki kwa nchi hii,alitoa misaada mingi ikiwemo chakula mashuleni jeshini na taasisi nyinginezo ukiwamo unga maarufu ujulikanao kama Bulgur Wheat. Inasemekana unga huo ilikuja kujulikana kuwa unga ulikuwa na sumu iliyokuwa ikiharibu polepole akili za watanzania hasa uwezo wa kukumbuka na uwezo wa kutoa maamuzi.

  Mzee huyu anahitimisha kwa kusema kuwa,vijana wengi waliokula unga huo ndo kwa sasa ndio wanashikilia madaraka, wakiwemo mawaziri, marais, wabunge, majaji, nk na kwa jinsi hiyo ndo maana viongozi wetu wa sasa wamekuwa ni watu wasiokuwa wapembuzi. Wamebaki watu wa kutii kila waambiacho na pengine ubunifu kimekuwa ni kikwazo.

  Jamani mimi ni kijana wa 1980 je, mliokuwepo kipindi hicho haya yana ukweli?
   
 2. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwa kumbukumbu zilizopo, Rais Reagan hakuwahi kuitembelea Tanzania. Marais wa Marekani waliowahi kutembelea Tanzania ni Jimmy Carter, Bill Clinton na George Walker Bush Jnr.

  Kumbukumbu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 1980-1985, kulikuwa na matatizo ya ukame uliosababisha upungufu wa chakula, na kukatokea balaa la njaa. Kwa hiyo, kilichotokea ni serikali iliomba msaada wa chakula kutoka Marekani. Serkali ya Marekani ilitoa msaada wa chakula aina ya Mahindi ya njano (ulijulikana kama Yanga), na unga wa njano (Yanga), na hizo unazoziita Bulgar Weat. Miaka hiyo mimi nilikuwa darasa la tatu (10-15 years), na nilikuwa na uelewa wa kutosha wa kilichotokea. Hayo mambo mengine ya kwamba chakula kile kiliweka dawa za kupumbaza akili, sijui.
   
 3. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160

  Nina wasiwasi sana na hiyo story. Labda ulimwelewa vibaya huyo mzee. Pia inawezekana kwa huyo mzee kuwa, pamoja na heshima aliyonayo kwenye jamii, bado atakuwa mpenda stori za vijiweni. Sikumbuki suala la Ronald Reagan kuja Bongo. Na isitoshe Reagan alikuwa rais nafikiri 1982-90, akiwa ametanguliwa na Carter na kufuatiwa na Bush senior.

  Na hili suala la watu kupewa chakula na kudai eti kilikuwa kina madhara fulani ni stori za vijiweni. Ndio stori kama hizo, utasikia cocacola inapunguza nguvu za kiume, Chanjo ya polio inaua uzazi, n.k.

  Labda tu nikuhakikishie kuwa Ukiondoa kwenye kuamini ushirikina, na kujifanya watu wa dini saaana, Watanzania hawana tofauti na watu wengine duniani. Kama ni ujinga ujinga hata kule marekani na canada upo mwingi. Kwa mtazamo wangu ni kuwa hatuendelei tu kwa sababu, hakijapatikani kikundi cha watu wachache wanaoweza kutawala/kutuongoza kwa umakini. Nchi inaweza ikawa na maendeleo hata kama kuna wajinga wajinga wengi, almradi tu nchi inaongozwa na watu wenye uwezo wa kweli wa kutawala na huku wakizingatia maslahi ya taifa badala ya binafsi. Ni watu wachache sana wanaohitajika kufanya mabadiliko.
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Cha kuchekesha ni kuwa hapa Tanzania wajinga wachache ndiyo wanafanya maamuzi kwa niaba ya werevu na wajinga wengine!!
   
 5. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hicho unachoita burgur,haukua unga bali ni ngano iliyokobolewa. Ilikuwa ikipikwa kwa mfano wa uji mzito ukitiwa na mafuta ya kupikia kidogo au maziwa. Shule nyingi hasa za misheni ulitumika. Ulisaidia sana kukuza akili za watoto. Mimi nilitumia ndio maana unaniona ni great thinker!
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo mkuu hoja kuwa unga ulikuwa unapumbaza siyo kweli au?
  Nimepapenda penye nyekundu, keep it up GT!!
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Bana TANMO si kweli... Tusifanye mistake ya kuwafanya wajinga wetu waonekane walikua na akili na kujali pia kabla hawajala unga huo, siamini kama wote waliwahi kula hata hivyo. Mi nafikiri imefika wakati Watanzania tuache kujiuliza maswali ambayo hayawezi badilisha hali ya nchi bali kuongeza maneno tu! Napenda saana kua unapopita mitaa mbali mbali ya jamvi la jamii forum unakuta watu wengi ni waelewa na uwakilishaji ni mzuri ila kinachonisikitisha ni kujificha... Tuende ngazi kwa ngazi, kwanza tuache kujificha hasa unapokua unasema la kweli na ni manufaa ya wananchi wote, then tuanze kuwakilisha matatizo ili tuweze kuyatatua kwa manufaa ya wanajamii.... Sorry naona kidogo nitakua nilienda off topic...
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sawa Mkuu. Hiyo 'bulgur' ilikuwa ni nafaka ya ngano, nakumbuka tulikuwa tunapikiwa shule za msingi miaka ya 60 hadi 70. Vilevile vile kulikuwa na unga wa njano pamoja na mafuta ya kupikia kwenye containers zenye alama ya kushikana mikono na maandishi USA. Nilikula sana hiyo bulgur na unga wa njano (yanga), na sidhani kwamba kwa sasa nina akili za kusahau.
   
 9. B

  Bobo Ashanti Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa kabisa mkuu na rais wa marekani enzi zile alikuwa ni marehemu JohnKennedy hali ilitufanya baadhi yetu tuseme il mikono ni wa Nyerere na wa Kennedy.Those good old days buddies.
   
 10. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Du! Sawa kabisa Mkuu. Tulisoma shule moja nini. Maana hata sisi tulikuwa tunafikiria hivyo hivyo. Unakumbuka kwenye sherehe za Muungano tulipewa vikombe vya plastic vina mboni ya Muungano? Nakumbuka changu kilikuwa cha kijani!
   
 11. c

  chetuntu R I P

  #11
  May 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unga wa njano (yellow corn), bulgur na hayo mafuta ya USA, kwanza ni very nutritious wameadd microntrient at a recommended RDA for emergency situation. Ni vyakula vya emergency kucover some nutritional deficiencies, kama utapiamlo, pellagra, beriberi ,anaemia. vitamain A,D,E wameadd kwenye mafuta. Tatizo linakuja kwa pregnant mothers wanaokula sana hizi food aids wanapita operation juu watoto wanakuwa wakubwa ku kilo.
   
 12. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Asante mayenga, naona huyo "Mzee" hakuwa mkweli au alisimuliwa tu juu ya Bulgar wheat. Ukweli ni huu ufuatao na naamini utaungwa mkono na wazee wengi waliokuwepo wakati huo kama mimi yaani miaka ya 1963 -65 wa Bulgar wheat. Bulgar wheat haukuwa unga bali ni ngano iliyokobolewa vema na kutunzwa kwenye mifuko iliyokuwa na nembo iliyokuwa imeandikwa kwa lugha za kiingereza na kiswahili zikisema "Chakula hiki kimetolewa kwa msaada wa watu wa United States kisiuzwe wala kubadilishwa" na "Food donated by the people of the United States not to be sold or exchanged" sambamba na hiyo bulgar wheat yaliletwa pia mafuta ya "Corn Oil" katika magaloni ya bati na unga wa njano uliobeba maandishi sawa na yaliyokuwa kwenye mifuko ya bulgar wheat. Chakula kile kilitolewa kama msaada na iliyokuwa serikali ya Rais Kenedy (aliyekuwa rafiki mkubwa wa hayati Baba wa Taifa) kwa niaba ya watu wa Marekani kusaidia chakula katika shule na wengi tuliokuwa Middle Schools na Secondary Schools wakati ule tulikula. Kwa kweli kilikuwa chakula kizuri kabisa ambacho kilikoma kuletwa muda mfupi baada ya uongozi kubadilika na Rais mwingine (Lyndon Johnson) kutwaa madaraka. Ni wakati huo huo walimu wa kujitolea toka Marekani walifurika wakifundisha nyanja mbalimbali. Mimi naamini kwa dhati kwamba chakula kile hakikuwa na madhara yoyote pamoja nakwamba hatukuwa na vifaa vya kisasa kama sasa vya kupima ubora wa vyakula kama TBS, ukweli ni kwamba wakati ule serikali ilikuwa serious na hakukuwepo rushwa na uchakachuaji kama wa leo ambapo pamoja na utaalamu na vifaa vyote vilivyopo iko hatari ya watu kulishwa sumu kutokana na utamaduni wa Kinigeria tulioukumbatia yaani wa utapeli, uchakachuaji na ulaji wa rushwa kubwa kubwa.
   
 13. T

  Tabby JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2016
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,894
  Likes Received: 5,521
  Trophy Points: 280
  Mkuu wanaoongea vibaya juu ya Bulgar ni kwa sababu hawafahamu ama wamekaririshwa tu. Ahsante kwa ufafanuzi mzuri.

  Ninaweza kupata wapi sasa bulgar ya shayiri? (Barley) kama unafahamu?
   
 14. Njopino

  Njopino JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2016
  Joined: Apr 8, 2014
  Messages: 210
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  Na hiyo ndio shida ya watanzania
   
 15. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2016
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,751
  Likes Received: 547
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante Sana kwa ufafanuzi
   
Loading...