Bulembo: Tutayapata majimbo upinzani Kigoma kwa gharama yoyote

Hata mchukue majimbo yote Tanzania..
Utawala huu hautofanya lolote la maana kwa Watanzania..
Umaskini ndio unazidi kuwa maradufu..
Na Mlaaniwe CCM.
 
hakuna namna kauli kama hizi zikakusanywa na kupelekwa kwa washirika wa upinzani wa nchi za nje ili wafanye utaratibu wa kuhakikisha uchaguzi hauingiliwi na polisi? maana tume ya uchaguzi ni polisi siku hizi kwa mujibu wa uchaguzi wa madiwani uliomalizika na hata kwa kiasi kikubwa uchaguzi wa 2015
 
Hilo ni neno tu la Kisiasa Kama Mbowe aliposema tutalinda kura zetu kwa gharama yoyote ile lakin Siku ya kupiga kura hata kukaa mita Mia Tano waliogopa
Wao wana wallet tu na nauli zenu, nyinyi Mna mabomu, AK-47, ndege za kivita, uchawi, umalaya, ushetani, ulitaka waende kweli muwaue kirahisi?
 
Ndio maana wengine tumeshauri bila Tume Huru au bila kubadili sheria za uchaguzi ni bora wapinzani wasishiriki katika chaguzi zote zijazo.

Hii kauli sio kauli nyepesi na ingekuwa ni katika nchi zinazooheshimu demokrasia na utawala wa sheria, huyu bwana angetakiwa kujiuzulu mara moja.
 
"Serikali ni ya Chama cha Mapinduzi, waliopo chini ya serikali wanaitumikia serikali na kutekeleza ilani yetu, kama kuna watendaji au mkurugenzi hafuati utekelezaji wa ilani tutawatoa, hatuwezi kukubari tuyakose majimbo haya, tunayataka kwa gharama yoyote ile," alisema Burembo.
Chanzo: Nipashe

Kama kigezo cha utekelezaji ilani ya CCM ndicho kinatumika kutathmini utendaji wa watumishi wa umma, basi serikali nzima: kuanzia Rais hadi M’kiti wa Kijiji, inapaswa itolewe!

Kwa ujumla, kwa logic hiyo, CCM inapaswa itolewe kabisa! Maana imeshindwa kuwafanya watendaji watekeleze ilani yake! Miaka 56 ya Uhuru, CCM haijafanikisha hata jambo moja kwa asimilia 100!

Bulembo, shukuru watanzania wengi ni mabozo na mazuzu! Hili tu, ndilo linaendelea kuiweka CCM madarakani.
 
Hilo ni neno tu la Kisiasa Kama Mbowe aliposema tutalinda kura zetu kwa gharama yoyote ile lakin Siku ya kupiga kura hata kukaa mita Mia Tano waliogopa
Chifu, nimekuuliza very honesty questions kule! Ebu jibu tafadhali; and majibu yako yata-determine if I will ever ask you again. Thanks in advance in bruv.
 
Hazina ya kwenu, bunduki za kwenu, mabomu ya kwenu lazima mtambe lakini nyie ni washamba kishenzi.
 
Hawa viongozi kuna haja ya kupatiwa kozi za public speaking. Mara nyingi hali ya hewa huchafua wao wenyewe kwa kauli zao.
 
Angekuwa mpinzani angekuwa yuko POLISI ili afafanue kauli ya gharama yoyote.Hakna haki hapa tz
 
Gharama yoyote ni kutupiga mapanga vichwani kama uchaguzi wa marudio uliopita - HATUTAKUBALI NG'OO
 
Kwa heri Zitto Kabwe!

2020 Kigoma imeahidi kumstaafisha Zitto Kabwe Siasa!
Sio Kigoma bali ni sisi CCM..nia tunayo nyenzo na uwezo..asiposusa atatimuliwa hata na return officers wetu..akamuone Tumbili tulivyomfanyia kule KG kusini
 
Back
Top Bottom