Bulembo: Tutayapata majimbo upinzani Kigoma kwa gharama yoyote

Wakati mwingine Shule nzuri sana...

Tatizo la huyu Jamaa ni Elimu..

Huyu jamaa alipaswa kuhojiwa na Mamlaka husika afafanue juu ya kauli zake...

Huu ndio Uchochezi sasa...

Ikitokea watu wakaumizwa au kupoteza maisha basi tunaye mtuhumiwa namba moja...
 
kifanyikacho 2020 ni kutangaza wanaccm tu,sasa hivi kuna kazi ya kutisha wakurugenzi ili wasiwatangaze washindi toka vyama vya upinzani,kwa hiyo kitakachofanyika utake usitake viti vyote vitaenda ccm la msingi hapa ni kujjiandaa tu kwa lolote
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakitakubali kuyakosa tena majimbo ya Mkoa wa Kigoma yanayoongozwa na upinzani, kwamba watayapata kwa gharama yoyote katika uchaguzi ujao

Bulembo ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Kigoma ametoa kauli hiyo wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa mkoa wa Kigoma wa kumchagua mwenyekiti wa mkoa huo, na kuwataka viongozi wa chama hicho mkoa wa Kigoma kuwafichua watendaji na wakurugenzi ambao hawafuati utekelezaji wa ilani ili watolewe.


"Serikali ni ya Chama cha Mapinduzi, waliopo chini ya serikali wanaitumikia serikali na kutekeleza ilani yetu, kama kuna watendaji au mkurugenzi hafuati utekelezaji wa ilani tutawatoa, hatuwezi kukubari tuyakose majimbo haya, tunayataka kwa gharama yoyote ile," alisema Burembo.


Mojawapo ya majimbo mkoani Kigoma yanayoongozwa na upinzani ni Jimbo la Kigoma mjini linaloshikiliwa na Chama cha ACT-Wazalendo, ambalo mbunge wake ni Zitto Kabwe.


Chanzo: Nipashe

Kwa taifa la wajinga kama hilo usishangae hayo kutokea yanawezekana
 
Back
Top Bottom