Wanadai mikopo imewaelemea
Ndugu Yohana Mbatizaji,
Wanataja mikopo kama sababu ya ugumu wa maisha kwao.
Nadhani ugumu wa kurejesha mikopo ni matokeo tu ya tatizo la msingi. Wanapaswa kushughulika na tatizo la msingi badala ya kuangalia matokeo ya tatizo.
Nionanvyo tatizo kwa Waalimu wetu ni utawala mbovu usio na nia ya kuboresha maslahi yao ili waweze kuendesha maisha yao kwa staha.
Kama maslahi yao yangeboreshwa, bila shaka Waalimu wetu wasingekabiliwa na jinamizi la mateso ya urejeshaji mikopo. Kwa hali hiyo, mikopo ingebaki kuwa ni fursa ya ziada kwao, hivyo ingekuwa na tija tofauti na hali ilivyo Sasa.
Jambo la kushangaza ni kwamba, ukweli huu Waalimu wetu wanaufahamu, lakini wao ndio wakati wa uchaguzi wanakuwa injini za kuhakikisha kuwa watawala wale wale ambao ndio chanzo cha matatizo yao, wanachaguliwa tena. Hata ikibidi HILA kufanyika, basi si ajabu Waalimu kutumika kufanikisha hila hizo.
Hili ni jambo la kusikitisha sana kwani, wenzetu hawa ktk kipindi cha uchaguzi hujisahau na kujiona wao ni sehemu ya watawala, hivyo huukana umma.
Lakini baada ya uchaguzi UKWELI HALISI huonekana kuwa kumbe hata wao wapo ktk tabaka la wananchi na sio watawala kama walivyojidanganya au walivyodanganywa.
Sasa ikifikia hapo huanza kulalamika kwani matokeo ya tatizo hujitokeza.
Nawashauri Waalimu wetu wapendwa, waache kushughulika na matokeo ya tatizo bali washughulikie tatizo.
Nawaheshimu sana Waalimu ila mmejiangusha WENYEWE..