Bulembo amtaka Lowassa awataje wanaoonewa kwenye kodi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
Msikilizeni huyu mzee live star tv muda huu.

Kaongea kama dakika tano tu na tunaambiwa katoa Tamko la Jumuiya ya Wazizi wa CCM. Binafsi sijamuona akisoma popote pale labda ni mswala ya teknolojia.

Bwana Bulembo anahoji Lowassa ni kama nani ndani ya CHADEMA mpaka atoe kauli ile ya kudai waliounga mkono CHADEMA wananyanyaswa na amemtaka aitishe mkutano na waandishi wa habari na awataje hao wafanyabiashara na ataje kama kuna kodi waliongozewa.

Bulembo aliongeza kuwa,Lowassa akitaka agombee tena 2020 na akasisitiza hata akigombea watamshinda kwa mara nyingine.

Bulembo, ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amesema wao hawawezi kukaa kimya kwa matamshi hayo ya mh.Lowassa.

Bulembo pia amekosoa kauli ya Makongoro Mahanga kuwa Magufuli hajapunguza ukubwa wa serikali bali ameongeza.

Chanzo:Star tv
 
Last edited:
sasa wewe ndio upo kwenye R/Luninga...badala ulete taarifa kamili ama details......unahemka na kupayuka
 
Ninachofurahia ni kwamba mh rais wangu lowassa amewashika pabaya, yaani akikohoa tu, haja zinagonga chupi
 
sasa wewe ndio upo kwenye R/Luninga...badala ulete taarifa kamili ama details......unahemka na kupayuka
Nlipoana ni live na huku tukiambiwa ni Tamko la Jumuiya ya Wazazi wa CCM, nikakaa kusikiliza lakini nilimuona akiongea kama mgeni aliekalibishawa studio tu na kaongea kwa muda mfupi ambao sidhani kama kweli umezidi dakika tano au 7 hivi.
 
Bulembo amehongwa ubunge kupitia mwanaye wa kike. Basi povu litamtoka mpk basi. Lowassa alisema "anasikia" imezuka tabia ya kuwanyanyasa waliounga mkono chadema. Akamalizia kwa kusema "kama" hiyo tabia ipo basi anaitaka serikali ya JPM iache mara moja.
 
Yeah, kwa akili za nyumbu ni kweli. Sasa hivi hakuna CHADEMA wala NCCR Mageuzi, ni Lowassa tu. Mtu mmoja yuko juu ya taasisi, only in Tanzania. Na huu ndio unaojiita upinzani!!!
 
Last edited by a moderator:
Mi nadhani Lowassa anapaswa kuyaishi maneno yake.

Kwamba,

Kama ana ushahidi aende mahakamani au a-Shut up.

Na huyo Bulembo nae bora akae kimya tu kuliko kuendelea kuwapa kick watafuta publicity.

I hate political football.
 
Yeah, kwa akili za nyumbu ni kweli. Sasa hivi hakuna CHADEMA wala NCCR Mageuzi, ni Lowassa tu. Mtu mmoja yuko juu ya taasisi, only in Tanzania. Na huu ndio unaojiita upinzani!!
daaah ina maana bado wewe unatukuza vyama siasa ya sasa sio chama ni mtu angalia nchi za watu eg america uk burundi rwanda uganda kenya wanampima mtu na sio chama nkurunzinza ,kagame mseveni obama havizungumzwi vyama ni watu so usishangae kuona jina lowasa linatawala
 
Ngonjera zilezile za kulalamika tumeibiwa kura ,ukiambiwa lete ushahidi hauleti,

Sasa akiambiwa awataje hao wanaoonewa kwa kodi ili sheria ichukue mkondo wake hataji


Sasa kama siyo jamii ya nyumbu ni nini
 
Back
Top Bottom