Arusha na Moshi zina mazingira tofauti kabisa na Bukoba au Kagera nzima. Kaskazini kuna mzunguko mkubwa wa fedha na vyanzo vingi vya mapato. Mlima Kilimanjaro unaleta mapato mengi, pale Arusha ni soko la madini, utalii mwingi unapita mikoa hiyo. Kagera mkoa una resources ambazo hazijaguswa ni kitendo cha kutokea sera za maana zilizosimama na viongozi sahihi miaka mitano tu mkoa unakuwa level za juu.
Nimeishi Moshi nikazuru Arusha, Arusha ni jiji ila tofauti ya Moshi na Bukoba kwa maendeleo ni ndogo wala hakuna widening of gap.
Kwanza hakuna umaskini kivile, tatizo ni ukosefu wa vyanzo vya mapato. Nimezaliwa Bukoba na kusoma uko O level sijawahi kuona tractor wala combine harvester, nimekuja kuyaona mikoa mingine. Sikuwahi ona mtaalamu wa kilimo wa serikali uko, sikuwahi ona pembejeo zinatolewa na serikali, ule mkoa ni semi autonomous ndio maana wana jeuri ya kutukana Rais kwenye kampeni maana hawamtegemei kwa lolote. Serikali au viongozi wakiamka wakaweka sera nzuri ambazo hata sio gharama kubwa utashuhudia kilimo cha kahawa kinakua haraka sana, vannila, parachichi, ndizi. Hivyo vyote wala serikali haihitajiki kutoa hela.
Mkoa unaishi kwa remittance kutoka mikoa mingine, sio kama Shinyanga wanaouza madini nje wakawa na hela za nje nje ukienda kuuza hata mitumba au viatu unapata wateja. Mtwara wakiuza korosho ukienda kuwauzia simu wananunua, Kagera mwaka mzima hauna msimu wa hela. Hawafi njaa ila hawana hela. Mipaka yenyewe ndio hiyo yenye migogoro, wakati Arusha wamepakana na Kenya yenye mahitaji tofauti na Tanzania, Kagera iko na Uganda ambao bidhaa zao na za Kagera ni zilezile. Utatoka Songea upite Arusha uuze mahindi Kenya, uliwahi sikia bidhaa yoyote ya msingi tunaiuza Uganda? Bidhaa za Uganda zina bei nafuu wakati hawana bandari, nguo zinanunuliwa China zinapita Mombasa zinaingia Uganda tunaenda zinunua Mutukula ya Uganda kwa bei nafuu kuliko zinazopita bandari ya DSM. Humu JF kuna nyuzi za biashara na Uganda, katafute kama kuna mjadala wa exportation, badala yake ni importation kutoka Uganda. Majirani wengine ni Rwanda na Burundi, tuna majirani wa hasara wao muda wowote wanatuletea wakimbizi, majambazi, wagonjwa wa Ebola, Zika virus na UKIMWI. All of them they don't have purchasing power.
Kagera ina disadvantages kuendelea ila inahitaji serious efforts kidogo. Kwanza umbali wenyewe tatizo, mtu utabeba mbao, ng'ombe, maziwa, mazao kutoka kule. Gharama za usafirishaji ni kubwa unatafuta alternative eneo la karibu, kule hakuna reli. Kama demand ni ndogo na uzalishaji ni mdogo