Bukoba sirudi tena ng'o


Hiyo inategemea na mtazamo wako ulikuwa unahitaji nini? Binadamu hatufanani,unaweza ukamtoa mtu hapo Bukoba na kumpeleka Dubai au Tokyo na asipapende! The Soul isn't where it lives but where it Loves.
 

Buoba hamna bahari....bali kuna ziwa Victoria....
 

SOKONI UMEFIKA; UMEKOSA NN

 

Kiongozi mi nilijua umezaliwa Tokyo na umekulia huko.....kumbe umetoka Mwanza???!!lol sasa tofauti ya Mwanza na Bukoba sio kubwa saaaana....bahati nzuri nilisoma Mwanza na niliwahi kuishi Bukoba na kufanya kazi pia kwa hiyo sidhani kama kuna ubaya huo ambao wewe unaisema....Bukoba mjini pako salama pengine kuliko miji yote hapa nchini,nilikaa miaka mitatu sijawawi kusikia ujambazi pale wala mlio wa risasi,ndizi za buku mnakula zaidi ya mashababi watatu kwa maana ya kwamba kama una chanzo cha mapato maisha yapo kawaida sana.
 

Mtoa mada kasema bukoba sio kagera, habari za ukerewe zinatoka wapi!!
 
bwanae mtu kwao wewe urudi usirudi kwani huko ni kwenu ? waache wenye kwao wewe angalia kwenu kunani.
Inawezekana wewe unatabia mbaya ya kudharau wenzako. una taabu sana wewe
Mimi sio mleta mada.

Nafikiri umeniquote kimakosa bila shaka jamaa amekufanya uchape kwa jazba matokeo yake badala ya kufikisha ujumbe kwa mlengwa ukanifikia mimi.

Ila hakuna tatizo ujumbe kaupata bila chenga.

Na kwa niaba yako nawasilisha
 
Ni kweli wahaya ni watu wanaoongoza miongoni mwa makabila yanayoongoza kwa watu wake kuwa na elimu ya juu na pia uwezo wa kiuchumi. Tatizo lao mimi naona wanawekeza zaidi nje yaani kwenye mikoa ya nje ya kwao kuliko kwao. Angali majumba ya kifahari yaliyopo Dsm na sehemu nyingine za nchi, angalia mashule yanayofanya vizuri, angalia mashirika mbali mbali ya binafsi nk. Wahaya ni matajiri lakini wamewekeza utajiri wao nje ya mkoa wao na wengi ni kama wamehama kabisa kwao ambapo huenda mara moja moja hasa wakati wa misiba tofauti na wachagga ambao wamewekeza kwao vizuri na hurudi kwao kila mwaka kufanya maendeleo ndio maana ukienda vijijini utakuta majumba ya nguvu kuliko hata yaliyopo mjini Dsm na kwingineko
 
We mi nimekaa Bk, miaka miwili, kwa kweli ni pazuri sana, kwanza hali yake ya hewa tu utapenda na maeneo ya kutembelea yapo ingawa si kivile ila kwa Mji kama Bk. ukilinganisha na mingine bado ni pazuri sana, mimi nilikuwa nakaa Kashai, National Housing, karibia na TEMESA, kwa kweli ni pazuri sijui wewe ulitegemea nini hasa mkuu?
 
Wacha tusema ukweli Bukoba ni kubaya tena ni kubayaaaaaaaa mbona wao huwa wanapondea kwa wenzao kazi misifa kwao hawapajengi ukweli ndo huo kama mumechukia kunyweni sumu.
 
Wacha tusema ukweli Bukoba ni kubaya tena ni kubayaaaaaaaa mbona wao huwa wanapondea kwa wenzao kazi misifa kwao hawapajengi ukweli ndo huo kama mumechukia kunyweni sumu.

Huna lolote chuki binafsi mbona husemi kwenu wapi
 

hahhahahah!! huko ukanakoita kwenu Mwanza kumefikia hatua hiyo shauri ya mchango wa wahaya au tuseme watu wa Kagera. Kaama alivyosema Tulimumu wahaya wamekuwa wawekezaji wakuu nje ya Bukoba si kwa majengo na biashara tu kama mtoa mada anavyolenga - kwa kiasi kikubwa hasa awamu ya kwanza imewatumikisha kitaluma bila kuwawezesha kuijenga Bukoba. Aidha wametumikishwa kwa uaminifu tofauti na makabila ambayo yalijikita katika kupora raslimali za nchi hii na kujenga kwao huku awamu ya kwanza ikiwakenulia meno.

hali ya vijijini ni nzuri - mfano uvunaji wa maji - huwezi kuta wahaya wanakunywa maji ya madimbwi wakishirikiana na mifugo kama wafanyavyo kwa mtoa hoja. kuna mifano mingi lakini hapa si mahala pake
 
Ndo maana wahaya wengi wana maji
 
Ni kweli mkuu, mleta uzi inaonyesha alishukia ile stendi ya vumbi pale akaibukia mitaa ya uswazini, basi akafikiri Bukoba yote iko hivyo.
 
Habari ya bukoba mkuu
 
Nenda hata ss hatukutak mkuu [emoji17] [emoji85]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…