Bujibuji na Mshana Jr, wanamtongoza mpenzi wangu Kichawi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Habari zenu wakuu,

Nimeingiwa na wasiwasi sana, nina mpenzi wangu nampenda sana, lakini hivi karibuni ameanza kubadilika.

Kila muda nikionana naye ananipa stori za mshana jr na Bujibuji, anadai amewafahamia JF. Anataka eti wamfundishe kujikinga na wachawi, hivyo anawatafuta. Kumbuka hajui kama mimi nipo JF, wala hajui kama najua wanavyoleta thread za kichawi.

Anadai eti anamtafuta Bujibuji ili ampe dawa ya kuona wachawi na kugundua nyoka wa Kichawi.

Mshana anataka ampe dawa na kujikinga na majini. Wiki mbili sasa akilala anaweweseka, anaota na kutamka maneno kwa Sauti. Kilichofanya niandike hapa, ni baada ya jana kuota na kusikia maneno akitamka kabisa BUJI, ikabidi nimuamshe, akasema nimemsikia vibaya alikua anaota akinywa Uji.

Mke wangu mwenyewe kila siku namuona kule MMU.

Naombeni msaada ili mpenzi wangu asichepuke kwani bado nampenda. Na hawa watu wanaomtongoza kwa dawa nawaogopa sana.
 
Ha ha ha. Waachie tu aisee kama unajipenda. Hawakawii kukugeuza inzi hao jamaa ukakosa vyote; Mruhusu tu kiroho safi akafundishwe vya kufundishwaa
 
Habari zenu wakuu,

Nimeingiwa na wasiwasi sana, nina mpenzi wangu nampenda sana, lakini hivi karibuni ameanza kubadilika.

Kila muda nikionana naye ananipa stori za mshana jr na Bujibuji, anadai amewafahamia JF. Anataka eti wamfundishe kujikinga na wachawi, hivyo anawatafuta. Kumbuka hajui kama mimi nipo JF, wala hajui kama najua wanavyoleta thread za kichawi.

Anadai eti anamtafuta Bujibuji ili ampe dawa ya kuona wachawi na kugundua nyoka wa Kichawi.

Mshana anataka ampe dawa na kujikinga na majini. Wiki mbili sasa akilala anaweweseka, anaota na kutamka maneno kwa Sauti. Kilichofanya niandike hapa, ni baada ya jana kuota na kusikia maneno akitamka kabisa BUJI, ikabidi nimuamshe, akasema nimemsikia vibaya alikua anaota akinywa Uji.

Mke wangu mwenyewe kila siku namuona kule MMU.

Naombeni msaada ili mpenzi wangu asichepuke kwani bado nampenda. Na hawa watu wanaomtongoza kwa dawa nawaogopa sana.
figganigga umenisababishia kwikwi za chembe ya moyo kwakuwa hapa nilipo nimecheka kwa kujibana lol
Mimi kamwe huwa sitongozi mteja wangu labda itokee tuu hasa kama ndo sharti la dawa yenyewe
Kinachonipa faraja lakini na mashaka pia hakuniota mimi bali Bujibuji
 
Back
Top Bottom