Buick na Cadillac

Buick na Cadillac

bullet

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Posts
1,047
Reaction score
545
Hivi kwa nini American Cars kama Buick au Cadillac hayapo sana Bongo? Ni kwamba producers hawana markting strategies kwenye nchi zetu? Au hakuna magari ya mtumba ya aina hiyo? Kama kwa magari ya kijapani.
Kwa nini hayapatikani nchini au kama yapo yapo kwa uchache sana?

Pili hizi Ford ninazoziona hata Tanzania zinatoka all the way US au zinazalishwa nchi ya pili kama South Africa?
 
Hata yangekuwepo nani angenunua magari yanayomeza mafuta lita moja kwa kilomita 5? Mabuick, macadillac, machevrolet waachieni haohao wamerikani.
 
American cars wao walitengeneza magari makubwa V8 na zilikuwa zinakunywa mafuta sana, na Soko lao lilikuwa kwao na uarabuni kwa sana.
Lakini ingawa wametengeneza siku hizi za 4 cylinders lakini bado Soko hamna.
Hazijulikani hata Ulaya soko lao halipo hivyo ni machache sana.

Africa magari ya kijapani ndio yameshika sana
 
Ndio maana hayapo Tanzania!?Mbona Ulaya na China yapo mengi?

Huko unakotaja bado huwezi kupalinganisha na Africa, wako mbali na spare zipo kwa wingi na rahisi, africa safari bado ndefu sana hatujawa bado kwenye target ya market yao
Hapo bora Cadillac kidogo, Buick ni spana mkononi hata kama umenunua zero mileage.
Ford is good
 
Back
Top Bottom