Buguruni: Sherehe yageuka msiba

Buguruni: Sherehe yageuka msiba

Kilichofanya niweke bandiko ni mambo mawili, kwanza kueleza tukio husika, pili kuna mleta mada anayejiita Grader kapost uongo kutokana na hiki ntakachoandika, amemsingizia huyo marehemu Panya road azikwa kifahari Buguruni kisiwani, pili amesema Buruguni ni kitongoji chenye kila aina ya laana! Kweli? Hivi mtu humjui hata jina, umri wake wala maisha yake unaazaje kumkashifu mtu.

Then unakashifu eneo husika unadai kuna kila aina ya ufedhuli na vijana wake wamepotoka, ina mana wakazi wa Buguruni wote hatuna maana? Au mwenzetu anaishi peponi?

Stori kamil ilikuaa hivi; Jumapili ya tarehe 31 mwezi Mei mtaani kulikuwa na sherehe, kuna binti anaitwa Zena alikuwa anaolewa, huyo Zena na marehemu walikuwa mtu na mjomba wake na ilipangwa tarehe 5 Ijumaa, marehemu arudi ili aje kufungishwa ndoa.

Hivi panya road anaweza kusubiriwa toka Sauzi aje bongo kufungisha ndoa? Tena anakuja kwa ndege? Bahati mbaya Jumatatu bongo wanamfanyia kitchen party Zena kule mjomba wake anapigwa risasi akiwa supermaket.

Baada ya kupewa ripoti Jumanne asubuhi walilia na sherehe ikawa basi!

Itaendelea part 2

=> Part 2
Kiukwel ilipangwa sherehe bab kubwa ifanyike pale mtaani. Sherehe ilipangwa ifanyike wiki nzima kuanzia tar 31 May had tar 7 June. Jumapili paliwekwa ngoma, Jumatatu usiku ikafanyika kitchen party lakini kwa bahati mbaya tulipokea taarifa zilizostua mioyo ya wengi pale tulipoambiwa kaka yao mkubwa anayeitwa Hamis ametutoka duniani.

Alifariki kwa kupigwa risasi akiwa supermarket nchin Afrika Kusini, taarifa ambayo ilizima chereko pale mtaani na kukatisha ratiba ya sherehe iliyosalia ambayo ilitakiwa Jumatano ipigwe baikoko, Alhamis upigwe mnanda, Ijumaa ipigwe taarab live band kutoka kwa mashauzi Classic na Jumamosi wamalizie na rusha roho kisha Jumapili waende ukumbini kwa ajili ya harusi lakini mambo hayakuwa hivyo sherehe yageuka msiba!! unajua chanzo cha marehemu kuuawa?

Ungana nami sehemu ya tatu.

Chanzo: Mimi ni jirani yao.

Nafikiri haujui unachokitetea, Mimi ni mzoefu sana kwa shughuli za uandishi wa habari za uchunguzi zaidi ya miaka 10 sasa, nilikuwa nisafiri kuelekea Dodoma siku ya jumatatu sijaenda kwani niliamua kubaki ili nikamilishe report hii ya kiuchunguzi. Ukweli unayejiita Dr Aluta huifahamu Buguruni na uhalifu unaofanywa(uvunjwaji wa sheria na maadili). Nimebahatika kufanya mahojiano ya ana kwa ana na ndugu,jamaa na rafiki wa Hamisi. Pia nimechunguza maeneo yote korofi na kufanya mahojiano ya kina na wahusika na kuridhika pasipo shaka Buguruni ni sehemu maarufu kwa uhalifu kama wizi,ujambazi,ukabaji,chabo,madawa ya kulevya,bangi,utumiaji na uuzaji wa pombe haramu,ukahaba,chuma ulete n.k. Mimi sijasimuliwa na mtu habari hiyo bali nimeifuatilia mpaka mwisho wake. Kwa kweli wanaokaa Buguruni chukueni tahadhali .
 
by Dr Aluta;
ninachotetea jamaa hakuwah kuwa panya road.

Dr Aluta, wewe umejuaje hakuwa panya road??

Au wewe ni mwanachama wa panya road!

cc suleyman kova.
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi fika buguruni kisiwani baa moja inaitwa hilton nikanywa nikala ikafika mida ya nne na nusu nkaondoka na car yangu mdogomdogo ile natoka kwenda mbele nikate kona kuingia main road pancha duuh……!
-sijakaa sawa machizi hawa hapa kumbe nami nipo fiti na mkanda wangu mweusi duuh tulimalizana kimyakimya wakanipa hadi walizo pora mitaa mingine#

hongera mkuu
 
Nafikiri haujui unachokitetea, Mimi ni mzoefu sana kwa shughuli za uandishi wa habari za uchunguzi zaidi ya miaka 10 sasa, nilikuwa nisafiri kuelekea Dodoma siku ya jumatatu sijaenda kwani niliamua kubaki ili nikamilishe report hii ya kiuchunguzi. Ukweli unayejiita Dr Aluta huifahamu Buguruni na uhalifu unaofanywa(uvunjwaji wa sheria na maadili). Nimebahatika kufanya mahojiano ya ana kwa ana na ndugu,jamaa na rafiki wa Hamisi. Pia nimechunguza maeneo yote korofi na kufanya mahojiano ya kina na wahusika na kuridhika pasipo shaka Buguruni ni sehemu maarufu kwa uhalifu kama wizi,ujambazi,ukabaji,chabo,madawa ya kulevya,bangi,utumiaji na uuzaji wa pombe haramu,ukahaba,chuma ulete n.k. Mimi sijasimuliwa na mtu habari hiyo bali nimeifuatilia mpaka mwisho wake. Kwa kweli wanaokaa Buguruni chukueni tahadhali .

we mwandish feki, unamfuatilia mtu hata jina kamil humjui. eti umeacha shughul zako, kweli!!?
 
Sherehe wiki nzima halafu tunalalamika ni kwanini sisi ni masikini.

Imaaaaagineeeee.....
Halafu siku mbili karudi home ndoa imemshinda....
Au ana papuchi ya dhahabu...lol..wat is so special..kupigia watu kelele tu na hapo ngono lzm itawale kwa wakeshaji
 
by Dr Aluta;
ninachotetea jamaa hakuwah kuwa panya road.

Dr Aluta, wewe umejuaje hakuwa panya road??

Au wewe ni mwanachama wa panya road!

cc suleyman kova.

mkuu mi siongei kishabik wala cwafaham hao panya road
 
Last edited by a moderator:
Majirani bana, wakiwa wanaambulia pilau na sambusa basi watamsifia mtu hata kama ni jambazi....njaa mbaya sana, JAMBAZI, MUUZA UNGA NA PANYA RODI WOTE WAHALIFU TU!

hiv kama ningemsif ningethibitisha kama ye jambaz acha akil za viroba.
 
ninachotetea jamaa hakuwah kuwa panya road.
Mimi sijui tafsri ya panya road lakini huyo unayemzungumzia yaani Hamisi Kumba alikuwa kibaka huko buguruni,sema baada ya baba yake mzee kumba kufariki ndio kidogo alipunguza matokeo ya wizi.Long time kidogo alikoswa kuchoma moto huko huko buguruni.
 
Haya mapanya road yalifika mpaka huku tabata yakiwa na kila aina ya silahaa hasa za kijadi.
 
# Dr.Aluta Endelea Nastory Mkuu Sisi Watu Wahuku mikoani Tunakufuatilia Achana Nawatu Wa Dar Wajuaji Sana!

Mkuu mbona Dr amemaliza kuwa mshkaji alipigwa risasi supermarket SA na alikuwa jambazi
 
Mimi sijui tafsri ya panya road lakini huyo unayemzungumzia yaani Hamisi Kumba alikuwa kibaka huko buguruni,sema baada ya baba yake mzee kumba kufariki ndio kidogo alipunguza matokeo ya wizi.Long time kidogo alikoswa kuchoma moto huko huko buguruni.

hauko mbal na ukwel, jamaa alikua mtu wa matukio. ila hakutaka kuchomwa moto.
 
Haa haaa ila alikuwa jambazi? Kuna watu mnavipaji vya kuchekesha

mkuu hiv panya road na jambazi wako sawa? tena ujambaz hafanyii bongo. ila panya road harakat zao ni ndan ya nchi. sasa connection iko wap?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom