Buguruni: Sherehe yageuka msiba

Buguruni: Sherehe yageuka msiba

Dr Aluta

Senior Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
121
Reaction score
39
Kilichofanya niweke bandiko ni mambo mawili, kwanza kueleza tukio husika, pili kuna mleta mada anayejiita Grader kapost uongo kutokana na hiki ntakachoandika, amemsingizia huyo marehemu Panya road azikwa kifahari Buguruni kisiwani, pili amesema Buruguni ni kitongoji chenye kila aina ya laana! Kweli? Hivi mtu humjui hata jina, umri wake wala maisha yake unaazaje kumkashifu mtu.

Then unakashifu eneo husika unadai kuna kila aina ya ufedhuli na vijana wake wamepotoka, ina mana wakazi wa Buguruni wote hatuna maana? Au mwenzetu anaishi peponi?

Stori kamil ilikuaa hivi; Jumapili ya tarehe 31 mwezi Mei mtaani kulikuwa na sherehe, kuna binti anaitwa Zena alikuwa anaolewa, huyo Zena na marehemu walikuwa mtu na mjomba wake na ilipangwa tarehe 5 Ijumaa, marehemu arudi ili aje kufungishwa ndoa.

Hivi panya road anaweza kusubiriwa toka Sauzi aje bongo kufungisha ndoa? Tena anakuja kwa ndege? Bahati mbaya Jumatatu bongo wanamfanyia kitchen party Zena kule mjomba wake anapigwa risasi akiwa supermaket.

Baada ya kupewa ripoti Jumanne asubuhi walilia na sherehe ikawa basi!

Itaendelea part 2

=> Part 2
Kiukwel ilipangwa sherehe bab kubwa ifanyike pale mtaani. Sherehe ilipangwa ifanyike wiki nzima kuanzia tar 31 May had tar 7 June. Jumapili paliwekwa ngoma, Jumatatu usiku ikafanyika kitchen party lakini kwa bahati mbaya tulipokea taarifa zilizostua mioyo ya wengi pale tulipoambiwa kaka yao mkubwa anayeitwa Hamis ametutoka duniani.

Alifariki kwa kupigwa risasi akiwa supermarket nchin Afrika Kusini, taarifa ambayo ilizima chereko pale mtaani na kukatisha ratiba ya sherehe iliyosalia ambayo ilitakiwa Jumatano ipigwe baikoko, Alhamis upigwe mnanda, Ijumaa ipigwe taarab live band kutoka kwa mashauzi Classic na Jumamosi wamalizie na rusha roho kisha Jumapili waende ukumbini kwa ajili ya harusi lakini mambo hayakuwa hivyo sherehe yageuka msiba!! unajua chanzo cha marehemu kuuawa?

Ungana nami sehemu ya tatu.

Chanzo: Mimi ni jirani yao.

Poleni sana, hata mimi nilishangaa panya road kafikaje South.
 
Ingawa hujaweka bayana historia ya marehemu kabra.huwenda aliishawahi kuwa panya road.huwenda.

Poleni sana wafiwa.
 
Kiukwel ilipangwa sherehe bab kubwa ifanyike pale mtaani. Sherehe ilipangwa ifanyike wiki nzima kuanzia tar 31 May had tar 7 June. Jumapili paliwekwa ngoma, Jumatatu usiku ikafanyika kitchen party lakini kwa bahati mbaya tulipokea taarifa zilizostua mioyo ya wengi pale tulipoambiwa kaka yao mkubwa anayeitwa Hamis ametutoka duniani.

Alifariki kwa kupigwa risasi akiwa supermarket nchin Afrika Kusini, taarifa ambayo ilizima chereko pale mtaani na kukatisha ratiba ya sherehe iliyosalia ambayo ilitakiwa Jumatano ipigwe baikoko, Alhamis upigwe mnanda, Ijumaa ipigwe taarab live band kutoka kwa mashauzi Classic na Jumamosi wamalizie na rusha roho kisha Jumapili waende ukumbini kwa ajili ya harusi lakini mambo hayakuwa hivyo sherehe yageuka msiba!! unajua chanzo cha marehemu kuuawa?

Ungana nami sehemu ya tatu.

Chanzo: Mimi ni jirani yao.
 
Kwenye hii sehem ntaeleza maisha ya marehem kwa ufupi.jina kamil la marehem anaitwa Hamis Omary Kumba. ni mtoto wa pili kati ya 8 katika familia ya mzee kumba.Jamaa alikua ni mtu wa miraba minne.alikua jasiri, asiyekubal kushindwa, mtetez wa wanyonge mtaan.mpaka anafariki marehem ameacha mtoto mmoja wa kiume anaeitwa siyabonga mwenye umri wa miaka 15.Baada ya kuona bongo maisha yanampiga chenga, mnamo mwaka 2009 akaamua kufunga safari kwenda kwa mdogo wake sauz(panya road ishaanzishwa?), ambae yupo huko tang mwaka 2001. mdogo kimaisha alikua safi tu. mpaka anafarik alirud nyumban bongo mwaka 2013. sehem ya 4 ntaeleza tukio mpaka anapoteza uhai wake na maisha yake kwa ujumla akiwa sauz. USIKOSE
 
Dr Aluta

Kiongozi weka habari yote kieleweke, punguza mbwembwe basi kwasababu hii ni habari ya kifo, ni vema tukaujua ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Kubali kataa wabongo wengi walioko south ni vibaka na majambazi dili zao za wizi na unga. Haya endelea kumtetea huyo jamaa yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom