hakuna jambo linalonihuzunisha maishani mwangu kama hilo.huwa nikipita hapa Sinza Mori jioni kuelekea kwangu,inabidi nipite upande wa pili wa barabara ili nisikutane nao maana sometimes wanakuwa wamechacha haswa hawana hata ya kula,wakikukaba?Ila kinachoniuma zaidi ni viongozi serikalini, hususani vitengo katika wizara husika,Je!wamefika ukomo wa kimawazo kuhusu suluhu ya jambo hili? wengi wao huanzia huku kwenye uchokoraa(sorry kwani hilo jina pia sio zuri) na viongozi wanawaona tangu wakiwa watoto wa mitaani, hadi kufikia hatua ya kuamua kujiuza kwani huku kwenye maisha yao hayo wamezoea kubakwa na kufanyiwa kila aina ya unyama!This is so bitter kwa kweli!Ifike mahali sasa hata katika Chaguzi zijazo, haya mambo yawe Addressed ipasavyo!Kiongozi asiyekubali haya matatizo kuwa katika ilani yake ya uchaguzi, basi tusimpe kura kabisa!Pia asasi za kiraia ziko wapi?mashirika ya kutetea haki za watoto na wanawake yako wapi?Au ndo yamekuwa chanzo cha mapato kwa wajanja?
INAUMA KWA KWELI!!!!!!!!!!TUSEME HAPANA, IMETOSHA!!!!!!!!!!!!!!