johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 718
- 703
Wadau.
Nimeandika mara tatu hapa juu ya mambo yasiyofaa ambayo yanaendelea katika hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyoko jijini Mwanza, ingawa hoja hizo hazijapata majibu na pia kwamba sitarajii kupata majibu, nafikiri kuna haja ya kuendelea kueleza uozo huo ili tu uweze kufahamika kwa wengine.
Alhamisi ya wiki iliyopita, mgonjwa wangu aliyelazwa katika moja ya wadi iliyoko ghorofa ya nane, aliandikiwa aina mbili za dawa: Neurobion na Erythromycin( sina uhakika kama nimeziadika ipasavyo), lakini aliagizwa kwenda kununua, kwa kuwa hazikuwepo hospitalini hapo!
Ndani ya Hospitali kuna duka la dawa ( Pharmacy) ambapo ukikosa dawa ndani unakwenda nje na kukuta dawa unazohitaji! Naambiwa kuwa duka hili pia ni mali ya Hospitali> hospitali hiiyo isiyokuwa na dawa katika eneo moja inayo dawa hiyo hiyo, katika kitengo kingine!
Labda hiyo sio shida, Ndani ya duka hilo nilikuwakuta vija a wawili, wakiume na kike, ambapo dada aliyekuwa ndani baada ya kuona karatasi yangu ya dawa aliandika kuwa Dozi ya Erythromycin, inauzwa shilingi 9000, huku Neurobion ikiuzwa kwa shilingi 14000. Jumla kuu inatakiwa shilingi elfu 23.
Wakati natafakari juu ya gharama hiyo, mtu mmoja aliyekuwa jirani, aliniambia kuwa gharama za dawa katika duka hilo ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 100 kuliko maduka ya mjini.
Nilikwenda Kayonza Pharmacy ambako dawa zote ambili nilizoambiwa kuwa Bugando zinauzwa shilingi 23000, Kayonza nilizipata kwa shilingi 4000!.
Mambo ni mengi lakini hiyo ndio Bugando