Bugando mtatuulia watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bugando mtatuulia watoto

Discussion in 'JF Doctor' started by mbutalikasu, Apr 28, 2012.

 1. m

  mbutalikasu Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani nisaidieni hawa madaktari wa Bugando wanaohusika na upasuaji wa watoto waliovimba vichwa wamejaa ubinafsi tu, kuna watoto wamelundikana katika vitanda wanalala 3 kila kitanda, wazazi wamepewa ahadi za kufanyiwa upasuaji tokea januari hadi leo hawajafanya hivyo ukienda jibu unalopewa ni kwamba mipira ya kuwawekea haipo jamani waoneeni huruma hawa watoto hawakupenda na walla wazazi wao hawakupenda. MUNGU wawekee watoto hao mkono wako waweza kupona
   
 2. R

  Ray2012 JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  huenda mgomo unaendelea!
   
 3. m

  mbutalikasu Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani madaktari hebu tusaidieni hili waoneeni huruma hawa watoto hawana hatia yoyote watibuni kama vifaa havipo iambieni serikali kuwa nyie siyo wapiga ramli mnatumia vifaa jamani, maskini mtoto wangu anakufa bugando
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  pole sana, tatizo si madaktari ni serikali yenyewe haipeleki vifaa kwa wakati. Ndio maana CT scan machine ya bugando haifanyi kazi muda mrefu
   
 5. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  swala la bugando na iyo wodi ya na.9 wala sio vifaa tu ni rushwa imetawala.daktari atakwambia hakuna vifaa lakini ukinyoosha mkono ukamuahidi laki mtoto atapasuliwa siku iyo iyo
   
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  mbona mnarudia yaleyale tuliyoyapigia kelele mkatutukana.? Mirija hakuna,tuwawekee mabomba ya umeme? Vitanda hakuna,tukawalaze kwetu? Tatizo la siasa za mpaka kanisani ndo hilo. Tulisema mkatuambia siye wabinafsi, sasa hivi tunafukuzana na hela tu. Pesa zenu acha wabunge waende kupondea raha na vimada wao india. Hivi mnajua kwamba mbunge anapokwenda india na mkewe wanalipwa kwa siku wote wawili kwa kodi zetu hata kama mke siyo mtumishi wa serikali?
   
 7. m

  mbutalikasu Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lakini kwanini ifikie hiyo hatua kwamba kuokoa maisha ya mtu mpaka upewe rushwa? Basi watufanyie ss watu wazima siyo watoto kama wale. Halafu uongozi wa hospital unaliona hilo nao upo kimya tu mie nahisi kama ni rushwa wanayokula wametumwa na dokta mkuu wa bugando ''ila dawa yao inachemka nitakuja nimshikishe mmoja awe kuku wa kafara''
   
 8. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  baada ya hiyo operation ya hydrophism wanapona?
   
 9. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  mkuu hapo nakugongea like... hilo ulilosema ndilo la muhimu, mie nipo hospitali isiyo na chumba cha upasuaji zaidi ya mwaka na ni hospitali ya mkoa, gharama ya kuikamilisha na vifaa ni 6 Billion, lakini chaguzi ndogo gharama ni 19Billion sasa serikali yetu inawajali wananchi?? kila mgonjwa anayekuja na anahitaji huduma ya upasuaji inabidi kumpeleka hospitali ya KCMC rufaa na huko analipa gharama za kutosha, tatizo la dakatari hapo sijaliona na ninadhani ni muda sasa wananchi wakaelewa yanayojiri badala ya kulaumu madaktari
   
 10. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  watu huwa wanakuwa negative sana khs wafanyakazi wa hospitali zetu. ni kweli sometimes wafanyakazi huwa wana makosa lkn kwa bahati mbaya sana watu hawaangalii kiini cha tatizo ni nini na badala yake wanakuja kugeneralize vitu wasivyovijua. Tukianza kuongea matatizo ya MSD watu wanabadili channel matokeo yake ndio haya ya mawazo ya mbutalikasu.
   
 11. m

  mbutalikasu Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka tatizo lipo pale unapoona leo anafanyiwa mmoja operation ukiuliza vifaa vimekuja unaambiwa kuwa bado ukiuliza mbona huyo kapata tiba hawakupi jibu sahihi halafu huo uongozi unalicgukuliaje suala la kukaa na mgonjwa miezi mitatu kitandani bila tiba kwanini wasiwaambie waende kwao warudi cku zijazo mtu unakaa hospital miezi 3 bila tiba basi watwambie kuwa bugando hakuna pelekeni muhimbiri tujue moja na hao MSD nao wamwogope MUNGU PIA
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  pole sana mzazi,inauma sana kama unaweza ukaongea na madaktari ununue vifaa mwenyewe wamtibu mwanao kunusuru maisha yake,SI SAHIHI LAKINI UTAFANYAJE NA MTOTO ANAHTAJI HUDUMA HARAKA
   
Loading...