BRT Kimara Terminal: Abiria walala chini kuzuia basi lisiondoke tupu

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Kama kawaida kadhia kubwa ya usafiri imeleta mtafaruku baada Magari kugeuza tupu na kuacha abiria.

Picha imemfuma abiria aliyelala chini kuzuia Gari zisipite.

IMG_20231128_125339.jpg
 
Kama kawaida kadhia kubwa ya usafiri imeleta mtafaruku baada Magari kugeuza tupu na kuacha abiria.

Picha imemfuma abiria aliyelala chini kuzuia Gari zisipite. View attachment 2827373
Hao BRT kiukweli kabisa wameshindwa kuundesha huo mradi.....wawape tu sekta binafsi wawasaidie kuundesha, Yaani hao BRT hata wakipewa kampuni kama Abood ama Bm bado watafeli tu
 
Kama kawaida kadhia kubwa ya usafiri imeleta mtafaruku baada Magari kugeuza tupu na kuacha abiria.

Picha imemfuma abiria aliyelala chini kuzuia Gari zisipite. View attachment 2827373
hivi huu mradi kuundesha kama inavyotakikana kila baada ya dakika tano gari itoke kituoni haiwezekani kabisa kwa sasa?

Utaratibu wa huo mradi uko hivyo kwa nini hawausimamii huo utaratibu wa hizo dakika?

Watu walioenda israel mwaka 2017 ndio hiki walienda kujifunza?

wale wazee walienda Bogota (Colombia) ndio hiki walienda kujifunza kuja kutesa wananchi?

Mkandarasi mwenye mradi aliweza kuonesha mfano wa kutumia dakika 40 kwa kimara gerezani na dakika 45 kimara kivukoni na inawezekana sana sasa shida ni nini kwa hawa wasimamizi?

Ni kweli hatuwezi kufanya marekebisho ya hayo magari kwa sababu hayaleti faida ama pesa inaenda mifuko mingine?

Eng. nakuaminia na falsafa yako ya punctuality time inawezekana kabisa hebu hili lifanyike acheni kusema magari yakizunguka mengi kwa wakati mmoja mnapata hasara hii sio dhima ya mradi turudishieni utaratibu wa mwanzo wa mradi mliweza kwa kiasi fulani kuleta mstumaini shida ni nini kwa sasa?.

Warudisheni ata hao Maxcom kwenye huo mfumo ambao umekwama mpaka sasa huo wa kadi na hizo mashine zilizonunuliwa kwa pesa nyingi na kisha kuishia kufanya kazi kwa miaka miwili tuu, haya ni matumizi mabaya ya fedha za uma.

Tunajidhalilisha sana kwa kuukimbilia huu mradi huku vichwa vyetu bado vinawaza kidadala.

Hivi ile tuzo mliopewa mwaka ule mnadhani kwa sasa mnastahili ata kidogo kuweza kufikiriwa kuwa mnaaminika kwa hizi huduma za sasa?.

Nasikitika sana kuona kila msimu wa mvua ni dart kutoa tangazo za kusitisha huduma kwa njia ya morogoro hasa hapo jangwani na mkwajuni hamuoni aibu kweli?.
 
Yale mabasi nadhani ni ya mtu binafsi, DART sijui UDART wao wapo kupewa percent yao tu sababu miundombinu ni ya serikali...
yalikuwa ya Robert Kisena na wamiliki wengine wa daladala kwa share kadhaa na sasa ubia ni serikali kwa asilimia kubwa tuu kupitia UDA (usafiri dar es salaam)
Nikipata muda nitaweka hapa asilimia za seriakli ni ngapi kwa sada na hao Udart ni ngapi ila kwa sasa mwenye hisa nyingi ni serikali na ndio maana kwa sasa mkurugenzi nadhani wamemtoa huko Latra.
 
Anatafutwa mwekezaji mwenye maslahi Kwa walengwa sasa huyu wa sasa lazima afelishwe watu wazame Wazima Wazima,,na nimeona Leo Mkuu wa Mkoa wa dar kaingia mkataba Fulani wa awali na wachina kuhusu uboreshaji wa Jiji(metropolitan city)
 
Back
Top Bottom