Broiler sio kuku wa kula kabisa!!

Kwa sisi tuliokulia nyumba zinazofuga nguruwe supu tumekunywa ni tamu hasa supu ya kongoro
Mimi nilikuwa nimezoea kitimoto cha kukaanga, rosti na choma baadaye nikaja kukutana na cha kuchemsha na kilikuwa poa tu, sema cha kuchemsha kama supu au kupikia kwenye ndizi/viazi mchemsho kinakuwa vizuri kama hakina mafuta mengi.
 
Mkuu umekasirika sana mpaka tunashindwa kukuelewa, humalizi sentensi kabisaaaa
 
Sasa kijijini broiler watatoka wapi?! Hata vijiji ambavyo chips mayai zinapikwa upate na mayonnaise, ukwaju, chachandu na tomato sauce si vinahesabika.
Halafu sio kwamba vijana wa mjini huwaambi kitu kuhusu broiler, ni kwamba broiler ni bei rahisi, walaini wakikaangwa au kuchomwa na ndio wanaopatikana.
 
Hawana baba wala mama? Nanwewe jamaa yangu li roho tu! Hao nani alikwambia wanaliwa supu? Kukiwa wiki 4 -6 anafaaje kwa supu?
 
Bodaboda huita "Boila"
 
Boss broiler ni kuku tu kama kuku wengine,ana baba na mama.
Kuku wa kienyeji akitaga yai ukatotolesha kwenye mashine wakaenda fugwa kwingine naye utasema hana baba wala mama?

Broiler ukimfuga kwa kumuacha ajitafutie chakula kama kuku wa kienyeji atakua taratibu tu na nyama itakomaa,atafikisha miezi 6 akipandwa anataga kama kuku wa kienyeji.
 
Vijana wa mjini wanajiendekeza tu kula vyakula vya hovyo kwa afya, suala la gharama halina mashiko kivile. Bei ya kuku wa kienyeji ni ndogo na uoatikanaji wake ni rahisi zaidi ya piza lakini kijana yupo tayari anunue pizza.

Nakumbuka wakati nipo chuo nikifika kwenye mgahawa chakula changu kilikua ugali dona, dagaa mixer nyanya chungu bamia na mboga za majani. Wakati wengi vyakula vyao vilikua chipsi mayai na soda wakati bei zinalingana tu
 
Unapoanza kulinganisha kuku na pizza ndio unapotea njia,
 
Hujawai Kula kifaranga cha kuchemsha .kinachemshwa na manyoya unapata juice
 
Nimefanya rejea ya mfano wa gharama ambao wewe umesema kwamba ni moja ya sababu vijana kukimbilia kula broiler.
Hivi kuna mwanafunzi wa chuo anayetegemea boom la serikali anayeza kuishi kwa kula kuku wa kienyeji au pizza??
 
we hebu sema unatania basi,,,yaani supu ya kitimoto inanyweka vizuri kabisa,nipo naitafakari hio radha....
Yah ina viungo maalumu na majan fulani yakiwekwa kwenye hiyo supu huto acha nimeona kwa wachina hii.
 
Kataa broiler kataa watoto wasio na baba( mayai).....Afrika tunajiletea janga kula mayai ya kisasa
 
Hivi kuna mwanafunzi wa chuo anayetegemea boom la serikali anayeza kuishi kwa kula kuku wa kienyeji au pizza??
Hata akiwa na uwezo hawezi kula kila siku maana kuna kukinai. Tunaongelea hizo hizo mara moja moja
 
Amjui kuwapika....mnapika shombo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…