Lady Ra
JF-Expert Member
- Mar 23, 2014
- 879
- 988
Wadau kwema?
Jana nilimtembelea mdogo wangu mmoja ambae yuko nyumbani kwa sasa (Hana kazi) kwa sababu zake za kibinafsi. Basi katika story za hapa na pale akanionyesha kwenye Laptop yake kua ameomba kazi sehemu mbali mbali kupitia mitandao mbali mbali.
Mojawapo ya Mitandao alioomba ni hawa BRIGHTER MONDAY. Amenionyesha mahali ambako kuna meseji ametumiwa lakini hawezi kuzifungua mpaka aji-upgrade kwenda Premium Package. Na Upgrade hiyo inahitaji kulipia Tshs 33,000/= kwa mwezi kwenda kwa hao Brighter Monday. Wasiwasi wake ni kua pengine hizi meseji alizotumiwa ni kutoka huko kwenye makampuni alikoomba kazi.
Lakini nimewaza inakuaje mtu kuiona meseji zake mpaka azilipie ili awe Premium? Yaani ni sawa na hapa JF ukitaka kuona PM zako basi inabidi ulipie, hii imekaaje? Ina maana kama ni kweli amejibiwa na huko alikoomba na anatakiwa ahudhurie Interview si ndo hatofahamu sasa? Kwanin basi wasingeweka hii toka mwanzo kua meseji zinalipiwa?
Binafsi naona kama huu ni utapeli kwa kivuli cha ajira, maana hata hizo meseji zenyewe huwezi kujua ni zipi, zimetoka wapi na zinahusu nini, unaweza kulipia ukakuta hata ni Matangazo ya Biashara ya watu. Pili nature ya mtandao wenyewe ni watu ambao wanatafuta ajira, pengine mtu hana hiyo hela ndio anatafuta ajira, sio sawa hii.