Brela acheni jeuri na ucheleweshaji wa huduma kwa makusudi!!

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,358
2,000
Habarini,
Hili la watumishi wa brela kuwa jeuri na kuchelewesha usajiri kwa makusudi kwa njia ya mtandao imekuwa kero sana kwetu.

Mtu unatafuta jina halafu unaandaa nyaraka zote muhimu wanakwambia ulipie unalipia kisha wanasema jina lako linafanana na majina mengine rekebisha unarekebisha baada ya hapo hawapokei simu j3 hadi ijumaa jioni wakipokea wanakwambia angalia tayari wameshughulikia kumbe bado na ukiwakumbusha wanakwambia huduma ni ndani ya siku tau hasa watu wamsaada kwa isajiri wa makampuni.

Pia kuna tabia ya kudai Brela ndiyo wenye mamlaka ya kusajiri au kutosajiri kampuni kitu ambacho kinawapatia jeuri sana na kujiona miungu watu.

Nashauri Brela nao wafanye kazi masaa 24 ili kuboresha huduma na uharaka wa kusajiri majina ya biashara na makampuni kwani kuchelesha usajiri ni kuchelewesha ukusanyaji kodi.
 

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,358
2,000
Pale kuna watu wana jeuri na kiburi sana
Kuna hizi namba za msaada kwa wateja 0735331001 na 0735331003 hazipokelewi na muda mwingi hazipatikani na akipokea kuna dada mmoja ambaye ndiyo hupokea simu 0735331001 mara nyingi atakuomba tracking number yako kisha utajibiwa kwa ukali ile mbaya kuwa "tunashughulikia" kuanzia hapo ndiyo umejiroga hutoshughulikiwa tena hadi ijumaa saa 9.25 jioni
 

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,358
2,000
Marekekebisho ni muhimu na haraka,wakipokea simu wataje majina yao kama ilivyo kwenye kampuni za simu huduma kwa mteja ili iwe rahisi kudeal nao au wawe wanabadilishwa mara kwa mara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom