Leseni na huduma zote za BRELA kwa njia ya Mtandao

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1573722913580.png


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Emmanuel Kakwezi amesema kwamba, moja kati ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Joseph Pombe Magufuli ni utoaji wa huduma zake zote kwa njia ya mtandao.

Bw. Kakwezi ameyasema hayo akiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo.
Ameeleza kwamba Wananchi wanaweza kuwasilisha maombi ya huduma zote zinazotolewa na BRELA popote pale walipo nchini kwa Mfumo wa Usaili kwa njia ya mtandao, (Online Registration System / ORS).

“Hivi sasa maombi yote ya Usajili yanatumwa kwa njia ya Mtandao, iwe ni Usajili wa Kampuni, Usajili wa Jina la Biashara, usajili wa Alama ya Biashara au Huduma, utoaji wa Leseni za Viwanda, utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na utoaji wa Hataza” amesema Bw. Kakwezi.

Bw. Kakwezi ameongeza kwamba Mabadiliko haya yanaambatana na faida nyingi, ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa kufanya usajili, mathalani usajili wa Kampuni hivi sasa unaweza kukamilika ndani ya siku moja.

Mfumo huu uwasaidia watumiaji kutuma maombi yao popote pale walipo nchini nan je ya nchi vilevile.

Zaidi ya hilo mfumo huu unamsaidia mtumiaji kufuatilia maendeleo ya maombi yake na kupata mrejesho kwa ajili ya kufanya marekebisho pale maombi yanapoonekana kuwa na kasoro.

Aidha katika kipindi cha miaka minne, BRELA pia imefanikisha uanzishwaji wa Shahada ya Uzamivu ya Miliki Ubunifu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shirika la Miliki Ubunifu la Kanda (ARIPO) na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO).

Mpango huu una lengo la kuongeza elimu kwa Umma na wataalam katika eneo la Miliki Ubunifu. Shahada hiyo ya Uzamivu imeanza kutolewa mwezi Agosti 2019.

BRELA kwa kushirikiana na COSTECH pamoja na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) imetekeleza mradi wa Upatikanaji wa taarifa za teknolojia zilizopo kwenye kanzidata za Hataza (TISCs) kwa ajili ya kutumiwa na watafiti na watumiaji wengine ambapo jumla ya Hataza milioni sabini na sita (76,000,000) zinaweza kupatikana kwenye kanzidata husika.

Katika kipindi cha Miaka minne, BRELA imefanikisha kuanzisha Utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na kundi B kwa njia ya mtandao. Mfumo huu umeunganishwa na Mifumo ya Malipo ya Serikali yani Government Electronic Payment Gateway (GEPG) na Mfumo wa Taarifa za Makusanyo

ya Mapato wa Mamlaka za Serikali za mitaa yaani Local Government Revenue Collection Information System (LGRCIS).

Majaribio ya Mfumo huu yalianza tarehe 1 Oktoba 2019 na mpaka sasa Leseni za Biashara Kundi A zinazotolewa na BRELA na Leseni za Biashara kundi B katika Manispaa za Bukoba, Chalinze, Wilaya ya Karagwe,Mji wa Mafinga, Manispaa za Ilala na Halmashauri za Jiji la Mwanza zinatolewa
kwa njia ya Mtandao.

Katika utoaji wa Leseni kwa mfumo huu takwimu zinaonesha jumla ya Leseni za Biashara 1206 zimetolewa kupitia mfumo huo ambapo kati ya hizo BRELA imetoa Leseni 470, Jiji la Mwanza Leseni 199 na Manispaa ya Ilala Leseni 537.

Bw. Kakwezi ameeleza zaidi kwamba ndani ya miaka minne BRELA imefanikiwa kuanzisha dirisha la Mfumo wa utoaji wa taarifa za Kibiashara za Kimataifa. Dirisha hili linamuwezesha mtuamiaji au mwombaji kufahamu taarifa mbalimbali za upatikanaji wa Leseni na vibali kwa bidhaa zinazouzwa nje na zinazoingizwa ndani ya nchi.

Dirisha hili linatoa fursa kwa mwombaji kutembelea tovuti ya www.trade.business.go.tz na kupata taarifa zote za Biashara zinazohusiana na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi (Export) na uaigizaji ndani ya nchi (Import).

Vilevile mtumiaji atafahamu Sheria, Kanuni, taratibu muda utakaotumika pamoja na gharama za kila aina ya huduma (Administrative procedures) atakayohitaji na wapi apite ili kufanikisha upatiakanaji wa huduma anayohitaji.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ilianzishwa chini ya sheria ya wakala wa serikali namba 30 ya Mwaka 1997 na hatimae kuzinduliwa rasmi tarehe 3 mwezi Disemba 1999.

BRELA ipo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na ilianzishwa kwa ajili ya kuratibu shughuli za biashara na kudhibiti sheria pamoja na utoaji wa huduma za Usajili wa Kampuni, usajili wa majina ya biashara, usajili wa alama za biashara na huduma, utoaji wa leseni za viwanda, utoaji wa leseni za biashara kundi, utoaji wa Hataza na Miliki bunifu.
 
Back
Top Bottom